Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Mungu anaangalia moyo wako na matendo yako na sio mavazi, angekua anaangalia mavazi basi magaidi wote wangeenda mbinguni maana huwa wanajifunika mpaka uso na macho

Tujitahidi kutenda matendo mema na kuweka mioyo yetu safi, unaweza kuvaa gauni refu panaaa kama gunia halafu usiku ni pakashume unaeruka na ungo...



Kikombe huoshwa kuanzia ndani lakini yapasa nje yake pia iwe safi.

Yani mtu aseme ameokoka lakini kimavazi ashindwe kuvaa Kwa kujisitiri?

Yani hata asieamini anajua kujisitiri sembuse mtu anayedai kuokolewa?!

Hapana!

Yatupasa kurejea kwenye misingi ya imani!
 
Watu hawataki kujikana nafsi zao na kujitwika misalaba na kumfuata Kristo.

Mtu anasema ameokoka lakini anapiga vimini kwa sana anashindwa na asieamini

Maandiko yameweka bayana kabisa kuwa “ mwanamke asivae mavazi yampasayo Mwanaume “ maana ni machukizo machoni pa Mungu lakini unakuta Mchungaji au mama Mchungaji anavaa, wanawake wanavaa Yani wengine utasema wanaenda night club

Tujifunze kujikana kwanza!
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Kwa hali ya kidunia ukikata mauno mwanaume na mkeo yupo kanisani nguo zikakuvuka
Je mkeo na waumini wa sasa watakuvumilia?
Tuanzie hapo kwenye imani
Ndo maana hata Sheria huwa na amendment au kanuni chukua hatua
 
Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa
Amosi 6:5-7 (ninyi mnaoimba nyimbo za upuuzi pamoja na sauti ya vinanda ................... Kama vile Daudi ................... Basi kwa ajili ya hayo sasa watakao kwenda utumwani na kelele za MACHEZO za hao walio jinyoosha zitakoma.
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Baada ya Daud kumuua Goliati watu waliimba na kucheza., bali walicheza kama matokeo ya furaha baada ya ushindi wa vita, na wala hawakucheza wakiwa kwenye hema Takatifu.

1 #Samweli 18:6-7 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.

Daudi baada ya kufanikiwa kulirudisha Sanduku la Bwana mahali pake, tunaona anacheza, #NOTE: Hakucheza Hekaluni na wala alipokuwa mbele ya Sanduku hakucheza ovyo bali alirukaruka tu kwa shangwe ; Ni kweli alicheza lakini alicheza kistaarabu na wala hapa hakujifunua nguo, Bali alikoenda kucheza hadi akajifunua nguo ni nyumbani kwake Na wala sio mbele za Sanduku la Bwana. Kwa hiyo kuna aina za uchezaji alizocheza Daudi

1. Aina ya uchezaji Mbele ya sanduku la BWANA: Daudi alipokuwa mbele za uwepo wa Mungu alicheza, lakini hakujifunua nguo yoyote, ina maana alicheza kwa Adabu na staha mbele za Mungu.

2 #Samweli 6:16-19 Ikawa, sanduku la Bwana lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za Bwana; akamdharau moyoni mwake.Wakaliingiza sanduku la Bwana, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabarikia watu kwa jina la Bwana wa majeshi. Akawagawia watu wote, mkutano wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake.
#NOTE: Program zote za kupokea sanduku zilimalizika salama na Daudi akawabariki watu salama na kila mtu akarudi nyumbani kwake, na wala haioneshi Daudi akijifunua nguo.


2. Aina ya uchezaji wa pili ni ule aliocheza akiwa nyumbani mbele ya wajakazi wake na si mbele za BWANA; Baada ya kumaliza program zote salama ndipo sasa Daudi wakati anarudi nyumbani kwake akaanza kucheza ovyo hadi kujifunua nguo.

