Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni tena, ni baada ya kunyimwa nafasi ya Muongozo

Kubenea anajitahidi sana kwenda sambamba na mwamba Zitto ila inabuma! Leo nae anataka kuonekana na kugonga vichwa vya habari ila kama Zitto. Huyu bwana kaingia bungeni hila na matamanio yake ni kuwa kama na kupambana na Mwamba Zitto. Hawezi,hana kipaji,kina Mnyika wenyewe wanajua Zitto ni nani. Gifted Zitto.
Nimesoma sana na kutafakari sana kuhusu hii thread na sijui Zitto anapenyeza vipi kwenye hii thread. Kubenea ni mtu wa aina yake na vivyo hivyo Zitto Kabwe; changamoto zao nje ya bunge na kwenye vyombo vya habari na jinsi unavyomchukia mmoja na kuonyesha mahaba kwa mwingine inafanya ushindwe kupembua hoja bila upendeleo. Jaribu kushughulika na hoja badala ya watu binafsi wenye huja usizozifahamu. Be a great thinker that you claim to be!
 
Ifike mahali wabunge wafanye kazi tuliyowatuma bungeni.
Sanaa na mbwembwe zisipewe nafasi.
Hakuna Mbunge wa upinzani anayepeleka sanaa Bungeni, Sanaa ipo kwa wabunge wa CCM na ndio maana wanashabikia kutoonyeshwa Live vikao vya Bunge kwa kuwa wengi wao huwa hawakai Bungeni, hawachangii hoja Bungeni, wakiwa Bungeni wanasinzia tu, na wakitoa hoja zao huwa ni hoja mfu na sio kwa ajili ya Taifa isipokuwa kulinda maslahi ya CCM hivyo wapinzani wanataka wananchi wayaone hayo mambo ya hovyo yanayofanywa na hao wabunge wa CCM.
 
Cha kusikitisha zaidi Spika wa Bunge ndio yule aliyepiga wapinzani wake ndani ya CCM wakati wa kampeni, Huyu Tulia kwa umri wake na muonekano kamwe hakuna anayeweza kumuheshimu bila kusahau mambo aliyoyafanya akiwa TPA na huyu Chenge ambaye amepewa uenyekiti pia hakuna Mbunge wa upinzani anayeweza kumuheshimu kwani ni mchafu kimaadili na hana sifa za kuwa kiongozi wa Bunge kwa kashfa za wizi wa fedha za umma bila kusahau kutumia cheo chake vibaya na ubabe kwa kuwagonga wale akina dada makusudi na gari yake na kusababisha vifo vyao hapo DSM.
Kwa hiyo kiuhalisia ndani ya utawala huu wa Magufuli Bunge hili ndio litakuwa Bunge bovu kuwahi kutokea ndani ya nchi hii tangu tupate uhuru.

Unachosema ni kweli.Ngoja tuone maana mwisho wa siku atajutia uamuzi wake wakutosikiliza upande wa pili.
 
Siyo kweli kwamba ni Tanzania pekee ambapo bunge halioneshwi LIVE. Bunge la Uingereza ambao ndio tunatumia mfumo wao wa kuendesha bunge letu hawaoneshi LIVE kila kitu. Kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu (mara moja kwa week), speech ya budget au kukiwa na statement ya serikali kuhusu jambo muhimi ndio wanaonesha LIVE, vinginevyo watu wanaendelea na maisha.

Sasa ww Uingereza na Tanzania ni sawa!! Kwanza kule kuna uwajibikaji Sio sawa na sisi
Viongozi wana wajali wananchi wao
Sisi bado wachanga sana pia bunge letu lina mafigisu figisu sana sasa lisipo kuwa live
Itasaidia wapumbavu kuendeleza upumbavu wao bungeni
 
Kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake! Nape atawanyoosha tu! Nyie endeleeni kususa ovyo mjue heshima yenu inashuka.
 
Nimesoma sana na kutafakari sana kuhusu hii thread na sijui Zitto anapenyeza vipi kwenye hii thread. Kubenea ni mtu wa aina yake na vivyo hivyo Zitto Kabwe; changamoto zao nje ya bunge na kwenye vyombo vya habari na jinsi unavyomchukia mmoja na kuonyesha mahaba kwa mwingine inafanya ushindwe kupembua hoja bila upendeleo. Jaribu kushughulika na hoja badala ya watu binafsi wenye huja usizozifahamu. Be a great thinker that you claim to be!
Huwezi leo ukakaa meza moja na mtu ambaye umeiaminisha dunia kuwa ni msaliti. Pili hii hoja kumbuka ni ya Zitto,sasa kwanini utake nijadili hoja na kumuacha mtoa hoja. Pia inakuuma nini wewe mimi kumjadili Zitto kama (single entity). Msifiche ukweli hamumpendi Zitto. Na hata hicho kikao basi tuu sababu dogo anajua,roho zinawauma. Wamepiga kampeni Zitto asirudi bungeni,mtu mzima karudi anawafunza siasa.
"Ukishindwa kumpiga,jiunge nae"
 
Kumbe lengo lao kuuza sura kupitia TV na siyo kuwawakillisha wapiga kura wao. Haooooooooooo, wamewkwenda zao kula Bata.

Kwani wabunge wa CCM wanafanya nini la maana mle Bungeni zaidi ya kupokea posho .............!!!?
 
Nape ndie kaifikisha Ccm hapo ilipo leo, kasaifia wapinzani kupata wabunge wengi kwa propaganda zake dhaifu ndani ya Ccm, sasa kageukia serikali ya JPM ianze kudharauliwa na kuonekana haiwajali watu wake. Kama JPM na waziri mkuu hawata mshtukia Nape mapema kuna hatari serikali yao ikapoteza sifa zote amabazo waliisha anza kuzijenga na kuaminiwa na watanzania.
Ni lazima ifike mahali tukubaliane kwamba Nape hana uwezo wa kuongoza hata nyumba ya familia moja.
Tukatae tukubali TBC inafanya kazi kwa ruzuku ya serikali hakuna sababu ya kuacha kuonyesha bunge. Ninalaani huo uamuzi.
Anaposema litarushwa usiku kwa lisaa limoja je mjadala wa bunge ni muda gani kwa siku???
Wanapotumia v8 kuzurura siyo gharama bali watanzania kupata habari ni gharama,,, inaingia akilini kweli??? Hii ni aibu.
Nilishangaa Jana alipoulizwa kuhusu nani anagharamia gharama za kurushwa live kwa mkutano wake na waandishi wa habari?
Jibu lake alisema kwani Mengi anapotumia Vyombo vyake vya habari nani anabeba gharama?
 
Kubenea anajitahidi sana kwenda sambamba na mwamba Zitto ila inabuma! Leo nae anataka kuonekana na kugonga vichwa vya habari ila kama Zitto. Huyu bwana kaingia bungeni hila na matamanio yake ni kuwa kama na kupambana na Mwamba Zitto. Hawezi,hana kipaji,kina Mnyika wenyewe wanajua Zitto ni nani. Gifted Zitto.
Upeo wako ndiyo ulipo fikia
Cheo cha kupewa lazima alipe fadhila.
 
..unavyompamba mwanaume mwenzio mpaka unasikitisha,halafu ukute una mke nyumbani!!
Tehe tehe,kwani Mbowe,Sumaye walivyokuwa wanampamba Lowassa nchi nzima hawakuwa na wake nyumbani? Pia nahitaji mke wa pili,upo tayari nikupose.
 
Back
Top Bottom