Vodacom yashindwa kufikia nusu ya lengo la mauzo ya hisa, kuomba iwauzie wasio watanzania

Walichokifanya Arusha kwa Lema kinaendelea kuwatafuna
Ndo ujingaa huu grade one naita... Ngoja waruhusu wakenya waje wanunue hizo hisa halafu uanze kuwa wa kwanza kulalamika kwanini wanamiliki uchumi wa taifa hili
 
Tatizo watu hawaelewi, hata tangazo lao la hisa wanakuambia kuwa kabla hujanunua hisa taguta ushauri kwa mtaalamu wako wa uchumi.
Wataalam wa mambo ya stock exchange nadhani ni wachache,na wengi wako Dar,

Angepatikana consultant angalau akafanya road shows,japo kununua hisa,kama ulivyosema inahitaji umakini,vinginevyo atakuwa unacheza kamari, mtaalam ataanza kusoma vitabu vya mahesabu,atajua trend ya kampuni kifaida,madeni,mtaji na mengine kisha atakushauri baada ya kukupa maono yake

Kuna kampuni ya kuuza gesi ya oxygen,TOL,iliwaingiza watu hasara mpaka leo, au NICOL ya wajanja wajanja
 
Ndo ujingaa huu grade one naita... Ngoja waruhusu wakenya waje wanunue hizo hisa halafu uanze kuwa wa kwanza kulalamika kwanini wanamiliki uchumi wa taifa hili
Mimi najilimia mahindi na viazi ulaya
 
Unanunua hisa halafu unaambiwa kampuni imebadilisha jina, wana hisa hatuwatambui
 
Kama za voda ambayo ndio kampuni kubwa zaidi nchini ya mawasikiano zimedoda,vipi na hyo mitandao mingine wakiingiza hisa zao sokoni zitauzika kweli?
 
Tupe analysis sio I think I think kibao.
Acha ujinga wewe soma prospectus ya Vodacom imeshakupa analysis itself kama ni mtu una uzoefu uwekezaji kwenye hisa utajua. Hii hapa ni snapshot:
Mobile operator
Customer
market share
Vodacom Tanzania 31%
Tigo 29%
Airtel 26%
Halotel 7%
Zantel 4%
Smart Telecom 2%
TTCL 1%
Source: TCRA Quarterly Communications Statistics Report, June 2016

Kwa hiyo usifikiri Vodacom itaendelea ku-dominate mobile phones products market wakati hata Halotel tayari ina 7% ya market share.

Hii hapa ni baadhi ya statement ya Vodacom yenyewe:

Vodacom Tanzania expects a more competitive industry landscape
to place pressure on its share of net additions. As a result,
Vodacom Tanzania’s market share is expected to be stable with a
possibility of a marginal decrease over the medium term. Retail
tariffs are likely to experience downward pressure over the short to
medium term, offset by increased usage which should increase
ARPU for the overall industry.

Lakini share zake bado ni nzuri lakini ziko overvalued. Ingawaje mimi binafsi nimezinunua.
 
Makampuni mengine ya simu nadhani hayawezi kununua Hisa za Vodacom maana hata wao wanatakiwa wauze 25% ya Hisa zao.
 
Kwan muda unaishaje wewe mleta mada vipi hisa sio nyanya zikaharibika
Unajua maana ya Initial Public Offering mkuu?,kuna muda maalumu ambao hutolewa pale kampuni inapoamua kuwa public na kuuza hisa zake katika soko la hisa kwa mara ya kwanza
187a94d7fa277fe4e322b9421e80edaa.jpg
 
Nauona mpango wa makusudi wa kukwamisha umilikishwaji wa sehemu ya makampuni ya mawasiliano kwa wananchi.kuna chezo linaendelea kuchezwa na hii consortium
 
Yawezekana bei yao ni kubwa sana. Huenda hilo limefanyika makusudi ili Wazawa wengi washindwe na hivyo kutoa mwanya wa kuomba watu wa nje waruhusiwe kununua hisa za voda. Kufanya hivyo kutakiuka dhamira ya sheria inayotaka Wazawa kumilikishwa asilimia 25 ya makampuni hayo. Serikali ishauriwe isikubali hadaa hii.
Sidhani kama hiyo ni sababu kubwa, maana mtu anayejua thamani ya uwekezaji, 85,000/= ambacho ni kiwango cha chini cha kununua hisa 100 ni kukubwa sana hadi iwe kikwazo!

