Rebeca 83
JF-Expert Member
- Jun 4, 2016
- 15,235
- 32,441
Habari JF,
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine tatizo la ajira limekua sugu kwa vijana . Takwimu zinaonyesha kundi la vijana linaongezeka; kutakuwa na ongezeko la vijana kufikia million 15 kufikia mwaka 2030 tofauti na sasa ambapo idadi ni million 11. Hili ongezeko la vijana linaweza kuwa na athari nyingi kama halitakuwa limewekezwa vizuri na jamii (invested)., kutojithamini(confidence/low self esteem),na kukosa uwezo wa kujihudumia kwa vitu muhimu na kuingia kwenye uhalifu. Hizi ni baadhi ya athari zinazoweza kuonekana kwa vijana. Huu ni mzigo ambao jamii itaubeba kwa gharama kubwa, kupunguza mzigo kwa jamii na kuboresha Maisha ya vijana (livelihoods) nchi yetu inahitaji mikakati mipya wa kupambana na tatizo la ajira.
Ningependa kupendekeza nchi yetu iwekeze kuwapa ajira vijana kupitia Kilimo. Kilimo ni uti wa mgongo na asilimia 76 ya watanzania tunategemea kilimo na kinachangia sana kwenye pato la taifa hivyo ni eneo lenye potential kuongeza ‘income’ kwa mtu mmoja mmoja na kwa nchi yetu. Nimeona pia mahali tuna Ardhi ya rutuba (Arable land) ambayo ni kubwa sana (44millions hectares) ambayo matumizi yake kwa sasa ni madogo (33% only),tunaweza ku ‘optimize’ matumizi yetu ya ardhi kufikia at least 90% na tutaona maendeleo.
Bandiko hili naomba tushirikiane njia za ku ‘optimize’ matumizi ya ardhi yetu kwenye kuwapatia vijana ajira. Mimi ningependakwanza kushauri kubadilisha ‘attitude’ ama ‘mind set’ za vijana wa sasa kuhusu kilimo,wengi wanaona kilimo ni cha kwa waliofeli, na ‘hakilipi’.. Mimi sio mchumi ila nahisi serikali ikiweka muundo mzuri wa kununua mazao kutoka kwa wakulima,au kutafuta masoko ya wakulima ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kununua mazao hayo labda itasaidia vijana kuingia kwenye kilimo. Namaanisha serikali ifanye ku ‘deal’ na manunuzi ya mazao na vijana wa deal only na kulima, yaani kuwe na security fulani mtu akilima ajue atamuuzia nani na wapi….kukiwa na hiii 'security' ya masoko ndivyo watu/vijana watajiingiza kwenye kilimo bila kuogopa kuwa kilimo hakilipi.
Pia ikiwekwa kama ‘policy’ au utaratibu maalumu kwa vijana labda kwa umri wa miaka 16-27 wanaotaka kuingia kwenye kilimo wafanye hivyo, kama vile jeshini watu wanaingia wakimaliza secondary hivyo hivyo iwe ni utaratibu kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye kilimo wawezeshwe na criteria iwe UMRI tu!! hii itasaidia kuvuta kundi kubwa la vijana wanaotaka kujiunga na kilimo ambao wana different ‘characteristics’ or ‘backgrounds’ rich/poor,educated/non educated etc hii itaondoa stigma kuwa kilimo ni cha kwa waliofeli.
Mapendekezo yangu nini kifanyike kuwasaidia vijana waingie kwenye kilimo;
Vijana wengi wanapungukiwa na fedha kumudu gharama za kununua mashamba na kulima, kwa hili naishauri serikali ifanye utaratibu wa kuwagaia viwanja vijana mashamba, tuna ardhi ya kutosha kwa kila kijana hesabu (44 millions hectares/ 11 millions young people) . Micro loans pia zinaweza kusaidia vijana kulipa gharama za kulima.
Kuwe na team maalumu wizara ya kilimo itakayo-deal na ku explore wanunuzi wa mazao ndani na nje, sasa hivi wizara inafanya kazi kijumla sana, inabidi kitengo kigawanywe ndani ya wizara kudeal na manunuzi ya mazao.
Mafunzo kwa vijana kufanya kilimo cha kiwango kikubwa (large scale), tutoke mahali tulipo sasa ambapo wengi tunafanya ‘small scale farming’ ambayo saa nyingine ni ngumu ku ‘survive’ na pia mafunzo kutumia ‘technology’ kulima.
Kuwe na utaratibu wa kuhakikisha vijana wanabaki kwenye kilimo kwa mfano ruzuku (subsidy), ‘vouchers’ za bei rahisi ( discounted fee rates) za kununua mbegu, mbolea ambazo zimelenga au mahususi kwa vijana pekee wanaojishughulisha na kilimo.
Nyingine nawakaribisha kujazia