Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,204
- 7,189
Mwishoni mwa miaka ya 1980, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa noti ya Shilingi Mia Mbili. Noti hii maarufu upande wake mmoja ulikuwa na picha ya wavuvi wawili wakiwa wamebeba samaki mkubwa wakiwa wanaelekea nchi kavu.
Najua wengi wetu hatufahamu kwanini iliwekwa picha ya wavuvi wale? Basi jua haikuwekwa kwa bahati mbaya.
Kwanza kabisa, Picha ile iliwekwa ili kutangaza moja kati ya shughuli ya kiuchumi ifanyikayo hapa nchini. Kwakuwa tuna bahari, Maziwa na Mito basi shughuli ya Uvuvi lazma itafanyika.
Jambo la pili, picha ile ya wavuvi ni picha itokanayo na watu halisi kabisa. Wavuvi hao ni Abdallah Mohamed pamoja na Ibrahim Amanzi wavuvi waliojipatia umaarufu miaka ya 1970 mpaka miaka ya 1980.
Walikuwa ni wavuvi maarufu wenye kuipenda kazi yao hadi kufikia kuwa marafiki wa Rais wa wakati huo JK Nyerere.
Wengine walishuku hao walikuwa ni "wale jamaa zetu" lakini naambiwa hawakuwa.
Kwa mchango wao kwa Taifa, jumlisha ukaribu wao na Mwl Nyerere, wakawekwa kwenye noti ya shilingi 200.
My take: Kama ni uchawa basi hawa ndio walikuwa machawa kwelikweli sio hawa wa siku hizi wanaoishia kulipwa buku 7.