Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY




SEHEMU YA NNE




Katika sehemu iliyopita nilieleza kuhusu vipimo vya Parrafin vilivyoleta majibu negative baada ya Oswald kupimwa na ili kumuangalia kama ana GSR kutoka kwenye bunduki iliyodaiwa kutumika kumuua Rais Kennedy.

Niliahidi kueleza kuhusu utata juu ya ufyatuaji risasi kutoka jengo la Texas School Books Depository.


Tuendelee…



UTATA WA RISASI ILIYOMUUA RAIS KENNEDY


Ili twende pamoja katika hiki ninachotaka kukizungumza nitashauri mara kadhaa urejee video niliyoiweka juzi iliyomuonyesha Rais Kennedy akipigwa risasi.

Pia nianze kwa kueleza suala muhimu kuhusu urekodiji wa 'video' kwa faida ya wote.

Ni kwamba, katika teknolojia ya kurekodi video kuna kitu kinaitwa frames. Kwa lugha rahisi kabisa, frames ni picha mnato ambazo zinaunda video. Ndio kusema kwamba, kipande kifupi cha video kina Picha mnato mamia kadhaa. Au kwa lugha nyingine nyepesi zaidi ni kwamba video ni muunganiko wa maelfu ya picha mnato zilizorekodiwa katika mtiririko wa kufuatana.

Ukiangalia ile video niliyoweka juzi (nimeiweka tena hapo chini) utaona upande wa juu kulia kuna namba zinatokea na zinaenda kama zinahesabu hivi. Namba zile zinakuonyesha muda huo husika unaangalia frame namba ngapi ya kipande hiki cha video.

Suala hili la kuelewa tukio gani limetokea frame namba ngapi kwenye kwenye video lina umuhimu wa kipekee sana kwenye kuelewa utata wa tukio hili la kuuwawa kwa Rais Kennedy kama ambavyo nitaeleza leo katika sehemu ya hii makala.


Sasa,

Nilieleza kuwa serikali kupitia Warren Commission wanashikilia msimamamo kuwa Oswald alitekeleza tukio peke yake kwa utashi wake pasipo kushirikiana na mtu yeyote yule. Serikali inashikilia msimamo huu ili kupinga msimamo wa wengi kuwa tukio hilo lilipangwa na watu na yawezekana kabisa ni watu wenye nguvu kwenye 'system'.

Pia nikumbushe nilipoandika kuhusu namna rais alivyopigwa risasi nilieleza kuhusu risasi ya kwanza kumpata ilitokea kooni/kifuani na kwenda kumpata Gavana Connally sehemu ya nyuma ya mgongo kulia chini kidogo ya kwapa na kumsababishaia majeraha makubwa tumboni, mkononi na kwenye paja.

Nadharia hii ya risasi moja kisababisha yote haya inaitwa "Single Bullet theory", kwamba risasi ya kwanza kumpata Kennedy ndio risasi hiyo hiyo ilimpata Gavana Connally.

Lakini kuna mazingira yanayoa ashiria kwa uthibitisho mkubwa kwamba Connally hakujeruhiwa na risasi ambayo ilimpata Kennedy mara ya kwanza.

Tuangalie hivi,


Ukitazama video katika frame ya 224 ni dhahiri kwamba huu ndio muda ambao risasi ya kwanza ilimpata Kennedy.

Hapa ndipo ambapo Kennedy anashtuka kwa maumivu na kunyanyua mkono wake wa kulia na kuukunja ngumi na kuuinua usawa wa mdomo.

Katika muda ambao frame 224 inaishia ndipo ambapo Connally anaonekana kushtuka pia kisha anageuka upande wa kulia na kujitahidi kugeuka nyuma kana kwamba anajaribu kumuangalia Rais Kennedy.

