Hivi kwa malalamiko haya yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Tanzania tunadhani ipo siku Mama Samia ataweza kuwaletea Wananchi maendeleo? Watu wanakamatwa na kuwekwa maabusu bila hatia yoyote kwa maelekezo ya watu wanaokesha misikitini na makanisani, hatuoni Kama tunaliletea laana Taifa? Tunadhulumu watu Kisha tunakwenda kusali si kumkejeli Mwenyenzi Mungu? Tumeshuhudia viongozi waandamizi nchini wakitwaliwa kwanini tusijifunze tu kwamba Duniani tunapita na madaraka tutayaacha? Tunataka afe Nani ndipo tukubali kuwa kifo kipo ndani yetu na umuhimu wa kuandaa nafsi zetu ni kitu cha Kwanza?
Mnawashikilia wazee wa miaka 80+ bila hatia yoyote, mnawanyima chakula huku ninyi mkiwa ampitishi dakika bila kula Tena mkiwa mnakula Kodi zetu, Ni ukatili wa namna gani mmeumbiwa ni watu wenye viburi vy madaraka?
Nchi hii imekuwa kama uwanja wa mapigano for more than five years now, mnapambana na chadema badala mpambane kuwakwamua wananchi walio na vipato vya chini. Ni Nani aliyewaambia ipo siku udhalimu utashinda haki? Kama mmekataliwa kwanini msitumie muda kuchunguza chanzo Cha kukataliwa kwenu?
Bungeni mmekaa wenyewe, serikali yakwenu, kila kitu Cha kwenu mnaangaika Nini na watu wanaozungumza kwenye majukwaa?
Mitandaoni tunasomeka Kama watu wakatili kwa sababu tu ya viongozi wachache wasio kuwa na hofu ya Mungu. Leo ni mwekezaji gani atakuja kiwekeza sehemu ambayo Rais ndiye Katiba? Ni Nani atakuja sehemu ambayo polisi wanakamata watu bila hatia ? Ni Nani atakuja kuwekeza sehemu ambayo maovu hayakemewi? Ni Nani tunategemea awekeze kwenye utawala usiotabirika unataka?
Mnatufanya tuzidi kuwa maskini, mmewafanya wawekezaji wakwapue fedha waondoke nazo kwenye mabegi kwa sababu tu ya watu wachache wasiojitambua. Tunapata hasara za mabilioni kwa makampuni kutorosha fedha wakishirikia na Watanzania, hakuna mwananchi aliye na uhakika Kama Kuna kiongozi mzalendo. Mmeliua Tqifa kwa mikono yenu mkipambana na chadema.
Tuhurumieni, wahurumieni wapiga kura hata Kama mnajua kura zao haziwasaidii, wahurumieni wasio na ajira, wahurumieni wajukuu zenu...mnafanya unyama usiovumilika na watu wakigeuka waalifu sijui mtafaidika Nini.
Inaumiza sana kuona kila Kona hakuna positive news juu ya nchi yetu, negative news ndo zimetawala na kuwa kipao mbele Cha watu. Inasikitisha kuona Taifa zima wakiwemo viongozi waandamini wamekuwa wafuasi wa Kigogo na wanaharakati, Taifa Lina watu wanaotenda wasichokiamini na wanatoka adharani kukiri kwamba wanafanya kupata mkate wa siku. Ni Tqifa la aina gani? Juzi tumempoteza JPM nadhani ilikuwa sehemu yakujifunza hao wanaomshauri Mhe. Rais wanaamin wanayomshauri au wanasikiliza Rais anataka Nini?
Kwanini Mhe. Rais usiwafanye wananchi kuwa washauri wako kuliko kuwafanya wananchi maadui? Nchi si ya wanachama wa CCM nchi ni ya wananchi.
Angalau ungejenga nchi ikarudi kwenye hadhi yake na 2024 ukaanza harakati za siasa za vyama. Umeanza kupambana na watu ambao hawana Cha kupoteza na wanazaliwa kila siku na mapambano yao dhidi yako yanapelekea madhara ndani na nje ya nchi. Jaribu kuruhusu nchi iwe ya Watanzania, ondoa nchini mikononi mwa dola maana soon utakuta unaanza kujaza wqtu mahabusu na Magereza Kama mtangulizi wako
Hakuna maendeleo Kama hakuna haki, hakuna amani Kama hakuna haki ...tutaendelea kuuza jina baya nje na mabalozi wetu nje wanaweza kuwa mashuhuda wa ilo.
Natamani uingie miyoyoni mwa Watanzania ujifunze wanataka nini uwatendee, haya manyanyaso yamekuwepo miaka mitano na hatukuvuna chochote tumeambulia kulibomoa Taifa.
Nikutakieni jumapili njema, napata hasira sana kuona wanaofanya haya ni ndugu zetu