Viongozi wa CHADEMA kutokumtambua Rais ni Kosa?

kwanini wasuse wakati ni ujira wao halali . Na hii kodi ni pesa za wananchi si ya serikali, sidhani kama na hiyo methali yako umeiweka mahali pake. Ni lazima wachukue huo ujira wao ili waweze kufanya kazi za bunge na kuwakilisha watu waliowatuma.

watu wenyewe ndio sisi ambao tunakatwa kodi na tumempa kura zetu jk kwa kishindo..........nenda lindi,mtwara,unguja,tanga,tabora,ruvuma,kagera na pwani....ht silaa hajulikani.................waache mahela hayo tuone....
ikumbukwe kura hazijapigwa na jf zimepigwa na watanzania wote nyie vipi bana!
 
Hata sisi makada wa CCM tuliukubali uchaguzi wako kwa roho moja. Knowing you are independent mind, and you will go to bunge and bring Kawe improvements and also creating legislations that will improve maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla. Halima, wewe bado mchanga katika siasa zetu, hata hivyo umeonyesha uwezo mkubwa tu wa kufikiria na kuchanganua mambo.

Umekwenda bungeni tukijua kwamba ili uweze kuleta mabadiliko uliyoyaongea sana kwenye kampeni zako inabidi ufanye kazi bega kwa bega na wabunge wenzako pamoja na watendaji wa serikali. Ulivyoapishwa kuwa mbunge ulikubali kulitumikia taifa kwa misingi ya katiba yake. Na ukamuomba Mola akusaidie. Sisi tulipata faraja sana, kuona mbunge kijana na mwanamama akituwakilisha, ukiachilia mbali itikadi zetu tofauti za kisiasa.

Halima, umekwenda bungeni baada ya wiki moja tu, hatukuelewi vizuri. Umeapa kufanya kazi na serikali hii lakini jana umefuata mkumbo na kutoka kwenye hutuba ya Raisi. Kwa sisi wakazi wa Kawe, kuwalk out sio tatizo. Tatizo ni unafiki wa hicho kitendo, juzi uliapa kuwa mbunge knowing kwamba lazima ufanye kazi na serikali hii. Pia utaanza kutimiza ahadi zako ulizotuahidi. Lakini, pia unasema kwamba humtambui Rais Jakaya. Halima, unatuchanganya huku jimboni. Miaka 5 ni mingi, na kama utakuwepo bungeni kufanya hii michezo ya kuigiza kwa kipindi chote, nadhani utakuwa unapoteza sana potential yako. Kwa sisi tunaokujua, tunaamini kabisa kwamba umeshindwa kwenda kinyume na uongozi wa chama chako. Lakini hilo haswa ndio linalotuogopesha, kushindwa kufuata misingi yako kwa sababu ya shinikizo la uongozi wa Freeman na mwenziwe Willbrod.

Huku Kawe ni wewe pekee utayekuwepo kwenye ballot hapo 2015. Na sisi wana Kawe tutakukumbuka kwa yale uliyojenga na sio kubomoa. Mpaka dakika hii, hujajenga hata moja, na unabomoa misingi ya ushirikiano with your number one partner in development of Kawe, serikali ya CCM.

Ni hayo tu, karibu Tegeta.

Selemani.

Hata mimi ni wa Kawe Darajani, chomoa kura yako 2015, mimi nachomeka ya kwangu. Kwani wakati wa kampeni matokeo yalikuwa tayari? Hivi move ya CCM ya kumtema Sitta kwenye Uspika na kukubaliwa na wabunge wa CCM sio usaliti kwa wananchi wanao wawakilisha?
 
Kwani hujui kuwa jamaa baada ya hatimaye kuamini kuwa amekosa mwana na maji ya moto, anataka wote wakose.

Katika wabunge wa Chadema hakuna hata mmoja aliyembumbu wa kufuata mambo kwa mkumbo, wote wanajua nini wanachokifanya, isitoshe wengi wanawaunga mkono, japo wapo wenye itikadi tofauti na wengine basi wabishi tu wasiopenda kuelewa na kukubali wataendelea kubisha, lakini naamini JK amepata taarifa na pia watu wanaomwezesha wamepata taarifa, na hii ndio njia ya kuonyesha hisia zao.
 
Jamani naomba mjadala uendelee kwa ustarabu. Kama mtu ana dukuduku lake au maoni yake atoe kwa kuzingatia sheria za JF. Kuna post zime kuwa edited kwa matusi au kufutwa kabisa. Matusi yakizidi hatua zita chukuliwa dhidi ya wote wanao chafua jukwaa.
 
