Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,241
4,811
Ibada za pasaka zinaendelea; kwaya mbalimbali zinatumbuiza. Nimeenda kwenye kanisa mojawapo kusali naomba nisilitaje jina.

Waimbaji wananengua na kucheza mithili ya ngoma za kienyeji na kidunia.

Wengine wananengua miuno kabisa.

Sasa huku ni kumsifu Mungu kweli?
 
Ukitaka kuvuta watu popote pale
  1. Kata viuno
  2. Zungumzia mahusiano au mapenzi
Waimbaji siku hizi wananengua kwa mashindano si kwamba wanapeleka ujumbe wa Mungu ila wanawatega watu

Wahubiri wanaofuatiliwa na watazamaji au wasikilizaji wengi ni wale wanaozungumzia sana ndoa, mahusiano, tabia za mabinti nk

Wabunge nao wanapenda sana kuvuta attention za watu kwa kukatika kwenye mikutano ya kisiasa na kuzungumzia mapenzi bungeni

Viongozi wa kisiasa kadhalika ...rejea ukatikaji wa Kangi Lug mbele ya mkubwa wake wa kazi nk

Hospitali nako unakuta TV ikionyesha nyimbo za vitovu nje wagonjwa wanafunua blanket, wengine wanasukumia net pembeni
 
4AD51F70-2860-4CE2-AF3B-1832E923C973.jpeg
 
Ibada za pasaka zinaendelea; kwaya mbalimbali zinatumbuiza. Nimeenda kwenye kanisa mojawapo kusali naomba nisilitaje jina.

Waimbaji wananengua na kucheza mithili ya ngoma za kienyeji na kidunia.

Wengine wananengua miuno kabisa.

Sasa huku ni kumsifu Mungu kweli?
Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Ni kweli kabisa,watu wakate mauno kuonyesha utukufu wa mungu. Halafu kuna jingine la wake wengi, kwenye biblia kuna aliyeoa wake wengi hili nalo ni la kuangalia wanaume waoe hata wake 9.
 
Ibada za pasaka zinaendelea; kwaya mbalimbali zinatumbuiza. Nimeenda kwenye kanisa mojawapo kusali naomba nisilitaje jina.

Waimbaji wananengua na kucheza mithili ya ngoma za kienyeji na kidunia.

Wengine wananengua miuno kabisa.

Sasa huku ni kumsifu Mungu kweli?
Ng'ang'ana mpaka kieleweke....

Ng'ang'ana ng'ang'ana ng'ang'ana mpaka kieleweke......

Hawa wanaojiita walokole sijui wanatupeleka wapi
 
Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa
Unakata kiuno huku unanena kwa lugha. Inapendeza.
 
Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa

Ila wafia dini kwa kuhamisha magoli hamjambo.
Mimi nakumbuka miaka ya zamani kidogo ilikuwa hairuhusiwi mwanamke kuvaa suruali au siketi fupi na kwenda nayo kanisani!
Cha ajabu miaka ya hivi karibuni wanawake wanavaa vichupi skin jeans na kwenda nazo kanisani na mmeanza kusema eti "Mungu haangalii mavazi, ila anaangalia roho"
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Hili ni fundisho la upotoshi limeingizwa makanisani na freemason lengo ni kuwapotosha watu.
Biblia imeweka wazi juu ya mitindo yote kuanzia mavazi,kusifu na kuabudu.
Msienende kama mataifa,kama mtu anacheza dansi zisizo na staha za kukata viuno Ili kuchochea ashiki sio mafundisho ya Biblia hayo.
 
Back
Top Bottom