Katika frame hii Gavana Connally haonyeshi dalilo yoyote ya kuwa katika maumivu (licha ya kushtuka).
Pia kuna dalili kadhaa zinaonyesha kuwa si muda huu ambapo alipigwa risasi.
Mfano ukimuangalia mkononi bado ameshikilia kofia yake ya 'pama'. Kama unakumbuka nilishaeleza huko mwanzoni kwamba moja ya sehemu ya mwili wa Gavana Connally ambayo risasi ilipenya ilikuwa ni sehemu ya juu ya kiganja chake cha mkono wa kulia na mfupa wake kupasuka katika vipande vinane.
Kwa hiyo haitegemewi mtu ambaye kiganja kimegawanyika katika vipande vinane aendelee kuwa na uwezo wa kushikilia kitu mkononi.

Lakini pia, kingine kinachothibitisha kuwa Connally hakupigwa risasi katika frame ya 224 ni kauli ambayo aliwahi kuitoa yeye mwenyewe. Namnukuu;

"..nilisikia mlio ambao mara moja nikang'amua kuwa ulikuwa ni mlio wa risasi. Nikashtuka na kugeula upande wa kulia kwa sababu nilihisi mlio bunduki ilikuwa imefyatuliwa kutoka upande huo. Lakini sikuona kitu chochote, niliona tu kundi la watu wanatupungia mikono. Nilipokata jicho kumuangalia rais nyuma yangu sikuweza kumuona bara bara…. nilikuwa nataka nimuone rais ili kujua usalama wake kwa kuwa niliposikia tu mlio wa risasi hisia zangu ziliniambia kuwa kulikuwa na jaribio la mauaji ya rais..."





Tazama tena video kwa kuzingatia "frames" (zinaonyeshwa upande wa juu kulia) ili kuelewa zaidi kuhusu utofauti ya frames niliouzungumza hapo juu kuonyesha kuwa Kennedy anaonekana alipigwa risasi frame ya 224 na Connally alipigwa risasi frame ya 275


Connally anaeleza kuwa baada ya hapo akawa anaanza kugeuka na ndipo ambapo alisikia maumivu kifuani na alihisi kuwa amepigwa risasi ambayo hata hakuisikia mlio wake.

Maelezo yake yanathibitishwa na ukiangalia kipande cha video, Connally anaonekana akitunisha mashavu kama anapuliza hewa nje na kukunja uso kwa uchungu katika frame ya 275 kuonyesha kwamba risasi ilikuwa imempata muda huu.


Sasa, kwanini nasisitiza na kuonyesha vidhibiti kuwa risasi iliyopata Kennedy katika frame ya 224 haikumpata Connally??

Ni kwamba, serikali kupitia Warren Commission wamekuwa wakieleza kuwa risasi iliyopata Kennedy ndiyi hiyo hiyo ilitokeza kifuani kwake na kwenda kumpiga Connally.

Ili hoja hii iwe sahihi maana yake ni kwamba kwa kuzingatia kasi ya mwendo wa risasi, tukio hili (risasi moja kumpiga Kennedy na Connally) lingetokea ndani ya 1/100 ya sekunde (sekunde moja gawanya kwa mia moja). Na tukio linalotokea ndani ya 1/100 ya sekunde haliwezi kurekodiwa kwenye frames tofauti ni lazima litatokea kwenye frame moja ya video.
Kutoka frame namba 224 ambayo Kennedy anapigwa risasi mpaka frame namba 275 ambayo Connally anaonyesha kuanza kuugulia maumivu ni takribani interval ya theluthi ya sekunde.

Theluthi ya sekunde ni muda mwingi sana kwa risasi moja kusafiri kutoka kwa Kennedy kumpata Connally.
Maelezo pekee ya kuelezea hili ni kwamba risasi ya kwanza kumpata Kennedy haikumpata Connally. Zilikuwa risasi mbili tofauti.
Lakini pia theluthi ya sekunde haitoshi kufyatua risasi mbili kutoka katika bunduki aina ya Mannlicher Carcona. Ukipiga risasi unahitaji kusubiri sekunde kadhaa ili 'kuikoki' tena bunduki na uweze kupiga tena, kwa kifupi ni kwamba kwa namna yoyote ile au muujiza wowote ule haiwezekani kufyatua risasi mbili ndani ya theluthi ya sekunde kutoka katika bunduki ya aina hii.

