MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 12,866
- 28,840
ELERAI MAJENGO ARUSHA :-
Hapo panaitwa Majengo. Ni moja kati ya mitaa inayopatikana jijini Arusha. Kuna;
Majengo ya Juu:-Temboni, Sacon, Mwisho wa Kidala, Shuma, Azimio (Hapa ndo pale azimio la Arusha lilifanyika enzi hizo na Dingi wa taifa Nyerere),Burka,nk.
Majengo ya Kati:- Mtaa Wa Ngurumo,Elerai,Sokoni,Kwa Mbaga,Urundini,nk
Majengo ya Chini:- Jengo Deki, Kwa Sefu, Kilo Ya Karatu, Lomba Ijuva, Kwa Mama Nairo,nk).,
Majengo ya Mgombani:- Mnarani kwa kina Mollel,Mabanzini,Chemchem,Kwa Mapadri,Mihambo,Matejoo,nk..
Eneo la mzingo kuzunguka Majengo nzima ni 11km (Usije na gari maana njia ni finyu a.k.a Vichochoro vingi). Majengo inapatikana kwenye latitude -3`21'57.96 na Longitude -36'40'0.12 kutoka usawa wa mstari wa Ikweta. Asilimia 56 ya wananchi ni Warangi na Wanyiramba (Wenyeji wote asili ni Waarusha). Asilimia 44 iliyobakia ni mchanganyiko wa makabila mbali mbali kuanzia Wachaga, Wapare, Wahehe, Wamang'ati, Wasukuma, Wajaluo, Wadigo, Wameru, Wambulu, Wakurya, Wasandawe, Wagosi, Wanyampaa (Mnyampaa Hair Cutting Saloon),Wangoni,nk.
Mgahawa uliokua unajulikana kuanzia mwaka 2000 kurudi nyuma ni kwa #Mama_Njeri Hotel (Maarufu kwa Chapati na Maharage yenye maji mingi) kwa shilingi 350 enzi hizo unapata Chapati 2 na maharage..Yaani mchanganuo wa hiyo 350 ilikua kama ifuatavyo :-maharage ni 150 unawekewa kwenye sahani sio bakuli, chapati 2 kwa 200 kila moja 100.. Jumla ya Chapati 2 na maharage yake ni 350 taslimu bila makato ya VAT...Ila sasa kuna mabadiliko ya Hoteli ziko mingi mpaka sizijui tena Ingawa nimezaliwa huko.. Mahali pekee uliyokuwa unaweza kupata Half-Cake kubwa zaidi duniani kwa bei elekezi ni Kivukoni Bar.
Bar iliyokuwa maarufu kwa Half-Cake mixer na mbege. Nje ya hiyo Bar kulikuwa na choo chenye ghorofa na ndo choo pekee East Africa nzima kilichokuwa cha ghorofa kipindi hicho. Ila kilivunjwa kutokana na kashfa za kipindupindu maana maji yenye kinyesi yalikuwa yanavuja toka ghorofani mpaka kwenye eneo la chipsi za Mama Abdul. Na ndio chipsi zilizokuwa bora kwa kipindi hicho,kwa bei ya shilingi 100 unajaziwa sahani... Banda la kwanza la kuonyesha video/movie lilikua kwenye nyumba ya Baba Kipese(R.I.P) na selector/Mwenye ku-Control hiyo Tv alikua ALEX akishirikiana na ndugu yake Vernus, baadae ndo zikafatia kibanda umiza, kwa Mweju mpaka Kantala pia akajulikana kwa kuonesha mechi.. Nadhani ndio mtu wa pili kufunga Dish akimfatia Mzee Bayo ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza Majengo nzima kuwa na dishi iliyojulikana kama ungo enzi hizo....
Nakumbuka mara ya kwanza kuona Computer na kuigusa ni kwa Mzee Kipese, pili mzee wetu Bob Lema na ndipo niliposhika Keyboard kwa mara ya kwanza na kuibonyeza kistaarabu.. Bob Lema ndiye mwasisi wa baiskeli za kukodisha mtaani,na nadhani ndiye mtu aliyeweza kuteka akili za watoto wengi zaidi mtaani kwa kipindi hicho (Abarikiwe sana popote alipo)..Simu ya kwanza Majengo ilikua nje ya baraza ya Cheetah Bar na ndo simu pekee iliyokua inaabudiwa kipindi hicho.. Raia wale waliokua wajanja kipindi hicho ndo walikua na kadi ya TTCL iliyokua ina-support kwenye simu hiyo (Caller Box)..
