Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,446
Moja ya mambo ambayo madikteta hawapendi ni kukosolewa, kwa miaka ya hivi karibuni mitandao ya kijamii imekuwa njia kubwa ya kukosoa mamlaka na kuleta mabadiliko katika jamii.
Kipindi Rais Samia anaingia madarakani mitandao mingi ilikuwa na bei ndogo za vifurushi mfano, mimi nilikuwa nikinunua GB 3 kwa shilingi 2000 ambazo zilidumu kwa siku 3, hiyo ni kupitia mtandao wa Airtel.
Pia nilinunua GB 2 kwa shilingi 2000 kupitia mtandao wa Halotel ambazo zilidumu kwa siku 7.
Kwa ile miezi ambayo nilikuwa na matumizi makubwa ya internet, nilinunua kifurushi cha Vodacom cha shilingi 50,000 ambacho kilinipa gb 30 za kasi na baada ya hapo kasi inapungua lakini naendelea kutumia vizuri tu kwa siku 30 tena una stream vizuri kabisa.
Baada ya huyu mama kuingia leo tunashuhudia shilingi 2000 eti haitoshi kununua GB 1 tena mtandao wa Tigo unafanya utapeli kwa kuwauzia watumiaji wake Mb 300 na kuziita GB 1, ukitaka kuhakiki, weka app ya kufuatilia matumizi ya vifurushi vyako utagundua kuwa ni mtandao 1 tu ambao vifurushi vyake ni halisi, tena mtandao huo pia umeanza michezo michafu ya kupandisha hovyo bei.
Ninacho ona hapa, hiki si kitu cha bahati mbaya, haya yatakuwa maelekezo ya kidikteta toka juu ili tupunguze kuhoji mambo ya msingi.
Naamini uzi wangu utadumu, poleni sana kwa aina mpya ya udikteta.