Kwa hiyo hii inatueleza kwamba risasi iliyompiga Kennedy na iliyompiga Connally zilikuwa risasi mbilo tofauti na zilipigwa kutoka kwa watu wawili tofauti.



Swali ni kina nani watu hawa??


Kabla hatujafika mbali kuanza kujiuliza ni nani mwingine labda alifyatua risasi nyingine hebu tuangalie vidhibiti zaidi.


Baraza la Senate liliwahi kuunda kamati ya kuchunguza mauaji mbali mbali ya kupangwa yaliyowahi kutokea nchi Marekani. Kamati hii iliitwa House Select Committee on Assassinations au kuwa kifupi kama HSCA
Moja wapo ya chunguzi walizofanya ni kuhusu mauaji ya Rais Kennedy.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alikuwa ni mtaalamu nguli wa patholojia, Dr. Cyril Wecht.

Dr. Wecht aliandika andiko la maoni yake kwa kamati hii teule ya Senate na akawaeleza kuhusu nadharia aliyokuja nayo kuhusu tukio hilo ambayo nadharia hii ilikuja kujulikana kwa wengi kama "Right to Left trajectory ".

Kama nilivyoeleza kwamba, serikali kupitia Warren Commission wanadai kuwa risasi zilipigwa na Oswald akiwa mkono wa kulia wa jengo la Texas School Books Depository.

Katika andiko lake kwenda kwa HSCA, Dr. Wecht anaeleza kwamba kwa kuzingatia kuwa ripoti ya serikali inaeleza kuwa risasi ilifyatuliwa kutoka ghorofa ya sita kutoka kwenye jengo tajwa, na pia kuzingatia upande wa jengo ambao unaelezwa Oswald alikaa, kwa maoni yake haiwezekani kwa risasi hiyo iliyompata Kennedy upande wa kulia pia kumpata Connally upande wa kulia wa ubavu chini kidogo ya kwapa

Kwanini?

Ukipima pembe mlalo (horizontal angle) kutoka jengo la Texas School Books Depository kwenda kwenye gari aliyomo rais na mahali ilipokuwa katika frame 190 ya kipande cha video unapata nyuzi 13 (kutoka kushoto kwenda kulia).
Papo hapo pia ukipima pembe wima (vertical angle) kutoka ghorofa ya sita kwenda kwenye gari ya Rais unapata nyuzi 21 kama utapima kwa kuchukulia kuwa bara bara ilikuwa tambarare iliyo sawa (horizontal plane) lakini kama ukizingatia kuwa gari la rais lilikuwa linapita kwenye bara bara yenye 'slope' ya nyuzi 3 maana yake kwamba pembe wima ya kutoka ghorofa ya sita mpaka kwenye gari ya Rais inakuwa ni nyuzi 18.

07d283952701031934077434b348fe85.jpg

Position ambayo Warren Commission wanadai Oswald alikaa katika jengo la Texas School Books Depository... (Duara la juu kabisa)

d9d2c316a7d861115b4fa2cacff7e8d2.jpg

Namna ambavyo inatarajiwa Oswald alikuwa akiuona msafara wa Rais kama alikaa hapo inapoelezwa na Warren Commission.... Angalia namna ambavyo kuna mti unamkinga kutopata "clear sight" ya target yake na pia kumbuka msafara ulikuwa uko kwenye mwendo... Ni ngumu mno kuweza kudungua target kutokea hapa na kuzingatia target anatembea (mtu kwenemye gari) na alafu hizo shots zipigwe kwa haraka haraka... FBI Marksmen walio bora kabisa wamejaribu kwa miaka kadhaa ku-recreate zile shots tatu zinazodaiwa kupigwa na Oswald kwa muda ule ule (chini ya sekunde 6) na kumpata target lakini mpaka leo hii hawajawahi kufanikiwa..


