Pre GE2025 Wakala wa Vipimo nchini (WMA) washukuru Rais Samia kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya kazi pamoja na kutoa stahiki za kifedha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,013
1,634
Wakala wa Vipimo nchini WMA umeandaa Iftar kwa lengo la maombi na Dua ya ufunguzi wa jengo jipya la ofisi baada ya kukamilika kwa ujenzi wake Jijini Dodoma.

Iftar hiyo iliwakuwakutanisha wadau mbalimbali, watumishi wa Ofisi hiyo, Viongozi wa Dini na Viongozi wa serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu tawala Mkoa wa Dodoma. Coletha Kiwale ambaye ni Katibu tawala msaidizi amesema kukamilika kwa jengo hilo kutawezesha mazingira mazuri kwa watumishi na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma inasisitiza Wakala huo kuongeza tija na kutatua changamoto kwa walaji.

Kwa upande wake CPA Saleh Chondoma ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Vipimo amesema kuanza kutumika kwa jengo hilo kutachochea walaji (wateja) kupata vipimo stahiki bila kuwa na vitendo vya ukiukwaji wa sheria.

Nao Viongozi wa Dini ambao ni Askofu Antony Mnyashimba, Askofu wa kanisa la Baptist na Mwenyekiti wa madhehebu ya kikristo Dodoma, pamoja naye Shekhe Ahmad Said Msemaji wa Shekhe wa Mkoa wa Dodoma wamesisitiza Wakala huo kutenda haki na uimara katika Vipimo bila dhuluma ili Taifa kuepuka majanga na misiba isiyo tarajiwa.

 
Back
Top Bottom