Elimu zaidi inatakiwa maana haya yanaonekana ni mambo mapya kwa watu wengi japo ni ya siku nyingi.
 
Acha ujinga wewe soma prospectus ya Vodacom imeshakupa analysis itself kama ni mtu una uzoefu uwekezaji kwenye hisa utajua. Hii hapa ni snapshot:
Mobile operator
Customer
market share
Vodacom Tanzania 31%
Tigo 29%
Airtel 26%
Halotel 7%
Zantel 4%
Smart Telecom 2%
TTCL 1%
Source: TCRA Quarterly Communications Statistics Report, June 2016

Kwa hiyo usifikiri Vodacom itaendelea ku-dominate mobile phones products market wakati hata Halotel tayari ina 7% ya market share.

Hii hapa ni baadhi ya statement ya Vodacom yenyewe:

Vodacom Tanzania expects a more competitive industry landscape
to place pressure on its share of net additions. As a result,
Vodacom Tanzania’s market share is expected to be stable with a
possibility of a marginal decrease over the medium term. Retail
tariffs are likely to experience downward pressure over the short to
medium term, offset by increased usage which should increase
ARPU for the overall industry.

Lakini share zake bado ni nzuri lakini ziko overvalued. Ingawaje mimi binafsi nimezinunua.
Unanimbia niache ujinge. Ulichofanya ni kutaka kuonyesha una akili. Soma argument yako ya kuhusu overprice ndo utajua mimi na wewe nani ni mjinga...Umesema 850 ni kubwa ndo nikatak an analysis ya real price. Umeishia tu kuleta data. Unless ufahamu maana ya analysis. I was expecting you to interrogate that data to justify your argument ya 850 ni overprice na uje na approximation ya price.. Tatizo unataka kujifanya una akili sana kumbe poyoyo..
 
Kingine ambacho voda wamekikosea (kwa mtazamo wangu) ni kuweka ulazima wa kuwa na salio kwenye simu pale unapotaka kutumia simu kununua hisa au kujua mawili matatu kuhusu hizi hisa!

Mimi kuna mtu aliniomba nimweleze mawili matatu kuhusu hizi hisa, nilimweleza lakini nkamwambia tunaweza kutumia njia ya simu kununua hisa, sasa ile tunapiga menu yao *150*36# tukaletewa ujumbe eti "Huna salio la kutosha kutumia huduma hii" :mad: :mad: :mad:

Nilimshauri huyu bwana aende NBC lakini kutokana na umbali akaghairi kabisa! Sasa hili pia ni kosa ambalo voda wanalifanya halafu hiyo bank ya NBC yenyewe kuna baadhi ya maeneo haipo!

Warekebishe ili iwe free subscription kwenye simu!
 
Prospectus ya Vodacom inaonesha miaka miwili gawio Kwa kila hisa ni chini ya Sh. 50.00. Bei ya Sh. 850.00 kwa hisa inayopata Sh. 30 hadi 40 Kwa mwaka ni kubwa mno. Rate of return ni ndogo mno. Telecom ni biashara yenye ushindani mkubwa sana na makampuni yalikuwa yanatengeneza faida kubwa kwa kufanya ukwepaji wa kodi. Baada ya kodi kuanza kutozwa inavyostahili faida imeshuka sana na hakuna mwelekeo kuwa faida itaongezeka .

Kushindwa kuuza hisa ni ishara kuwa soko halina confidence kwanza na thamani ya hisa zenyewe, Pili mustakabali wa muda mrefu wa kampuni, tatu hali ya uchumi Kwa ujumla bado haijakaa sawasawa.

