Vodacom yashindwa kufikia nusu ya lengo la mauzo ya hisa, kuomba iwauzie wasio watanzania

Na huo ndio ukweli, wabongo wengi wanachojua ni UMBEA, KUPIGA DOMO na MAJUNGU ingawa serikali inajitahidi kuwalinda lakini ni mazuzu kama nini KUJIHISI HISI, KUJISHUKU SHUKU, POROJO ZA SIASA . Na laiti kama hizo HISA zingekuwa ACCESSIBLE Kwa watu wote, ZOTE ZINGENUNULIWA NA "WAKENYA" na WAHINDI, Maana hata huko waliko nadhani WANAZITOLEA MATE. Sisi tubaki kupewa tu UBUYU NA MANGE KIMAMBI
hahahahahahhahha
 
Nimesoma na kuelewa, kwanza niseme tu kuwa WATANZANIA wengi hatuna uelewa kuhusiana na HISA, hatujui tutanufaika vipi, wapi tupate msaada kuhusu hisa, je nikitaka kuuza nitauzaje na mambo mengi kemkem, kwa tatizo kama hili ningeshauri VODACOM wasogeze muda mbele lakini kama haitoshi wangetoa vipeperushi mapema vinavyoweza kufikisha ujumbe kwa undani kuhusiana na hisa zao badala ya kusema piga namba 100 afu unapoteza muda kusikiliza matangazo yao, lakini kama hili halitoshi wangepita mapema mikoani kuhamasiha watu ana kwa ana hii ingesaidia watanzania kuelewa angalau ABC kuliko kuweka matangazo Clauds fm, EA radio nk. Kwa kiasi kikubwa tuliopo mtaani tunaulizwa hizo pesa nikinunua hisa, siku nikiwa na tatizo naweza kuzitoa? Unamjibu hapana anasema ni heli kuweka MPAWA tu

Lakini kwa upande mwingine kwa mtoa mada ni kwamba hisa si jambo la lazima kwa mtu asiyehitaji, swala la kuwakata watu mshahara ili tu kiasi fulani kiende huko Vodacom utakuwa wendawazimu, cha msingi ni elimu lkn piah muda wa uuzaji hisa hizo ndio tatizo kubwa na changamoto kwa cc huko IDIMA
Muda wa kuuza hisa haujazingatia kwamba hapa ni Tanzania,elimu bado sana,may be wafanye miezi miwili mpaka mitatu,
 
Kwakweli itolewe elimu ya hisa uone kama watanzania hawatanunua hizo hisa.

Tatizo kubwa ni kwamba elimu ya hisa sijaona ikitolewa kwenye vyombo vya habari zaidi ya uhamasishaji tu wa watu wanunue hisa. Mimi mwenyewe napenda sana kufanya hivyo ila sijui nikiweka let say laki 5 nitakuwa napata faida namna gani....kwa wakati gani na kiasi gani walau kwa mwezi.

Pia, hio laki 5 nitakatwa shilingi ngapi kama kiingilio n.k

Naona upo mpango wa makusudi wa vodacom kutotoa elimu kwa umma ili zoezi libume turudi ktk utaratibu wa awali.

Tunaomba mtupe elimu hasa kwa maswali niliyoyatoa hapo juu...
 
Kwan muda unaishaje wewe mleta mada vipi hisa sio nyanya zikaharibika
 
Gazeti la THE CITIZEN limeripoti kwamba kampuni kubwa ya simu,Vodacom Tanzania,ina mpango wa kuomba soko la hisa liiongezee muda wa kuuza hisa baada ya kushindwa kufikia lengo.

Tarehe ya mwisho kuuza hisa ni tarehe 19/4/2017

Baadhi ya mawakala kama Orbit Securities walipanga kuuza hisa zenye thamani ya bilioni 200,lakini mpaka sasa wameuza hisa zenye thamani ya bilioni 100.

Vyanzo vinasema Vodacom wanapanga kuomba serikali iruhusu taasisi na watu kutoka nje ya nchi pia wanunue hisa katika kampuni hiyo

(Natambua pia kuna jamaa mmoja japo simkumbuki jina,ameishitaki Vodacom na kuzuia isiuze hisa akidai kwamba na yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Vodacom, Vodacom wanamkataa kwamba sio mmiliki,matokeo ya kesi hayajajulikana mpaka itakapoamuliwa na mahakama,sasa sijui mahakama ikiwapiga chini Vodacom,itakuwa na madhara gani kwa walionunua hisa)

Wana uchumi,tunaomba mtupe tafsiri ya mambo hayo,yanaashiria nini? Ila binafsi nilikuwa nataka serikali ifanye moja au mawili

MOJA: Vyama vya ushirika nchini vinayumba sana kimapato hasa pale msimu wa mazao unapokuwa haueleweki,serikali iwaite viongozi wa vyama hivi kama Nyanza,Kilimanjaro Cooperative Union,Kagera Cooperative Union na vingine,iwalazimishe wawekeze Vodacom walau bilioni mbili kwa kila ushirika,au zaidi,hii itafanya diversification ya uwekezaji na kuvifanya vipate mapato ya uhakika kwa miaka mingi ijayo na kuvifanya vihimili mitikisiko ya kiuchumi.