c00fc1055b0a2ba30ed570203e935f91.jpg

Namna ambavyo tunatarajia shots tatu kutoka ghorofa ta sita zingesafiri... (trajectory)

9f9fb86f21014f9e6f9f062cdaa608e1.jpg

Tazama kwa makini umbali na 'angle' kati ya jengo la Texas School Books Depository na mahali shots zilipotua (alama nyekundu kwenye Picha)


Sasa, ifahamike kuwa namna ambavyo Rais Kennedy alikaa kwenye siti yake alikuwa amekaa kuegemea kabisa kwenye mlango wa gari na hata ukiangalia video kuanzia mwanzoni utaona akiwa ameweka mkono juu ya mlango wa gari. Lakini Gavana Connally alikuwa amekaa katikati ya siti yake mbali kidogo na mlango wa pembeni yake.

Hivyo basi kwa kuzingatia 'trajectory' ya risasi kutokana na nilivyoeleza position ya mdunguaji kule juu, Dr. Wecht anaweka hitimisho kwamba, kama risasi iliyompiga Kennedy ndiyo pia ilimpiga Connally basi ilitakiwa impate upande wa kushoto wa uti wa mgongo na sio kulia kama ambavyo ilitokea.

Kwa hiyo hii inatupa vidhibiti kingine kwamba kuna kila dalili kwamba kulikuwa na zaidi ya mdunguaji mmoja.



Ni nani huyo mdunguaji/wadunguaji mwingine???


Lakini pia, tuvute subira labla ya kujiuliza tena swali hili, tutazame kidhibiti kingine.

Huko nyuma nilieleza juu ya mzozo uliotokea Parkland Memorial Hospital baada ya madaktari kugoma mwili wa Kennedy kuondolewa pasipo kufanyiwa autopsy lakini Kenneth O'Donnell na maafisa usalama wakatumia mabavu kuondoka nao mwili wa rais bila kufanyiwa autopsy.

Kwanza hii inatia mashaka kuwa pengine kuna kitu ambacho madaktari wangekiona katika autopsy na kuvuruga kabisa kilichokuwa kimepangwa au maelezo ambayo tayari yalikuwa yameandaliwa na wauaji wa Kennedy kuaminisha ulimwengu.

Lakini hata hivyo bado kuna vitu kadhaa muhimu ambavyo vinaonekana katika cheti cha kifo kilichotolewa hospitali ya Parkland.

Kwa mfano katika kwenye cheti inaonyesha kwamba Kennedy alipigwa risasi katika usawa pingili ya tatu ya shingo kwenda chini. Lakini katika ripoti ya Warren Commission wameongeza karibia inch tano au sita kwenda juu na kuripoti kuwa alipigwa risasi katika 'base of the neck'.
Hii inatoa hisia kwamba walikuwa wanalazimisha kuweka usawa huu wa risasi kuingia ili waweze kuhalalisha wanachokilazimisha kwamba risasi hiyo hiyo ikaenda kumpiga Connally ubavuni chini kidogo ya kwapa la kulia.

Kama tukizingatia kilichoandikwa kwenye cheti cha kifo kwamba risasi ilipigwa katika 'third thoracic vertebrae' basi isingelimpata Connally ubavuni chini kidogo ya kwapa.


Pia daktari wa zamu ambaye alimpokea Kennedy siku hiyo hospitali, Dr. Robert N. McClelland anaeleza kuwa walipokuwa wanajitahidi kuokoa maisha ya rais, alipomuangalia nyuma ya kichwa kidonda alichokiona kwa utaalamu wake kilikuwa ni 'exit wound' (kidonda risasi ilipotokea).
Kwa hiyo hii ina maanisha kwamba risasi iliingilia mbele na sio nyuma kama inavyodaiwa kwenye ripoti ya Warren Commission.