Tanzania kuna kampuni kubwa tano Za simu, hali inayofanya ushindani uwe mkubwa sana na uwezekano wa Vodacom kuendelea kuwa kiongozi wa soko ni mdogo. Kuna suala la confidence Katika management ya Vodacom ukiangalia jinsi Rene Meza alivyoondoka na kashfa za Shivacom. Yote hayo ni mambo Muhimu ambayo wanunuaji wa hisa huyafikiria na inatakiwa wayafikirie kabla ya kununua hisa.

Kununua hisa ni tofauti kabisa na kununua viwanja na siwashauri watanzania waende kichwa kichwa. Kabla ya kununua hisa lazima ujiridhishe sana. Na wala haitakiwi watu wafanyiwe kampeni kama Za kisiasa. Inatakiwa performance ya soko la hisa DSE ndo iwe kichocheo na si vinginevyo. Haya mambo ya kupigiana kampeni hayafai kwenye uchumi, watu wanaweza kuja kupigana inapotokea hisa zikafanya vibaya.
 
Gazeti la THE CITIZEN limeripoti kwamba kampuni kubwa ya simu,Vodacom Tanzania,ina mpango wa kuomba soko la hisa liiongezee muda wa kuuza hisa baada ya kushindwa kufikia lengo.

Tarehe ya mwisho kuuza hisa ni tarehe 19/4/2017

Baadhi ya mawakala kama Orbit Securities walipanga kuuza hisa zenye thamani ya bilioni 200,lakini mpaka sasa wameuza hisa zenye thamani ya bilioni 100.

Vyanzo vinasema Vodacom wanapanga kuomba serikali iruhusu taasisi na watu kutoka nje ya nchi pia wanunue hisa katika kampuni hiyo

(Natambua pia kuna jamaa mmoja japo simkumbuki jina,ameishitaki Vodacom na kuzuia isiuze hisa akidai kwamba na yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Vodacom, Vodacom wanamkataa kwamba sio mmiliki,matokeo ya kesi hayajajulikana mpaka itakapoamuliwa na mahakama,sasa sijui mahakama ikiwapiga chini Vodacom,itakuwa na madhara gani kwa walionunua hisa)

Wana uchumi,tunaomba mtupe tafsiri ya mambo hayo,yanaashiria nini? Ila binafsi nilikuwa nataka serikali ifanye moja au mawili

MOJA: Vyama vya ushirika nchini vinayumba sana kimapato hasa pale msimu wa mazao unapokuwa haueleweki,serikali iwaite viongozi wa vyama hivi kama Nyanza,Kilimanjaro Cooperative Union,Kagera Cooperative Union na vingine,iwalazimishe wawekeze Vodacom walau bilioni mbili kwa kila ushirika,au zaidi,hii itafanya diversification ya uwekezaji na kuvifanya vipate mapato ya uhakika kwa miaka mingi ijayo na kuvifanya vihimili mitikisiko ya kiuchumi.

MBILI: Mashirika ya hifadhi ya jamii yawekeze Vodacom,Tigo,Airtel pesa zao baada ya kujiridhisha kwamba zitazaa na watapata faida kubwa kuliko kuziacha fedha hizo zikae tu Benki Kuu ambako zitawatoa mate wakubwa na kuzitumia katika miradi isiyoeleweka

TATU:Ufanyike ubunifu zaidi wa kuwashirikisha wananchi na wafanyakazi wawekeze katika makampuni haya,wafanyakazi wana mishahara, serikali kupitia wizara ya fedha inaweza kuweka dhamana ya,kwa mfano,kuwakata wafanyakazi wanaotaka,katika mshahara,Tsh laki mbili,mpaka milioni kwa kipindi cha mwaka au miezi sita,na mapato hayo yakaenda moja kwa moja Vodacom au kampuni yeyote kama hisa,hii wakifafanuliwa wataelewa na wengi watakubali,hii inaweza kufanywa na serikali na au kwa kushirikiana na makampuni binafsi,watatembelea maeneo wanayofanya kazi na kufafanua na kuwaunga wahusika.