MBILI: Mashirika ya hifadhi ya jamii yawekeze Vodacom,Tigo,Airtel pesa zao baada ya kujiridhisha kwamba zitazaa na watapata faida kubwa kuliko kuziacha fedha hizo zikae tu Benki Kuu ambako zitawatoa mate wakubwa na kuzitumia katika miradi isiyoeleweka

TATU:Ufanyike ubunifu zaidi wa kuwashirikisha wananchi na wafanyakazi wawekeze katika makampuni haya,wafanyakazi wana mishahara, serikali kupitia wizara ya fedha inaweza kuweka dhamana ya,kwa mfano,kuwakata wafanyakazi wanaotaka,katika mshahara,Tsh laki mbili,mpaka milioni kwa kipindi cha mwaka au miezi sita,na mapato hayo yakaenda moja kwa moja Vodacom au kampuni yeyote kama hisa,hii wakifafanuliwa wataelewa na wengi watakubali,hii inaweza kufanywa na serikali na au kwa kushirikiana na makampuni binafsi,watatembelea maeneo wanayofanya kazi na kufafanua na kuwaunga wahusika.


TATU: kila halmashauri ina vikundi vya akina mama na vijana ilivyovisajili,hivyo basi kila halmashauri iwekewe lengo la kuhakikisha vikundi visivyopungua kumi mpaka ishirini wameviita ofisini kwao na kuvishawishi kununua hisa hizo,hii itasaidia serikali iache kuombwa hela na vikundi hivyo au watu hao.

NNE: Makampuni hayo yanayouza hisa yawekewe lengo ya kuwafikia akina mama na vijana kwa asilimia Fulani kama sharti mojawapo,hii itawasaidia kufikia kundi hili ambalo kila Siku limekuwa likipigiwa kelele

TANO: Badala ya kuwauzia watu wa nje hisa hizo baada ya watanzania kushindwa kuzinunua,serikali yenyewe izinunue ili iweze kupata faida,na pia kuchunguza mwenendo wa faida wa kampuni hizo,pia mashirika ya umma wanaweza kununua,itakuwa aibu kwa hisa hizo kuuzwa nje ya nchi kwa sababu sisi tumeshindwa kuzinunua
Nchi yenyewe haileweki hii,unaweza nunua hisa likatoka tamko hapa ukapoteza pesa yote.Bora wanunue wageni maana ukiwaletea ujinga wanakupeleka kwenye mahakama za kina IPTL!
 
Mawazo mazuri tatizo hujui nn kinachomaanisha kwenye uwekezaji wa hisa. Orbit securities na mawakala wengine na vodacom hawawezi kufikia malengo ya uuzaji wa hisa kwa sababu zifuatazo
1. Soko halivutii kuwekeza kwa wakati huu kwan hakuna kampuni hata moja inayofanya vizuri sokoni na kuporomoka kwa mauzo ya hisa kwa ujumla ndo kunakofanya watu washindwe kuweka pesa zao dse.
2. Vodacom plc hawavutii kuwekeza kwan ni zaidi ya mwezi toka wameanza kuuza hakuna mabadiliko katika bei yao jaribu kutazama kampuni kama swala zilizoolozeshwa hivi karibuni zilifanyaje kwa wiki za mwanzo ili kuvutia investors.
3. Uwekezaje kwenye shares ni hatar mno kwa nyakat hizi ni mara kumi kuwekeza kwenye realaestate maana ni sekta ambayo ukuaji wake upo wazi sana na nyakat zilivyobadilika kumekuwa na faida maradufu.
 
Kwakweli itolewe elimi ya hisa uone kama watanzania hawatanunua hizo hisa.

Tatizo kubwa ni kwanba elimu ya hisa sijaona ikitolewa kwenye vyombo vya habari zaidi ya uhamasishaji tu wa watu wanunue hisa. Mimi mwenyewe napenda sana kufanya hivyo ila sijui nikiweka let say laki 5 nitakuwa napata faida namna gani....kwa wakati gani na kiasi gani walau kwa mwezi.