Hii pia inathibismtishwa hata ukiangalia video.
Rais Kennedy anapopigwa risasi ya pili anaonekana dhahiri kichwa kikisukumwa na risasi kurudi nyuma kwa kishindo. Na si hivyo tu hata kipande cha fuvu la kichwa kilichofumuliwa kinadondokea kwenye 'bodi' (trunk) ya nyuma ya gari.

Pia kiwango kikubwa cha ubongo kinarushwa nyuma ya gari na kudondokea kwenye follow up car ya wanausalama na kiwango kingine kinawadondokea hata mapolisi wa pikipiki waliopo nyuma.

Mojawapo wa mapolisi hawa wa piki piki Bobby Hargis, aliyekaa mkono wa kushoto nyuma ya gari ya Rais, anaeleza kuwa alidondokewa na kiwango kikubwa cha ubongo kilichoruka katika kasi kubwa na kutua kwa kishindo mwilini mwake kiasi kwamba alidhani labda naye amepatwa na moja ya risasi zilizokuwa zinapigwa.


Hii yote inazidi kututhibitishia kuwa kulikuwa na waduanguaji zaidi ya mmoja katika tukio na mdunguaji aliyepiga risasi iliyomuua rais (fatal shot) alikuwa amekaa mbele ya msafara au mkabala nao lakini kamwe sio nyuma, tena juu ya ghorofa.


Kwa hiyo swali linarudi tena, ni akina nani hawa walimdungua rais??



Natamani tuwe na subira tena tuangalie kidhibiti cha misho kwa sasa (tutaviongelea vingine huko mbeleni mwa makala).


bf9ca552059c9a4e5be14c10cd66898a.jpg

Cheti cha kifo cha Rais Kennedy ambacho kilitolewa na Parkland Memorial Hospital siku ya November 22, 1963


Ushahidi wa Abraham Zapruder

Mpaka kufikia kusoma makala hii ni imani yangu kuwa lazima umewahi kuona video inayoonyesha mauaji ya Rais Kennedy.

Video hii imerokodiwa na mtu anayeitwa Abraham Zapruder. Hii ndio sababu ya kipande hiki maarufu cha video kuitwa "Zapruder Film".
Huyu alikuwa mi mwananchi wa kawaida tu ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na shabiki wa Rais Kennedy.

Kutokana na napenzi yake makubwa kwa Rais Kennedy alipojitokeza barabarani kwenda kumlaki rais kama wananchi wenzake wengine, aliamua kwenda na kamera yake ya matumizi ya nyumbani aina ya Bell & Howell Zoomatic Director Series (model 414 PD) ambayo aliinunua mwaka 1962.


Baada ya kurekodi tukio la kuwasili kwa rais na kwa bahati kufanikiwa kurekodi namna rais alivyopigwa risasi na baadae mkanda wake wa video kuchukuliwa na maafisa usalama.
Kuna memo iliyoandikwa kwa mkono na afisa wa Secret Services ambayo iliwahi kupatikana na kufanya Zapruder kuitwa kutoa ushahidi pindi Warren Commission ilipoundwa.

Memo hii iliandikwa siku ya tukio November 22, 1963 kutoka kwa Agent Maxwell D. Phillips kwenda kwa Agent James Rowley.
Katika hiyo memo Agent Phillips anamueleza Agent Rowley kuwa "..kwa mujibu wa Mr. Zapruder, mdunguaji alikuwa nyuma ya Mr. Zapruder.."