Robo tatu ya nyumba ni za udongo na kodi ya mwezi ni kuanzia 3000 na kuendelea..Pia kuna makampuni makubwa yaliyowekeza Majengo Mfano :-Makao Makuu ya Tanapa Tanzania nzima, Culture Heritage,TFSC,Family Team (Zamani Jumbo), Bush 2 Beach Safari Company, MCW,Arusha Modern School, Kimoso, Elerai IT College, Hill Top Cottage, Kanisa La AICT, Burka Estate, Sugar Land Pub,Konoike (Kwa Pateli), AVCO (Kwa Kakee),nk
Barabara kuu imetengenezwa kwa kiwango cha lami na wananchi wamebatiza mtaa jina kutoka Majengo Ya Juu kua Majengo Calfornia City (Sio rasmi Serikalini).. Watu maarufu kama Mzee Ngurumo(R.I.P Babu), Mama Musa, Kumbaa, Kasuku, Kabembera, Baba Kimbagu, Leon Butcher, Ndongaa, Priscus, Ally Bantu, Baba Ziada, Mfarisayo, Mamlai, Mzee Mkota, Mama Jerry, Mama Mzee, Teddy(Mama Jack), Esta Makandee(Anisamehe maana najua hapendi ili jina), Chege, Ali-Soo,John Ndende, Mdudu, Mgunduzi, Kingu, Mwarabu, Anasi(Jengo Deki), Tasha, Buju, Kizili, Bonge, Husna M-mbulu, Hussein Ndonga, Mama Kipese, Doto, Zungu, Mzee Manjano, Mzee Furaha, Ally Magambaa, Mekuu, Edesi, Salimu Boy, Chale muuza duka jalalani, Mwituu, Oresi, Mapee, Mzee Paulo, Baba Okinyi, Mzee Kimaro, Kinungaa, Afida, Kazeni/Maganga Gurgo, Kitwana, Mzee Benja, Jonas Benja, Mama Benja, Mau & Mudy, Mzee Ndururu,KCU (Kichwa Cha Ukoo), Mong'oo, Matumbure, Kidansa msafi, Juma Machupii, Lomba Ijuva, Kamjamaa, Magololi, Short wa Mtango, Enock, Heaven, Mama Mnema, Abeli mpiga picha, Lema, Baba & Mama Chande, Kamamaa(Dada'ake M-Lost), Makamasii, James fundi pikipiki(Baba), Mama Nasibu, Kidansa Mchafu, Makakaa,Mzee Mrewedi, Deo Mwanambilimbi, Maganga, Banzi, Serenga, Mama Serenga, Ngengai, Babu Masindai, Mama Sipe, G wa Daida, Hamis Mtoto,Ramso, Spark Dawg, Adam Mchomvu, Mapere na Makambale, Amir Mafutaa, Macho ya Paka, Magesa, Mwananchi, Mgosi, Mama Fontoo, Sheikh Khalifa,Mama Pilii,Robert Rasta,Mtei muuza Duka au maarufu kama Kauka kutokana na kukonda kwake,Nondo,Mama Faraji,Mzee Kea,Mama & Baba Kiandiko,Baba & Mama Riziki,Bwashee,Jakaranda,Papaa Mafido, Marieta, Abdala Chadema, Papa King, Mama Shiri, Swalehe a.k.a Sule G, Mkude, Mama Tedy, Mzee Mtango, Mama Tadei, Mama & Baba Kimolo, Mwenda,Mama Shafii,Chuma,Lau, Aree,Mweju,nk utawapata bila malipo yoyote.. Najivunia kuzaliwa Kwenye hizi chocho maana zimenikomaza ki-askari.. IN LOVING MEMORY of Mama Habiba,Bro Mahmud Zuberi(Mudy),Babu Kibiongo (Muuza Barafu),Mama Kisali,Mzee Msaki,Mzee Almasi,Umeme,Hamza,Kapera,Baba Kipese (Mzee Rodgers),Mama & Mzee Ngurumo(Mama & Baba Matumbure),Geofrey,Mzee Mnazi,Baba Dennis,Mama Okinyi,Mama & Baba Esta,M-Lost (Godii),Makori,Faru,Lucy(Dada),Mama Hidaya,Hidaya,Halima,Mama Fidoo,Mama Tida,Mangele,Azimio(Misti), Mzee Almasi,Mzee Bunju na wote waliotangulia mbele za haki Tunawakumbuka..
Kila raia aoneshe heshima kwa mtaa wake kwa kuandika jina la mtaa aliokulia au anapoishi kijemedari NB:- Hii listi inabidi kui-update maana watu wetu wengi wameshafariki na kutudi mavumbini..Uwanja wetu wa Urundini umeuzwa bado Chachamango..(ITAENDELEA.....)
Credit Rasta Natty Jerry Brant