Waandishi wa Habari mtakuwa mmemsaliti Nape mkiwepo kesho wakiapishana

Ni muda muafaka kwa TBC kupata hadhi yake ya kuwa kituo cha taifa.

Viongozi wote wa serikali wawe wanatumia TBC pekee iwe marufuku kwenda kwenye vyombo binafsi na iwe marufuku kwa vyombo binafsi kuhudhuria press na shughuli za serikali.

Hivyo vyombo vilazimike kuilipa TBC ndiyo wapate hizo taarifa za serikali otherwise waandike habari za akina Hamorapa Tu.

Ni suala la kuandaa sheria tu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu Nape ni Mbunge wa Mtama sio Mchinga. Swali; hivi waandishi wakigoma na wamiliki wakiwatuma wakaandike itakuwaje. Kimsingi tasnia hii inahitaji marekebisho makubwa ya kutambua nafasi yao. Kwa ufupi wana kazi ya kufanya kuepuka changamoto tuzionazo leo hii.
Asante kwan kunirekebisha mkuu .asante pia kwa maoni yako
 
Hata wasipoenda, wewe umeshasaidia kujua kuwa kesho watu wanaapishwa. hongera kwa kazi mkuu. Mwisho wa mwezi nenda ikulu uchukue posho yako.
 
Kila mwandishi nadhani amesikia leo kuwa Nape ameenguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya tasnia yenu ambako kumempelekea mbunge wa Mtama ndugu muheshiwa Nape kupoteza uwaziri wake mbichi kabisa.

Mmeshuhudia namna Clouds ilivyovamiwa na kiongozi wa mkoa wa Dar ndugu ******* ambaye leo ndio angekuwa hatakiwi kuwepo ofisini, lakini kwa kwa hali ya kushangaza mtu alodili akiwa kiongozi wa serikali kukemea na kuunda tume kitu ambacho toka enzi za maswahibu ya kina Kibanda, Mwangosi hatujawahi ona waziri mwenye dhamana ya habari akidili kufanya ambacho hiki Nape amejaribu kukifanya kwa ajili ya Uhuru wa wanahabari,

Leo mtakuwa watu wa ajabu kumwacha Nape mwenyewe na nyie kwenda kuripoti tukio zima la upishwaji wa mtu ambaye anarithi nafasi ya mtetezi wenu.
Cha msingi kesho Machi 24 muda huo kila chombo cha habari kiwe bize na utafutaji wa habari zingine kwani uapishwaji huo unatokana na KUPUUZWA KWA MALALAMIKO YENU.

Wadau wa habari tunaichukulia kesho kama mtaweza kuitumia siku hiyo kwa kutoletea tukio hilo labda litaweza saidia kilio chenu kusikika huenda pia MKAMFARIJI Nape kwa uhamuzi wenu huu.
Aisee umenena. Hilo halikuwemo kichwani mwangu. Waache TBC tu ndo waende
 
Nape aliwekwa na Mh Rais,ameondolewa na Mh Rais kwa mapenzi yake. Waandishi wana hoja gani kususia shughuli za serikali? Nape hakuwekwa kuwa waziri na waandishi.
 
Na bado chombo chochote kitakachosusia habari za Mkuu wa mkoa wasishangae kukosa biashara za taasisi za umma kama matangazo nk.
Tit for tat
 
Mbona vyombo mbali mbali huko nyuma hadi leo wamiliki na wahariri wamesweka ndani na vyombo vyao kufungiwa bila Clouds hata Waziri mwenye dhamana kuingilia kati?
Mnasahau CEO wetu wa Jamii Forum Maxie siku za nyuma alivyosweka ndani na kufunguliwa mashtaka,je Nape au Clouds walilaani kitendo hicho?
OPEN YOUR EYES ghafla mmekuwa na mapenzi ya kupindukia TANZAPHILIA?
 
Back
Top Bottom