2 #Samweli 6:20 Ndipo Daudi akarudi ili awabarikie watu wa nyumbani mwake. Na Mikali, binti Sauli, akatoka nje aende kumlaki Daudi, naye akasema, Mfalme wa Israeli alikuwa mtukufu leo namna gani, akijifunua mwili wake mbele ya vijakazi vya watumishi wake, mfano wa watu baradhuli mmojawapo, ajifunuavyo mwili wake mbele ya watu, asipokuwa na haya!
Uchezaji huu wa DAUD akiwa nyumbani ni tofauti na ule aliocheza mbele za BWANA na ndio maana Mikali akasema Daud anacheza mfano wa watu #BARADHULI,


Ukisoma Biblia yako yenye misamiati mwishoni mwa Biblia inasema #BARADHULI ni Mtu asiyefaa, au ni mtu #Mpumbavu sana.

Ina maana kwamba Daudi alivuka mipaka ya uchezaji wa siku zote na ndio maana hata mke wake alishangaa. Kwa hiyo na wale wanaocheza makanisani kwa kumuiga Daudi kwamba alijifunua hadi nguo nao ni MABARADHURI yaani ni #WAPUMBAVU.

Sasa aina hii ya uchezaji wa pili wa Daudi ndio uchezaji unaotumiwa na baadhi ya Wakristo ndani ya majengo ya ibada na ndio mtindo huohuo unaotumiwa na wacheza #Sengeli na #Bongofleva ambao hucheza hadi kujifunua nguo,ndani yake kuna viduku na unenguaji(kukata mauno).

Kwa hiyo hata wale ndugu zangu wanaosema wanacheza Makanisani kwa sababu Daudi alicheza hadi kufunua nguo wanakosea; Daudi alipokuwa mbele za Mungu hakucheza viduku, au kunengua na wala hakujifunua nguo, bali alipokuwa nyumbani ndipo alicheza hadi akajifunua nguo, kwa mantiki hiyo kama unamuiga Daudi kwa kucheza ovyo, basi hivyo viduku kachezee nyumbani sio Kanisani, maana hata Daudi alifanya hivyo pia na wewe jifunue nguo.

Lakini pia kwa wale wanaume mnaosema mnamuiga Daudi kwa kucheza basi nawaombeni mumuige Daudi pia kwa kutembea na wake za watu, maana Daudi alizini na mke wa Uria. Kwa hiyo si kila jambo ndani ya Biblia linahitaji utekelezaji hapana!! Kuna matukio mengine yaliandikwa ili kutuonya sisi tusiige,

1 #Wakorintho 10:11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.


Sasa kinacho sababisha watu kucheza ovyo ni kutokana na uwepo wa mrundikano wa vyombo vingi ambavyo vikipigwa hupelekea midundo yenye msisimuko wa mwili, Na ndipo sasa baada ya tukio hili la Daudi la kucheza ovyo hadi kujifunua nguo Mungu ikabidi atoe onyo juu ya vyombo vya musiki kwa wale wanaomuiga Daudi:


#Amosi 6:5 ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi;


Kwa hiyo kitendo alichokifanya Daud cha kupiga vyombo vingi vya musiki hadi ikampelekea kujifunua nguo Mungu hakukiafiki na ndio maana anaonya.
 
Kikombe huoshwa kuanzia ndani lakini yapasa nje yake pia iwe safi.

Yani mtu aseme ameokoka lakini kimavazi ashindwe kuvaa Kwa kujisitiri?

Yani hata asieamini anajua kujisitiri sembuse mtu anayedai kuokolewa?!

Hapana!

Yatupasa kurejea kwenye misingi ya imani!
Nakubakiana na wewe lakini Sasa mwanamke kuvaa suruali kuna ubaya gani, maana wengi wanaokujaga kanisani na suruali sio zile za kubana ni yale mapana ambayo hayaonyeshi maungo yao yao au suruali za vitenge au wengine anavaa suruali na kigauni juu
 
Asante kwa neno, nimebarikiwa sana
Licha ya kwamba tunamuona Daudi akicheza kwenye matukio mbalimbali, lakini katika suala la uimbaji ndani ya Ibada Daudi alikuwa makini na alipokea maelekezo kutoka kwa Mungu jinsi ya kuongoza kwaya ya Walawi, na hatuoni waimbaji hawa wakicheza kwenye Hema Takatifu wala Hekaluni, bali walisimama wakiwa na vyombo vyao waliimba kwa utulivu nyimbo za kumtukuza Mungu

