Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

PM

Majibu yako yatapandisha watu pressure humu na kudondoka. Majibu yako yanaibua kero mpya ya muungano. Fanya mpango na media wadau twende kwenye mdahalo mubashara, huenda tukasikika zaidi ya humu jamvini.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hakuna chochote kipya kisichojulikana, wala hakuna kero yoyote mpya, tena vijana wa juzi ndio hamjui, sisi wenzenu kuingia Zanzibar tulikuwa tunaingia kwa passport as foreigners, na ukirejea pale Airport unapitia international arrivals!, mizigo yako inapekuliwa enzi hizo manual, unalipishwa ushuru kama waliotoka nje ya nchi!.
Ardhi haina kero yoyote, ila Watanzania bara wote ambao ni serious wanataka maeneo Zanzibar, waambie wanione tuu niwape connection, mahari kule ni hata thumni tuu, unafungishwa ndoa ya mkeka, unaomba kitambulisho cha ukaazi, ukiisha pata, unampiga talaka 3, na kuendelea na maisha yako, unanunua land utakavyo!, tena beach plots!.

Nadhani ikifanywa sensa ya makabila ya Bara waliohamia Zanzibar, nadhani Wasukuma tunaongoza!, yale madodo mabivu kuyapata usukumani ni ng'ombe 100!, kule Zanzibar unayakuta ni madogo mabivu yamedondoka yenyewe!, wewe kazi yako kujiokotea tuu!, kwanini Wasukuma tusikimbilie?.

P
 
Kujipendekeza kwa waislaam unapata faida gan wewe ni kafir kwao takataka kbs mnajipendekeza na kiwathamin ilhali wao hawana habar na nyie
Kumbe na kaudini udini nako kana nafasi yake kwenye suala hili ?!! Kazi kweri kweri !! Mara malumbano ya So called Sukuma gang vs Asali ! Mara Usimba na Uyanga 😂😂. Ndio maana Tunasemaga Nchi ngumu sana hii ,

Mpaka sasa bado hatujui nini hasa tukipiganie kama kipaumbele chetu. !!
 
Kujipendekeza kwa waislaam unapata faida gan wewe ni kafir kwao takataka kbs mnajipendekeza na kiwathamin ilhali wao hawana habar na nyie
Mtu yoyote anayeleta udini kwenye issues ambazo dini haihisiki ni mtu muflis kabisa!. Haki haina dini, ukiwa ni mtetezi wa haki utamtetea yoyote bila kuuliza dini yake!. Hapa naitetea SMZ na haki ya Wazanzibari kumiliki ardhi Tanzania kama Watanzania wengine wote.
Mwisho ni mimi sio kafir, kafir ni asiye na dini, mimi ni Mkristo wa kanisa Kuu, Katoliki Takatifu la Mitume!.
P
 
Suala la udogo wa Zanzibar lingekuwa na mantiki iwapo wazanzibar wangekuwa wanatumia ardhi yao tu. Lakini wanaaccess ya sqkm zaidi ya 900,000 za Tanganyika halafu bado mtu anasema wana ardhi ndogo! Mmechanga vitu halafu aliyechanga kidogo hataki chake mtumie wote!!? Huu ni ubinafsi mkubwa.

Pia Nyerere hakuwa na Mamlaka ya kutoa ardhi ya nchi kama zawadi. Ardhi siyo yake, yeye ni msimamizi tu.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na kwa maslahi ya taifa.

Maslahi ya leo ni hii issue ya SMZ kumiliki eneo la ekari 6000 Bagamoyo. Tangazo la SMZ Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
limeleta taharuki na sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi baadhi ya watu kutoa povu!.

Kuna watu wanatafsiri potofu kuwa sehemu ya Ardhi ya Tanzania Bara ni sehemu ya Zanzibar!.

Ukweli ni huu
Anza na bandiko hili la mwaka 2014 iujue historia ya eneo hilo lilimilikiwa vipi na Zanzibar Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku kisha soma majadiliano ya Bunge ya miaka ya nyuma kuhusu issue hii.

View attachment 2644793

Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo

MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA
aliuliza:-

Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:-

(a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo?
(b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa vile swali linaloulizwa na Mheshimiwa Mbunge linahusu mali zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sio Wizara ya Muungano napenda kumjulisha Mheshimiwa kuwa Wizara yangu haiwajibiki kujua kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado inamiliki au haimiliki shamba hilo.

