Viongozi wangu wa CCM inatosha sasa, TEC hawatatuelewa hadi tueleweke!

Bakwata na wale Waislam waliokuwa wanajadili waraka wa TEC wako wapi? Aibu zenu. Wenzenu hao wanababaikiwa na kubembelezwa kama watoto. Mara wanapewa hela /michango..

Nyinyi kazi yenu ni kutumika tu halafu mnaachwa hapo na matatizo yenu. Wakikwama sehemu wanawatumia mtoe matamko uchwara huku shida zenu ziko palepale.
 
Kabla ya 2015 mimi nilikuwa na mtu ambaye alikuwa anaweza kupeleka kwenye mfumo wa nchi maoni yangu juu ya nani ateuliwe na CCM kugombea urais.Nilikuwa natoa hoja mbili kuu kumpendekeza Magufuli; 1. Kati ya viongozi wote yeye bado alikuwa ana imani ya wananchi,2.Alikuwa anatoka kwenye kanda yenye wapiga kura wengi.
Kwa sasa huyo mtu hayuko jirani na mfumo wa sasa.Lakini kwa kuzingatia kuwa mimi nikisema kitu mara nyingi ndiyo huwa ni uhalisia,nashauri CCM wasimteue Mama mwaka 2025 kugombea urais.Ikiwezekana Mwinyi,Rais wa Zanzibar agombee huku Bara.

Angegombea Mwinyi wasingekuwa na haja hata ya kupiga kampeni. Mwinyi ni kifaa hasa. Angepita kwa 80%, kiulainiii kabisa.
 
Lazima niseme. Nguvu kubwa inafanywa na viongozi wetu wa CCM Taifa ambao pia ni viongozi serikalini kupata 'uungwaji mkono' na Maaskofu wa Kanisa Katoliki. Ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Kuanzia Mwenyekiti/Rais hadi viongozi wengine waandamizi wamekuwa 'busy' na kutafuta kukubalika na wakatoliki.

Pamoja na ukweli kuwa ili ushindi upatikane na utulivu wa kiuongozi utamalaki lazima ukubalike na TEC, sasa imekuwa 'too much'. Makada wabobezi na waandamizi (hasa tulio wakatoliki) tunatumwa bila kusemwa kwa Kardinali, Maaskofu, Mapadre na wengineo ili kusaka kukubalika kwa viongozi wetu.

Amini nawaambia viongozi wangu wa kichama na kiserikali, TEC hawatashawishika kirahisi.

Hawatasahaulishwa msimamo na Tamko lao juu ya mkataba tata wa DP World. Hawatalaghaiwa kwa ahadi za kifedha; kupokelewa uwanjani au kupewa kanzu. TEC bado wanalo la bandari na wamejipanga kuusimamia msimamo wao.

Ili CCM tujisafishe mbele ya TEC, Tamko lao liheshimiwe. Kupigana vikumbo kujisogeza kwao hakutasaidia chochote. TEC imesheheni waelewa wa mambo zaidi ya wanasiasa wa zamani na wa sasa. Si wepesi kuyumbishwa kwa ahadi zisizo na kadi; michngo ya michongo na zawadi maridadi.

CCM tumeshaanza kampeni, wenzetu vipi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
We mwongo!
Mbona 2010 Katoliki walimkataa JK wakasimama na Padri Slaa na still mtoto wa mjini aliwaonyesha shoo
 
Viongozi Kwanza waone aibu na wakiri na kutubu dhambi ya uongo juu ya Dubai na kusumbua umma.Mamlaka ya nchi iwatose waongo na wachumia tumbo waliopotosha imma kwa kusema wasichokiamini na kutosema wanachokiamini.Iwatose hats Kama Ni gesture tu Lakini imma ujue kuna juhudi za kujirudi.Nchi imekosa wenye hekima na busara kwa kuwa waliopo wanakandiwa na kuzodolewa na manungayembe ya kisasa,vijana makuwadi wa mitaji na fedha chafu,eti kwamba kwa kushauri na kutahadharisha wanasumbuliwa na njaa.Ni maneno yanayoweza kutamkwa tu na vijana wazaliwa mitaroni,wasiostahili kupewa dhamana kwa shughuli za chama na serikali.Rais asiposituka na kutenda tunakaribisha mafuriko.TEC si ya mademagogue,Ni ya watu walioshiba elimu,wenye kujitoa ili wengine wapate kimwili na kiroho .Tunataka kuona Yuda Iskariote akijinyonga na kuvitema vipande vya dinari vilivyoleta kilio kwa jamii.Bila hivyo mengine yote lelemama na ulaghai uliokithiri!
 
