Utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi za Rais Magufuli 2015 hadi 2020

Unakuwa mjinga sasa,katiba imetoa room kwa wananchi kujadili mustakabali wa taifa lao mahali popote!Iwe mitandaoni,kwenye radio,TV au mikutano yote sawa!
Mpango wa serikali hupelekwa bungeni,ndio maana nasema hakuna dira ya kutufikisha huko!Kuwa kama mwenye elimu,usitie akili zako mfukoni
Kama mwananchi unayohaki ya kujadili utekelezaji Wa serikali yako kwa maana ya kile inachokifanya kama ni kizuri au kibaya, tena unbalance na siyo kubaki kuponda tu ndipo unaonekana mwenye akili timamu siyo kutaka kujadili.mambo.ambayo kimsingi kuna mamlaka ambazo zinahusika kushughulika nayo kwa niaba yako kama mwananchi. Au haujui unachokisema hapa mbunge wako, diwani wako wrote wanakijua? Nenda kwa hao wakueleweshe badala ya kutuletea u-_kil.aza wako humu
 
Wananchi tuliopewa nguvu na ibara ya 18 na 20 ya katiba ya JMT,usiwe mjinga kiasi hicho!Kama hujui haki zako,tutakusaidia kuzitambua!
Katiba inakupa fursa ya kuomba serikali ikupe mpango uujadili kwenye social network?
 
Tr 1 inajenga km 105 kati ya 1500 . Kwa bajeti hiyo inachukua miaka 15 kumaliza reli toka dar hadi kigoma
Umesahau kuwa Serikali ya China imeahidk kutoa fedha za ujenzi wa reli hiyo
 
Kama mwananchi unayohaki ya kujadili utekelezaji Wa serikali yako kwa maana ya kile inachokifanya kama ni kizuri au kibaya, tena unbalance na siyo kubaki kuponda tu ndipo unaonekana mwenye akili timamu siyo kutaka kujadili.mambo.ambayo kimsingi kuna mamlaka ambazo zinahusika kushughulika nayo kwa niaba yako kama mwananchi. Au haujui unachokisema hapa mbunge wako, diwani wako wrote wanakijua? Nenda kwa hao wakueleweshe badala ya kutuletea u-_kil.aza wako humu
We jamaa upuuzi umekuzidi,hao uliowataja ni wawakilishi wangu bungeni!Ndio wamepewa mamlaka ya kimaamuzi,lakini kwenye suala la kujadili wananchi tumepewa Uhuru huo!Ndio maana JF kuna majukwaa mbalimbali ili kutoa fursa kwa wananchi kufanya mijadala yao ili viongozi wakipita waone na wachukue kitu!Hata kama maoni yangu huyapendi vumilia hivyo hivyo dawa iingie!Badilika usiwe mjinga
 
Katiba inakupa fursa ya kuomba serikali ikupe mpango uujadili kwenye social network?
Pitia katiba nimekuwekea hapo chini!
Unauliza maswali ya kijinga sana!Bajeti ndio zimebeba mipango ya serikali!Tumejadili bajeti humu JF,ndio maana nasema hakuna mpango utakaotufikisha kwenye serikali ya viwanda!
 
Attachments

  • katibayatanzania.pdf
    261.2 KB · Views: 18
5. AHADI; - Kuondoa kodi za Hovyo zinazowakandamiza wanyonge
UTEKELEZAJI; - Kwenye Bajeti ya 2016/17, kodi za hovyo zimefyekwa
bajeti.png
 
Kama mwananchi unayohaki ya kujadili utekelezaji Wa serikali yako kwa maana ya kile inachokifanya kama ni kizuri au kibaya, tena unbalance na siyo kubaki kuponda tu ndipo unaonekana mwenye akili timamu siyo kutaka kujadili.mambo.ambayo kimsingi kuna mamlaka ambazo zinahusika kushughulika nayo kwa niaba yako kama mwananchi. Au haujui unachokisema hapa mbunge wako, diwani wako wrote wanakijua? Nenda kwa hao wakueleweshe badala ya kutuletea u-_kil.aza wako humu
Hapo ndio nimeona udhaifu wako,huelewi unachozungumza!Tunayo haki ya kujadili hata yale serikali inayoazimia kuyafanya!Wewe unalazimisha tujadili matokeo tu,no way!
 
