Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,849
- 7,014
Natumaini mu wazima humu, ni siku nyingine tukiwa bado tunasubiri muafaka wa mchezaji Kagoma kama atabaki Simba au atarudi Yanga, Mzee wetu magoma na yeye ni mpaka kieleweke !!,
Anyway tukirudi kwenye kichwa cha habari, Ujerumani imekubali kuwapokea Wakenya 250,000 na kuwapa nafasi za kufanya kazi nchini humo.
Makubaliano hayo yamefikiwa kati ya Rais William Ruto na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Makubaliani ni kuingiza experts sio vibarua, kundi la kwanza ni skilled workers (mfano wahandisi, it, wahasibu, madaktari, walimu, n.k), kundi la pili ni semi skilled workers (mfano madereva, wapishi, reception, store keeper, n.k)
Tayari madereva Watano toka Kenya wamefika kwenye mji wa Flensburg Ujerumani kupitia mpango huu. (Maderva hulipwa wastani wa euro 14 / shilingi elf 42 kwa saa)
Lugha kuu ujerumani ni kijerumani lakini asilimia 56 ya watu Ujerumani wanaweza kuongea kiingereza, ni sawa na kwenda Uganda unaweza usijue lugha yao ya kiganda lakini ukijua kiingereza inasaidia, inakuwa rahisi zaidi kujifunza kijerumani taratibu unapojua kiingereza.
Faida..
- Fursa za kujiongeza kielimu na kupata kazi zenye mishahara ya kizungu (Mwalimu analipwa milioni 8 kwa mwezi)
- Kupunguza tatizo la wahitimu wengi wasio na ajira Kenya, hata kwenye ajira za kiswahili mfano walimu wa kiswahili na watangazaji wa vituo vya Idhaa za Kiswahili kama BBC na DW, wakenya ni wengi na wanaenda kujazana zaidi.
- Baadhi ya pesa wanazopata ujerumani zinarudi Kenya, mfano mdogo kutuma euro 500 nyumbani kila mwezi, ni kiasi kidogo ujerumani lakini kwetu ni shilingi milioni 1 na nusu, ni ada ya mwaka mzima chuoni, si haba ni mtaji wa kuanza biashara , n.k.
- Kupata connections za biashara za kimataifa, Mfano kununua maparachichi Tanzania kwa mia mbili, kuyauza ujerumani kwa elf 5.
- Diaspora inazidi kupanuka, baadhi ya sehemu kunakuwa na vijiji / mitaa iliyojaa wakenya
- Inakuwa rahisi kwa wakenya kuingia ujerumani wakiwa na ndugu, marafiki na jamaa waliojaa nchini humo.
- Wakenya kupata fursa za kutumia vipaji kupata pesa zaidi, Kuna vijana wadogo ujerumani wanacheza mpira wanakunja milioni 200 kila wiki.
- n.k.