Ikumbukwe kwamba Zapruder alikuwa anarekodi msafara akiwa kwa mbele (mbele ya msafara pambeni barabarani) na kipindi rais anapigwa risasi alikuwa karibia mkabala na gari la Rais. Kwa hiyo kuamini kwake kuwa mdunguaji alikuwa mahali fulani nyuma yake ilikuwa inathibitisha tena kwamba aliyemdungua Rais hakuwa juu ya ghorofa la Texas School Books Depository.

Zapruder alipoitwa mbele ya Warren Commission aeleze kwa nini alihisi kuwa mdunguaji alikuwa mahali fulani nyuma yake, alisema kwamba alipokuwa anarekodi alipata fursa ya kuona kwa uzuri zaidi nini kilikuwa kinatokea. Kwanza aliona fuvu la mbele la rais linafumuliwa na kisha kichwa cha Rais kutupwa nyuma kwa kishindo kikubwa kuashiria kwamba risasi ilimpata kwa mbele.

Pia Zapruder akaeleza jambo ambalo pengine watu wachache waliokuwepo kwenye tukio waliliona, akasema kwamba… sekunde chache baada ya risasi iliyomdungua Rais, aliona kundi la maaskari wanakimbia kuelekea mahali fulani nyuma yake na aliamini kuwa nao wameng'amua kuwa mdunguaji alikuwa huko.


Ushahidi wa Zapruder una nguvu kubwa sana katika suala hili, kwani licha ya watu wengi kuwepo sehemu ambapo Rais Kennedy alidunguliwa kwa risasi lakini pengine yeye ndiye alifauatilia kwa umakini zaidi tukio hilo sekunde kwa sekunde na hata kulirekodi na mpaka leo hii kuwa ndio rekodi pekee ya video iliyopo juu ya tukio lile.


Huyu bwana nitamuongelea kwa upanza zaidi huko mbeleni na namna ambavyo alifarikia kwa "utata" miaka michache baadae, na si yeye pekee bali pia wenzake kadhaa ambao walikuwa watu muhimu sana kwenye kutatua kitendawili cha kifo cha Kennedy, watu kama Jack Ruby (aliyemuua Oswald hadharani) na Clay Shaw (asset wa CIA aliyeropoka kuhusu njama ya kumuua rais) nao walifariki vifo vya kutia shaka sana miaka michache baadae.
Mfano Zapruder alifariki kwa "kansa ya tumbo", Jack Ruby alifariki kwa " kansa ya oafu", na Clay Shaw alifariki kwa "kansa ya pafu" ambayo ilienea kwenye ubongo na ini.

Wote walipata hizi "kansa" miaka michache baada ya tukio na ndio ulikuwa muda ambao wananchi wamechachamaa nchini Marekani kutaka kujua ukweli wa nini kilitokea.


Lakini maneno yake Zapruder kupitia ushahidi alioutoa mbele ya Warren Commission, yanaturejesha tena katika dalili zinazoonyesha na kuthibitisha kuwa kulikuwa na wadunguaji zaidi ya mmoja siku ile tofauti na serikali wanavyotaka tuamini.!!


Hii pia inaturejesha tena kwenye swali letu la msingi, watu hawa walikuwa akina nani?? Na zaidi ya yote kwanini walifanya vile???





264647964cda77efca8724cfbd4b406c.jpg

Ili kuweza kupata shot kama hii ya video ni dhahiri kwamba Zapruder alikuwa amekaa mishaps na gari ya msafara na ulitokea mbele yake}


89f322de0991c21dd11b2485357d3fdd.jpg

ThPicha hii ilipigwa na moja ya wananchi waliojitokeza kumlaki Kennedy... Inaomuonyesha Zapruder kwa mbali akiwa eneo ambalo alikuwa anarekodi msafara

04bfe802f235bfb93f304d726391d011.jpg

Abraham Zapruder (kulia) akifanyiwa mahojiano




Itaendelea....


The Bold - 0718 096 811
 
SEHEMU YA NNE


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden



bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush K NI K dagii middle east Elly Andrew nyakubonga zakaria ramadhani
 
Back
Top Bottom