Hapo ndio nimeona udhaifu wako,huelewi unachozungumza!Tunayo haki ya kujadili hata yale serikali inayoazimia kuyafanya!Wewe unalazimisha tujadili matokeo tu,no way!
Unapaswa kujua mantiki ya uzi huu na si kuropoka tu
 
Pumba tupu huwezi kuendesha nchi kwa sera mufilisi za kukurupuka. Eti anapambana na mafisadi! Acheni uongo wenu huwezi kupambana na mafisadi huku Lugumi, MV Dar, UDA, Pride, escrow anawakingia kifua na kutochukua hatua yoyote dhidi ya hawa mafisadi. Once a fisadi always a fisadi hata ukiwa ndani ya Ikulu.

Wadau, amani iwe kwenu.

Bila shaka Uchaguzi umemalizika. Naamini pia Rais amemaliza kupanga safu yake ya Uongozi ngazi ya serikali. Naamini pia atakabidhiwa chama Julai 23 ili aweze kukisimamia chama kiweze kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020.

Uzi huu ni mahsusi kwa ajili ya kuweka utekelezaji wa kile alichoahidi Rais wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Tutaangaza pia na Ilani ya CCM ili ifikapo mwaka 2020, tuweze kumpima Rais wetu kwa mizania iliyo sawa.

1. AHADI; - Elimu Bure hadi Kidato cha Nne
UTEKELEZAJI; - Muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwake, Rais alifuta ada na michango yote ya shule za
Msingi na Sekondari na kwa sasa watoto wetu wanasoma Bure.

2. AHADI; - Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Standard Gauge
UTEKELEZAJI; - Shilingi Trilioni Moja imetengwa kwa mwaka wa fedha 2016/17 kama kianzio

3. AHADI; - Uanzishwaji wa Mahakama ya Majizi na Mafisadi
UTEKELEZAJI. - Jumla ya Shilingi Bilioni 2.5 zimetengwa kwa ajili ya Mahakama hiyo. Majengo
yamepatikana, wafanyakazi wa Mahakama hiyo wamepatikana

4. AHADI; - Milioni 50 kwa Kila Kijiji
UTEKELEZAJI; - Fedha hizo zimetengwa kwenye Bajeti ya 2016/17. Vijana wanahamasishwa kuunda
Vikundi ili wapatiwe mafunzo ya Ujasiriamali ili wanufaike na fedha hizo

5. AHADI; - Kuondoa kodi za Hovyo zinazowakandamiza wanyonge
UTEKELEZAJI; - Kwenye Bajeti ya 2016/17, kodi za hovyo zimefyekwa hasa kwenye mazao ya Biashara

6. AHADI; - Umeme wa kutosha na wa Bei nafuu
UTEKELEZAJI. - Gharama za Ankara za umeme zimepunguzwa. Pia Service Charge imeondolewa
7. Ahadi: - Kuhakikisha wanafunzi hawakai chini....
Utekelezaji: - Madawati ya kutosha yametengenezwa na ahadi hii imetekelezwa kwa zaisi ya Asilimia 90

Wadau. Huu ni mwanzo tu na nitaendelea kuweka updates kwa kila ahadi itakavyotekelezwa. Kwa yale ambayo sijayaainisha humu, nawaomba wadau mnikumbushe nani nita update mara kwa mara.
 
Pumba tupu huwezi kuendesha nchi kwa sera mufilisi za kukurupuka. Eti anapambana na mafisadi! Acheni uongo wenu huwezi kupambana na mafisadi huku Lugumi, MV Dar, UDA, Pride, escrow anawakingia kifua na kutochukua hatua yoyote dhidi ya hawa mafisadi. Once a fisadi always a fisadi hata ukiwa ndani ya Ikulu.
Mkuu, kama unakataa moja tu la kupambana na ufisadi lakini umeunga mkono hoja nyingi haina neno
 
Lizaboni habari yako, asante kwa update nzuri, naomba ulete mafanikio kwenye upatikanaji wa maji, japo huku kwetu tuna enjoy kwakuwa tangu rais wetu aingie madarakani maji yanatoka karibia kila uchao, asante baba Magufuli na asante ccmkwa kutuletea rais muadilifu na mchapa kazi. Mungu ibariki serikali ya awamu ya tano na Tanzania yetu.
 
Wapi nimeunga mkono hata hoja moja wewe? Acha kukurupuka. Hapa ni majanga tu. Huwezi kuendesha nchi kwa sera za kukurupuka na kubaka demokrasi huku ukiwakingia kifua mafisadi halafu ukategemea kupata mafanikio.

Mkuu, kama unakataa moja tu la kupambana na ufisadi lakini umeunga mkono hoja nyingi haina neno
 
Ni mwanzo wa matumaini sana,na ukizingatia bado pia pamoja na kupanga bajeti kama.hiyo,ndugu Lizabon,rais anaonekana bado na wembe ule ule kukabiliana na ufisadi,nuru ileee naiona Tanzania mpya
 
Back
Top Bottom