Nachanganyikiwa mnaposema kodi ya wananchi mil 40 au watanzania tupo mil 40 na waliopiga kura ni mil 8 tu yaani hiyo hesabu yako ywa walipa kodi ina include na huyu binti yangu wa miezi miwili? au unaamanisha nini hasa tafadhali nifafanulie.
Huyo binti yako unapoenda kumnunulia maziwa ya kopo hujui kuwa unalipa kodi kweli wewe hujui kodi inapotoka unafikiri ni mil 8 waliopiga kura tu je ambao hawakupiga kura hawalipi kodi?.
 
Jamani naomba mjadala uendelee kwa ustarabu. Kama mtu ana dukuduku lake au maoni yake atoe kwa kuzingatia sheria za JF. Kuna post zime kuwa edited kwa matusi au kufutwa kabisa. Matusi yakizidi hatua zita chukuliwa dhidi ya wote wanao chafua jukwaa.

I concur. Tutumie janvi vizuri.
 
Upuuzi mtupu, hii post imekaa ki-CCM sana. Lakini pale shati-la-kijani-CCM litakapowabana watawapigia magoti CHADEMA.
 
"Mh Zitto kabwe, Mh Shibuda, Mh Lucy owenya, Mh ndesamburo pamoja na kafulila hawa wote leo hawakwenda bungeni kwa kuwa hawakutaka (kutoka wakati Rais anahutubia), walipingana na tendo hilo,Je kama Rais aliapa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri na wabunge pia unawezaje kusema humtambui?????hivi ndivyo adabu ya mtoto kwa baba yake???ama kweli MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO,ila sisi wananchi tutawafunda" - Violet Mzindakaya.

Watanzania tuko kama makopo tupu. Yeyote anayetupa takataka zake ndani yetu tunapokea. Tufunguke akili na macho yetu na tuanze kufikiri 'critically'. Kama kuna watu wanalalamikia mfumo fulani ambao wanadai hauwatendei haki njia nzuri ni kusikiliza malalamiko yao na siyo kuwazuia wasilalamike. Walivyofanya Chadema ni haki yao na hata kama baadhi walifuata mkia, ndivyo sisi binadamu tulivyo.

Cha msingi ni je, Chadema wamesikilizwa na tatizo lao limeeleweka na kutatuliwa na mamlaka husika? Na katika yote matokeo ya kitu yanasababishwa na chanzo chake. Chanzo cha wabunge wa Chadema kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ni nini?
 
Hao CHADEMA hovyo sana! Kama kweli hawamtambui basi sharti wasiingie bungeni na wasichukue ile hela ya posho wala pesaingine manake itakuwa kama wanachukua kutoka serikali wasioitambua!! Yule kiongozi wa upinzani bunge lililopita aliwaambia hivyo kwani wao CUF hawaku ingia baraza la wakilishi mpaka muafaka ulivyofikiwandipo wakarudi barazani na kuanza kuchukua fweza.

Namna gani hii!!!!????

unajua maana ya serikali?
wabunge wa kweli hawaendi bungen kuangalia posho wanaangalia maslahi ya wananchi waliowachagua.
 
"Mh Zitto kabwe, Mh Shibuda, Mh Lucy owenya, Mh ndesamburo pamoja na kafulila hawa wote leo hawakwenda bungeni kwa kuwa hawakutaka (kutoka wakati Rais anahutubia), walipingana na tendo hilo,Je kama Rais aliapa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri na wabunge pia unawezaje kusema humtambui?????hivi ndivyo adabu ya mtoto kwa baba yake???ama kweli MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO,ila sisi wananchi tutawafunda" - Violet Mzindakaya.

AA Dada VAI ...wewe umelelewa na nani?
 
Halima, kwa kukusaidia tu kuchanganua mambo. Kawe ulipata kura 43,365. Na Raisi Jakaya Kikwete alipata kura 45,321. Kuna wana Kawe wengi tulikupa kura wewe za ubunge na kumpa Jakaya za uraisi. Ninachokwambia ni kwamba majority of your constituency voted for President Jakaya (ambaye haumtambui) than you. Najua una uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo na unajua ninachoongea ni nini.
 
Hakuna sheria, ndiyo maana wanadai katiba mpya inayoeleweka, yenye kukithi matakwa yote ya wananchi.
 
Hao CHADEMA hovyo sana! Kama kweli hawamtambui basi sharti wasiingie bungeni na wasichukue ile hela ya posho wala pesaingine manake itakuwa kama wanachukua kutoka serikali wasioitambua!! Yule kiongozi wa upinzani bunge lililopita aliwaambia hivyo kwani wao CUF hawaku ingia baraza la wakilishi mpaka muafaka ulivyofikiwandipo wakarudi barazani na kuanza kuchukua fweza.

Namna gani hii!!!!????

Kwani walichokifanya CUF ndicho kipimo cha kutomtambua Rais tu? There're many ways of skinning a cat!
 
Back
Top Bottom