2 #Mambo ya Nyakati 29:25 Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa Bwana wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani Bwana aliamuru hivi kwa manabii wake.
Hawa waimbaji hawakuimba wakiwa wanacheza viduku au kukatika viuno bali waliimba wakiwa wamesimama 2 #Mambo ya Nyakati 35:15 Nao waimbaji, wana wa Asafu #wakasimama mahali pao, kama alivyoamuru Daudi, na Asafu, na Hemani, na Yeduthuni mwonaji wa mfalme; nao mabawabu walikuwa katika kila lango; hawakuhitaji kuondoka katika huduma yao, kwa kuwa ndugu zao Walawi wakawaandalia.

KWANINI HAITAKIWI KUCHEZA NDANI YA MAJENGO YA IBADA?
1. Eneo la ibada sio sehemu ya kurukaruka kama Disko, ni mahali pa unyenyekevu palipotengwa maalumu kwa ajili ya mwanadamu kumuabudu Mungu na ndio maana tunatoka nyumbani kwenda kanisani. Kwa hiyo kinahitajika kicho.
#Waebrania 12:28-29 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;maana Mungu wetu ni moto ulao.
#Habakuki 2:20 Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.

2. Malaika wenyewe ambao ni watakatifu wanamuabudu Mungu kwa kuimba kwa unyenyekevu wakiwa wamefunika nyuso zao, na sio kwa kurukaruka:
#Isaya 6:2-3 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

3. Ikiwa unapoenda kwa Baba yako mzazi au kwa bosi wako kuomba msaada unaenda kwa unyenyekevu na kicho, inakuwaje kwa Mungu uende kwa kucheza viduku na kunengua, ambaye yeye Mungu ni zaidi ya baba yako,na ni zaidi ya boss wako?
#Malaki 1:6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?

4. Je kuna mtu ambaye Alisha wahi kwenda kwa mzazi wake au kwa Boss wake kuomba mahitaji Fulani na akaenda kwa kupiga kelele na kwa kuchezcheza viduku?
Kucheza ndiko kunawafanya watu waimbe nyimbo za matusi na za kipuuzi,kwa sababu asiliia kubwa ya nyimbo za siku hizi hazina ujumbe wowote, bali zinapendwa kwa sababu ya style za kucheza na midundo iliyomo, #Zaburi 47:7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili.
 
Mungu anaangalia moyo wako na matendo yako na sio mavazi, angekua anaangalia mavazi basi magaidi wote wangeenda mbinguni maana huwa wanajifunika mpaka uso na macho

Tujitahidi kutenda matendo mema na kuweka mioyo yetu safi, unaweza kuvaa gauni refu panaaa kama gunia halafu usiku ni pakashume unaeruka na ungo...
Mkuu weka ushahidi wa andiko hapa linalisema;

"Mungu anaangalia moyo wako na matendo yako na sio mavazi"
 
Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa
 
Nakubakiana na wewe lakini Sasa mwanamke kuvaa suruali kuna ubaya gani, maana wengi wanaokujaga kanisani na suruali sio zile za kubana ni yale mapana ambayo hayaonyeshi maungo yao yao au suruali za vitenge au wengine anavaa suruali na kigauni juu


Hii mada ya mavazi inahitajika mjadala mpana.

Neno la Mungu hali kuweka provision ya kuwa hilo vazi la Mwanaume likiwa pana basi itakuwa Sawa la hasha!

Imeandikwa: “ mwanamke asivae mavazi yampasayo Mwanaume “ maana ni machukizo machoni pa Mungu .

Hakuna provision yoyote kwamba iwapo yatakuwa mapana hayo mavazi ya kiume basi mwanamke akivaa itakubalika la hasha!
 
Huwa nashangaa sana mtu akitumia reference ya maandiko matakatifu kutetea ujinga na yuko serious kabisa
 
Daudi alifanya zaid ya yote.
Tusiwashikie sana mabanhgo ilihali sisi bado tu wachafu
 
Back
Top Bottom