TEC haiwezi kutaka CCM ishindwe uchaguzi hata mara moja !!
Wewe kweli unaijua TEC, tena hata kuliko wakatoliki wenyewe!na hii inathibitisha ukweli kwamba kuwa mkatoliki sio sababu ya kujua politics za kanisa lako! Ukweli ni kwamba TEC haiko tayari kuona CCM inaanguka, yanayowaunganisha ni zaidi ya yanayowatofautisha!
 
Na huo ndio ukweli wenyewe ! 🙏🙏
 
Waambieni Wakatoliki ni kosa kupeleka kwenye mimbari za kanisa mambo ya serikali kama kushauri au kukaripia iwe kwa viongozi wao.
Lakini kwa hii sioni afya kwa kweli hebu fikiri kama ingekua waislamu ndiyo wamehusika na hili misikitini mwao ingekuaje?
Zaidi ni kwanini akiingia Muislamu Wakatoliki wanakua na maneno mengi sana
Udini?
 
Hata Mimi naunga mkono,kwani lazima Kila kitu hao TEC waunge mkono? Ni upuuzi kutokubalia kukubaliana na itakuwa Haina maana Sasa ya kuwa na Taifa.

Maendeleo huletwa katikati ya mgongano wa fikra,TEC na RC hawaendeshi hii Nchi ni mambo ya kipuuzi kuwaza hivyo na inajenga mbegu ya chuki kw watu wa madhehebu na dini zingine.

Inakera sana.
Ni wengi,wasomi,na matajiri nà popote ukienda wapo

Taasisi ya kwanza kama siyo ya pili nyuma ya CCM kwa ushawishi na yenye mizizi toka shinani huko hadi taifa
 
Lazima niseme. Nguvu kubwa inafanywa na viongozi wetu wa CCM Taifa ambao pia ni viongozi serikalini kupata 'uungwaji mkono' na Maaskofu wa Kanisa Katoliki. Ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Kuanzia Mwenyekiti/Rais hadi viongozi wengine waandamizi wamekuwa 'busy' na kutafuta kukubalika na wakatoliki.

Pamoja na ukweli kuwa ili ushindi upatikane na utulivu wa kiuongozi utamalaki lazima ukubalike na TEC, sasa imekuwa 'too much'. Makada wabobezi na waandamizi (hasa tulio wakatoliki) tunatumwa bila kusemwa kwa Kardinali, Maaskofu, Mapadre na wengineo ili kusaka kukubalika kwa viongozi wetu.

Amini nawaambia viongozi wangu wa kichama na kiserikali, TEC hawatashawishika kirahisi.

Hawatasahaulishwa msimamo na Tamko lao juu ya mkataba tata wa DP World. Hawatalaghaiwa kwa ahadi za kifedha; kupokelewa uwanjani au kupewa kanzu. TEC bado wanalo la bandari na wamejipanga kuusimamia msimamo wao.

Ili CCM tujisafishe mbele ya TEC, Tamko lao liheshimiwe. Kupigana vikumbo kujisogeza kwao hakutasaidia chochote. TEC imesheheni waelewa wa mambo zaidi ya wanasiasa wa zamani na wa sasa. Si wepesi kuyumbishwa kwa ahadi zisizo na kadi; michngo ya michongo na zawadi maridadi.

CCM tumeshaanza kampeni, wenzetu vipi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Ccm na Tec mna ushirika gani ?
 
TEC haifanani na akina Waitara, Katambi, Mollel, Kafulila au akina Mkumbo; ambao wakiwa na njaa wanapiga sana kelele, wakirushiwa mfupa, ni kushangilia na musifia kama wehu.

TEC haiwezi kunyamazishwa au kubadilishwa katija wanachokiamini kuwa siyo sawa, kwa kurushiwa mchango au kutembelewa maofisini kwao. Kitakachobadilisha msimamo wa TEC ni Serikali na viongozi kuachana na ule mkataba wa kishenzi wa DP.
Vipi una lolote la kusema tena leo baada ya mkataba kusainiwa kati ya TPA na DP-WORLD mbele ya TEC?
 
Back
Top Bottom