(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haijui kama shamba hilo ambalo liko chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitumia shilingi ngapi katika kuliboresha, namshauri Mheshimiwa Mbunge akapate majibu ya takwimu hizo Wizara inayohusika katika Serilkai ya Mapinduzi Zanzibar.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba kutoa maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, shamba hilo ambalo ni kweli kama alivyosema Naibu Waziri lilimilikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini kwa miaka mingi sana karibu 30 halitumiki, kwa hivi karibuni Serikali imemega sehemu na kuwapa wawekezaji, watawekeza katika mambo ya biofuel na Sehemu bado inaendelea kuwa mali ya SMZ.

View attachment 2644761

My Take
  1. Wabara ondoeni shaka kuhusu umiliki wa SMZ eneo Bagamoyo, SMZ inalimiliki eneo hilo kihalali kabisa kwa vile walipewa na Mwalimu Nyerere.
  2. Kitendo cha SMZ kumiliki eneo huku Tanzania bara, hakulifanyi eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, ni eneo halali la SMZ ila ardhi ni ya Tanzania bara.
  3. Nchi yoyote inaweza kumiliki eneo nchi nyingine yoyote, umiliki huo haulifanyi hilo eneo kuwa sio sehemu ya nchi husika.
  4. Japo SMZ inalimiliki eneo hilo lililokuwa hekta 6,000, kwanza SMZ, haina hati ya umiliki bali ina kibali cha umiliki No. LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971.
  5. SMZ ililitelekeza eneo hilo kwa miaka 45, hivyo serikali ikalimega kumpa mwekezaji, Halmashauri ya Bagamoyo imelipima viwanja inaviuza.
  6. Kwa vile ni eneo halali la SMZ, na sasa SMZ imeibuka kuonyesha ina interest na eneo lake, then itarudi serikalini kuelezea hiyo interest, serikali itakwenda kulipima limebakia kiasi gani, SMZ itapimiwa upya na kugawa.
  7. Iwapo SMZ bado italihitaji eneo lote la awali la ekari 6,000, then italazimika kuwalipa fidia watu wote waliomegewa kihalali.
  8. Kama pia limevamiwa na wananchi, then sheria yetu ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999 will apply kwa mtu aliyetelekeza eneo lake kwa miaka 45, wale wavamizi wana haki fulani.
  9. Ikionekana madhara ya kuwaondoa wavamizi ni makubwa kuliko kuirejeshea SMZ eneo hilo, then kile kibali cha umiliki wa SMZ kinafutwa, wananchi wanapimiwa, na SMZ wanapewa eneo jingine, tuna mapori kibao ya kumwaga, hata wakitaka heka 10,000 wanapewa.
  10. Hii ya kuwagaiya wavamizi imefanyika sana kwenye maeneo ya jeshi na maeneo ya RTD, wavamizi wamepimiwa na kuhalalishiwa!.
Hivyo Watanzania wenzangu isiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hili, after all eneo lote la Zanzibar ni sehemu ya JMT hakuna sababu ya watu kutoa povu, Wanzanzibari kuniliki Ardhi Bara lakini Wabara hawewezi kumiliki ardhi Zanzibar, kwasababu Wazanzibari ni Watanzania wenzetu wana haki zote za Utanzania, ila Zanzibar ni the minority, visiwa vyao ni very tiny, tukiruhusu kila Mtanzania kumiliki ardhi Zanzibar, itaelemewa na kuvizamisha visiwa vile!.

Wakati wa kuumbika nchi, Zanzibar ilikuwa eneo la bara likamegeka kwa sea erosion, hivyo Visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanzania bara ndio maana dhima ya muungano wetu adhimu ni udugu, sisi ni ndugu moja, Waarabu walipokuja Zanzibar ile 1732 Sultan Seyyid Said alipohamoshia Sultanet take toka Oman kuja Zanzibar, aliwakuta wenyeji halisi ni Wahadimu, kutoka Bara, alivitwaa visiwa hivyo toka ukoo wa Mwinyimkuu, na waliompindua Sultan kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni wajukuu wa Mwinyimkuu wenye Zanzibar yao, ndio maana slogan ya Mapinduzi Daima ipo, na baada ya muungano tumekuwa kitu kimoja, ndio maana slogan ya muungano ni tutaulinda kwa gharama yoyote.