TATU: kila halmashauri ina vikundi vya akina mama na vijana ilivyovisajili,hivyo basi kila halmashauri iwekewe lengo la kuhakikisha vikundi visivyopungua kumi mpaka ishirini wameviita ofisini kwao na kuvishawishi kununua hisa hizo,hii itasaidia serikali iache kuombwa hela na vikundi hivyo au watu hao.

NNE: Makampuni hayo yanayouza hisa yawekewe lengo ya kuwafikia akina mama na vijana kwa asilimia Fulani kama sharti mojawapo,hii itawasaidia kufikia kundi hili ambalo kila Siku limekuwa likipigiwa kelele

TANO: Badala ya kuwauzia watu wa nje hisa hizo baada ya watanzania kushindwa kuzinunua,serikali yenyewe izinunue ili iweze kupata faida,na pia kuchunguza mwenendo wa faida wa kampuni hizo,pia mashirika ya umma wanaweza kununua,itakuwa aibu kwa hisa hizo kuuzwa nje ya nchi kwa sababu sisi tumeshindwa kuzinunua

Binafsi naona kama vile kuna mchezo voda wanataka kucheza au waliingia sokoni kwa kulazimishwa na sheria! Shares zao pamoja na matangazo mengi, hazikuwekewa mazingira ya kuvuta watu wa kawaida wasio na ufahamu wa kutosha wa kuhusu biashara hii kununua shares hizo! Hii ilipelekea kuwapa mwanya baadhi ya watu wenye ufahamu finyu kuhusu biashara hii kuwakatisha watu tamaa ya kununua! Ukifuatilia kwa karibu utagundua kuwa wengi wa walionunua shares ni ama wana ufahamu wa biashara hii ama wana uthubuutu wa ziada wa kucheza na shilingi yao!
 
Prospectus ya Vodacom inaonesha miaka miwili gawio Kwa kila hisa ni chini ya Sh. 50.00. Bei ya Sh. 850.00 kwa hisa inayopata Sh. 30 hadi 40 Kwa mwaka ni kubwa mno. Rate of return ni ndogo mno. Telecom ni biashara yenye ushindani mkubwa sana na makampuni yalikuwa yanatengeneza faida kubwa kwa kufanya ukwepaji wa kodi. Baada ya kodi kuanza kutozwa inavyostahili faida imeshuka sana na hakuna mwelekeo kuwa faida itaongezeka .

Kushindwa kuuza hisa ni ishara kuwa soko halina confidence kwanza na thamani ya hisa zenyewe, Pili mustakabali wa muda mrefu wa kampuni, tatu hali ya uchumi Kwa ujumla bado haijakaa sawasawa.

Tanzania kuna kampuni kubwa tano Za simu, hali inayofanya ushindani uwe mkubwa sana na uwezekano wa Vodacom kuendelea kuwa kiongozi wa soko ni mdogo. Kuna suala la confidence Katika management ya Vodacom ukiangalia jinsi Rene Meza alivyoondoka na kashfa za Shivacom. Yote hayo ni mambo Muhimu ambayo wanunuaji wa hisa huyafikiria na inatakiwa wayafikirie kabla ya kununua hisa.

Kununua hisa ni tofauti kabisa na kununua viwanja na siwashauri watanzania waende kichwa kichwa. Kabla ya kununua hisa lazima ujiridhishe sana. Na wala haitakiwi watu wafanyiwe kampeni kama Za kisiasa. Inatakiwa performance ya soko la hisa DSE ndo iwe kichocheo na si vinginevyo. Haya mambo ya kupigiana kampeni hayafai kwenye uchumi, watu wanaweza kuja kupigana inapotokea hisa zikafanya vibaya.
Umesema vizuri sana hapa. Ili hisa zinunuliwe lazima faida yake ionekane. Nachokiona mimi ni bei kubwa walioweka ambayo kwa biashara iliyopo inaonekana kabisa faida ya vodacom itazidi kupungua. Valuation ya hisa inawezekana ilizifanya ziwe juu kuliko thamani yake halisi.

Unapopeleka bidhaa sokoni ikakosa soka kuna uwezekano bei ikawa kubwa, kama supply na demand iko constant
 
Back
Top Bottom