Pia. Hio laki 5 nitakatwa shilingi ngapi kama kiingilio n.k

Naona upo mpango wa makusudi wa vodacom kutotoa elimu kwa umma ili zoezi libume turudi ktk utaratibu wa awali.

Tunaomba mtupe elimu hasa kwa maswali niliyoyatoa hapo juu...
Soko la hisa liko Dar es salaam tu!! Walau wafungue ofisi kikanda na wawe na Siku maalum ya kufungua soko kikanda.

Pia mitandao ya kijamii na teknolojia haitumiki kutoa elimu,ni rahisi kukutana na video clip ya wema sepetu kuliko ya mtu wa soko la hisa akitoa elimu,hawaandai na kusambaza video zao.

Hii inaenda kwenye wizara na idara zote za serikali,kwa mfano maafisa Kilimo na mifugo wamejaa tele wizarani, vyuoni,ungetaraji wawe na mkakakti wa kuandaa video fupi fupi za Kilimo cha mpunga,alizeti,pamba,kahawa n.k au ufugaji wa mbuzi,ngombe,nguruwe kitaalam,hii haigharimu kitu na ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii unakuwa na positive impact.

Nadhani kuna haja ya kubadilika mahali
 
Nchi yenyewe haileweki hii,unaweza nunua hisa likatoka tamko hapa ukapoteza pesa yote.Bora wanunue wageni maana ukiwaletea ujinga wanakupeleka kwenye mahakama za kina IPTL!
Mdau mmoja anasema kama una milioni zako kadhaa kanunue kiwanja au shamba/nyumba,kila Siku unakuwa unaiona na inauzika
 
Hahaha unaweza nunua baada ya mwaka ukaambia kampuni haijapata faida,mbona yale ya madini yanauza hisa Ulaya na hapa hayauzi?
 
Voda ni wahuni hisa wanakwamisha zisinunuliwe ili wajiuzie kupitia hoja ya wageni wekeni mfumo mzuri wa manunuzi simuni tuone kama hisa azikununuliwa
 
Watu hawana uelewa na haya mambo ya hisa!

Mm binafsi natamani kununua hizo hisa lakini sijui nitafaidika kwa kiasi gani, mda gani na kivipi?
 
Hahaha unaweza nunua baada ya mwaka ukaambia kampuni haijapata faida,mbona yale ya madini yanauza hisa Ulaya na hapa hayauzi?
Halafu ukiwa na hisa chache unakuwa huna sauti,wale walioweka mabilioni ndio mara nyingi wana sauti,inaweza kupatikana faida wakaamua kuiwekeza,japo inaongeza wigo wako wa umiliki,lakini sisi masikini majengo yetu huwa yavuki mwezi au mwaka,asubuhi tu tutaanza Julia hatujapata gawio
 
Mtandao wenyewe vifurushi wanaviuza ghali, Spidi yao ya Internet siku za karibuni ni ndogo mno, soon watapoteza wateja kwa kampuni ya TTCL, Kwa hali hii ni dhahiri thamani ya hisa zao itashuka hata gawiwo lao litakuwa dogo mno au hakuna!

Kwa Mazingira ya namna hii siwezi kutupa pesa yangu huko!
 
Mtandao wenyewe vifurushi wanaviuza ghali, Spidi yao ya Internet siku za karibuni ni ndogo mno, soon watapoteza wateja kwa kampuni ya TTCL, Kwa hali hii ni dhahiri thamani ya hisa zao itashuka hata gawiwo lao litakuwa dogo mno au hakuna!

Kwa Mazingira ya namna hii siwezi kutupa pesa yangu huko!
 
Huu utapeli wa sirikali sijui utaisha lini... Unaondoa hela kwenye mzunguko kisha biashara zinadorora wafanyakazi wa makampuni wanapunguzwa kisha unalazimisha kampuni za simu kuuza hisa kisheria. Hizo hisa atanunua mama yenu??
 
Mtandao wenyewe vifurushi wanaviuza ghali, Spidi yao ya Internet siku za karibuni ni ndogo mno, soon watapoteza wateja kwa kampuni ya TTCL, Kwa hali hii ni dhahiri thamani ya hisa zao itashuka hata gawiwo lao litakuwa dogo mno au hakuna!

Kwa Mazingira ya namna hii siwezi kutupa pesa yangu huko!
TTCL wanaweza kuwa vizuri? Maana makampuni mengine yameikuta,yameipiga bao, ni kama vile haina wateja imebetweka kwa kutegemea simu za mezani za ofisi za umma
 
Back
Top Bottom