Miongoni mwa gharama hizo ni kumsamehe madeni, kumpa 4.5% ya fedha za mikopo na misaada, ajira na hata kumpa eneo lolote Wazanzibari watakalotaka.

Watanzania bara tujifunze kuwa na shukrani, tushukuru sana Zanzibar, ukanda wa eneo la maili 10 ya Pwani ya ya bahari ya hindi, lilikuwa eneo la Zanzibar, ikatugawia!, miji yote ya Pwani kuanzia Dar, Tanga, Bagamoyo imejengwa na Sultan of Zanzibar!

Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar, hata ile replica ya Ikulu pale Chamwino ni mjengo wa Kiarabu!, mbona watu mnakosa shukrani kwa mambo mazuri kama haya, mnaona nongwa Zanzibar kumiliki eneo huku Bara!

Mapinduzi Daima
Muungano Tutaulinda kwa gharama yoyote!.

Paskali.
Tunachojifunza hapa;Mwl.Nyerere alipenda Muungano hata akatoa sehemu ya bara kumilikiwa na Zanzibar.
 
Pia Nyerere hakuwa na Mamlaka ya kutoa ardhi ya nchi kama zawadi. Ardhi siyo yake, yeye ni msimamizi tu.
Rais wa nchi anayo mamlaka hayo. Pale Royal Palm ilipo, ilikuwa ni sehemu ya Gymkana Club, uwanja wa Basketball wa timu ya Pazi, Nyerere akawapa Tanrus co. Ltd. Mwinyi aligawa 21 Beach plots from Police Mess to Masaki, kwa marafiki zake!. Kikwete amewapa maeneo Rwanda, Burundi na DRC kujenga ICD zao.
It's legit.
P
 
Nao waturudishie visiwa vyetu vyote vya Zanzibar na eneo lote lililokuwa la Tanganyika (Kilwa) miaka buku iliopita
 
Attachments

  • FB_IMG_1686182690771.jpg
    FB_IMG_1686182690771.jpg
    91.2 KB · Views: 11
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na kwa maslahi ya taifa.

Maslahi ya leo ni hii issue ya SMZ kumiliki eneo la ekari 6000 Bagamoyo. Tangazo la SMZ Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
limeleta taharuki na sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi baadhi ya watu kutoa povu!.

Kuna watu wanatafsiri potofu kuwa sehemu ya Ardhi ya Tanzania Bara ni sehemu ya Zanzibar!.

Ukweli ni huu
Anza na bandiko hili la mwaka 2014 iujue historia ya eneo hilo lilimilikiwa vipi na Zanzibar Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku kisha soma majadiliano ya Bunge ya miaka ya nyuma kuhusu issue hii.

View attachment 2644793

Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo

MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA
aliuliza:-

Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:-

(a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo?
(b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa vile swali linaloulizwa na Mheshimiwa Mbunge linahusu mali zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sio Wizara ya Muungano napenda kumjulisha Mheshimiwa kuwa Wizara yangu haiwajibiki kujua kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado inamiliki au haimiliki shamba hilo.

(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haijui kama shamba hilo ambalo liko chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitumia shilingi ngapi katika kuliboresha, namshauri Mheshimiwa Mbunge akapate majibu ya takwimu hizo Wizara inayohusika katika Serilkai ya Mapinduzi Zanzibar.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba kutoa maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, shamba hilo ambalo ni kweli kama alivyosema Naibu Waziri lilimilikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini kwa miaka mingi sana karibu 30 halitumiki, kwa hivi karibuni Serikali imemega sehemu na kuwapa wawekezaji, watawekeza katika mambo ya biofuel na Sehemu bado inaendelea kuwa mali ya SMZ.

View attachment 2644761

My Take
  1. Wabara ondoeni shaka kuhusu umiliki wa SMZ eneo Bagamoyo, SMZ inalimiliki eneo hilo kihalali kabisa kwa vile walipewa na Mwalimu Nyerere.
  2. Kitendo cha SMZ kumiliki eneo huku Tanzania bara, hakulifanyi eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, ni eneo halali la SMZ ila ardhi ni ya Tanzania bara.
  3. Nchi yoyote inaweza kumiliki eneo nchi nyingine yoyote, umiliki huo haulifanyi hilo eneo kuwa sio sehemu ya nchi husika.
  4. Japo SMZ inalimiliki eneo hilo lililokuwa hekta 6,000, kwanza SMZ, haina hati ya umiliki bali ina kibali cha umiliki No. LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971.
  5. SMZ ililitelekeza eneo hilo kwa miaka 45, hivyo serikali ikalimega kumpa mwekezaji, Halmashauri ya Bagamoyo imelipima viwanja inaviuza.
  6. Kwa vile ni eneo halali la SMZ, na sasa SMZ imeibuka kuonyesha ina interest na eneo lake, then itarudi serikalini kuelezea hiyo interest, serikali itakwenda kulipima limebakia kiasi gani, SMZ itapimiwa upya na kugawa.
  7. Iwapo SMZ bado italihitaji eneo lote la awali la ekari 6,000, then italazimika kuwalipa fidia watu wote waliomegewa kihalali.
  8. Kama pia limevamiwa na wananchi, then sheria yetu ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999 will apply kwa mtu aliyetelekeza eneo lake kwa miaka 45, wale wavamizi wana haki fulani.
  9. Ikionekana madhara ya kuwaondoa wavamizi ni makubwa kuliko kuirejeshea SMZ eneo hilo, then kile kibali cha umiliki wa SMZ kinafutwa, wananchi wanapimiwa, na SMZ wanapewa eneo jingine, tuna mapori kibao ya kumwaga, hata wakitaka heka 10,000 wanapewa.
  10. Hii ya kuwagaiya wavamizi imefanyika sana kwenye maeneo ya jeshi na maeneo ya RTD, wavamizi wamepimiwa na kuhalalishiwa!.
Hivyo Watanzania wenzangu isiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hili, after all eneo lote la Zanzibar ni sehemu ya JMT hakuna sababu ya watu kutoa povu, Wanzanzibari kuniliki Ardhi Bara lakini Wabara hawewezi kumiliki ardhi Zanzibar, kwasababu Wazanzibari ni Watanzania wenzetu wana haki zote za Utanzania, ila Zanzibar ni the minority, visiwa vyao ni very tiny, tukiruhusu kila Mtanzania kumiliki ardhi Zanzibar, itaelemewa na kuvizamisha visiwa vile!.

Wakati wa kuumbika nchi, Zanzibar ilikuwa eneo la bara likamegeka kwa sea erosion, hivyo Visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanzania bara ndio maana dhima ya muungano wetu adhimu ni udugu, sisi ni ndugu moja, Waarabu walipokuja Zanzibar ile 1732 Sultan Seyyid Said alipohamoshia Sultanet take toka Oman kuja Zanzibar, aliwakuta wenyeji halisi ni Wahadimu, kutoka Bara, alivitwaa visiwa hivyo toka ukoo wa Mwinyimkuu, na waliompindua Sultan kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni wajukuu wa Mwinyimkuu wenye Zanzibar yao, ndio maana slogan ya Mapinduzi Daima ipo, na baada ya muungano tumekuwa kitu kimoja, ndio maana slogan ya muungano ni tutaulinda kwa gharama yoyote.

Miongoni mwa gharama hizo ni kumsamehe madeni, kumpa 4.5% ya fedha za mikopo na misaada, ajira na hata kumpa eneo lolote Wazanzibari watakalotaka.

Watanzania bara tujifunze kuwa na shukrani, tushukuru sana Zanzibar, ukanda wa eneo la maili 10 ya Pwani ya ya bahari ya hindi, lilikuwa eneo la Zanzibar, ikatugawia!, miji yote ya Pwani kuanzia Dar, Tanga, Bagamoyo imejengwa na Sultan of Zanzibar!

Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar, hata ile replica ya Ikulu pale Chamwino ni mjengo wa Kiarabu!, mbona watu mnakosa shukrani kwa mambo mazuri kama haya, mnaona nongwa Zanzibar kumiliki eneo huku Bara!

Mapinduzi Daima
Muungano Tutaulinda kwa gharama yoyote!.

Paskali.
Hiyo miji na hiyo ikulu hakujenga kuturuzuku sisi, alijenga kwa interest zake huyo sultan. Hivyo masilahi mapana ya Tanganyika yaheshimiwe!!!!
 
Back
Top Bottom