Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Nafikiri chuki ikizidi inapoteza umakini wa kufanya jambo,paskali uwafungulie uzi siku nyingine nao wawe makini,zaidi ya hapo baba kijana ataendelea kutimua mbio zake za kawaida kumshinda mwanawe!
 
Nchi inahitaji maendeleo ya watu ...tumejichelewesha sana kusaka kiki za demokrasia kwani ndio upuuz waliotaka tuufikirie.

Kwa hiyo hayo maendeleo ya vitu yanaletwa kwa kunajisi box la kura? Kuna uzi huku jukwaani unasema kama tunajenga miradi kwa pesa zetu za ndani iweje, deni la taifa lipande kwa 20t ndani ya miaka minne? Nenda huko maana sio mada ya kidemokrasia, praise team wenzako huko wanatukana tu maana hawana majibu. Mada hii tuachie tunaojadili demokrasia.
 
Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.

Hata akisema hivyo haitasaidia maana wapiga kura wengi hatujajiandikisha kwa sababu tulijua fika uchaguzi utahujumiwa, na hilo limedhihirika.
 
Daraja la juu la ubungo litanisaidia Nini mkulima wa chikichi Kigoma?
Hizi ni dalili za ubinafsi wa kipuuzi!!! Hujui kuwa gharama kubwa inayotokana na matumizi makubwa ya nishati ya mafuta kwenye foleni pale makutano Ubungo itapungua sana!? Upungufu huo utasidia ela zilizokuwa zinatumika kununulia mafuta za zitatumika kununulia vitu vingine vya muhimu kwa watanzania wote hata na huyo mkulima wa chikichi Kigoma!?

Acha ubinafsi wa kipuuzi!!!
 
Nchi inahitaji maendeleo ya watu ...tumejichelewesha sana kusaka kiki za demokrasia kwani ndio upuuz waliotaka tuufikirie.
Africa kuna nchi gani ilikuwa na maendeleo ya watu kama Libia, nchi gani taja moja tu. Lakini kutokana na kukosekana kwa demokrasia tumeona nini kimetokea hadi sasa wananchi wamebaki madhalili. Demokraisia si jambo la kupuuza hata kidogo.
 
Paskali,
"Law of probability," inakataa kuwa katika makundi mawili mathalan yanajaza form zilizo sawa na wajazaji wa makundi hayo wawili wanafanana kwa kila hali katika sifa zao pakawa makosa yawe yanafanywa na kundi moja tu.

Hili kisayansi haliwezekani kabisa kwa asili 100.

Lakini tujaalie kuwa hili limewezekana ingawa sijui "control" gani itumike.

Tatizo litakuwa limehamia kwenye "Law of Probability," itabidi sheria hii yenyewe iangaliwe upya ili paweze kupatika maelezo na huu si utafiti mdogo.

Kwa ajili hii basi ya hayo niliyoeleza hapo juu hivyo vifungu vya sheria havina maana yeyote ikiwa utatumia, "Law of Probability," nikikusudia sayansi namba kutegua tatizo hili.

Kwa nini basi hayo yametokea?

Jibu ni kuwa kutakuwa na, "intervening cause."

Sasa hapa mwanasayansi uwanja ushafunguka atakapofikia kujua hili katika utafiti wake kitakachofuatia ni kutafuta sababu ya matokeo haya ya makundi mawili yaliyo na sifa sawa lakini moja lijitokeze na kuonekana hodari na hili lingine liwe "mbumbumbu," limesheheni watu wajinga hawawezi hata kujaza taarifa nyepesi za majina na anuani za nyumba zao wenyewe wanazoishi miaka na miaka.

Hawa "mbumbumbu," kwa miaka mingi wamekuwa viongozi katika jamii wakiwaongoza watu.

Hapa yanahitajika maelezo.
1111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111111
 
Pascal kiukweli pamoja na yote jpm aliyoyafanya uliyoyataja hapo huyu mtu HAKUBALIKI, na hili yeye mwenyewe analifahamu fika na watu wake Serikalini, na pale Lumumba wanalifahamu fika..

Sasa vigisu zote hizi za nini basi.. anajua fika kwenye free and fair election (ambayo kwanza haipo) kwenye Uchaguzi unaosimamiwa na TAMISEMI ambayo ipo Ofisi yake atashindwa tu..

Ndio chanzo cha kufanya ujinga wote huu.

Niliwahi kuandika huko nyuma, naomba niandike tena hapa, wagombea Urais wa Nchi wawe seriously wanapimwa AFYA ya akili kabla ya kupitishwa na NEC. Nchi inaweza kuongozwa hihivi na KICHAA.
Hakubaliki kwani uchaguzi wa urais huo? Kujaza mkosee nyie lawama mumpe magu. Mjitafakari muache kuishi kwa mazoea.
 
Swali zuri sana! Unasema unajenga reli nzuri, meli, ndege safi, flyover, umeme rufiji nk na kuhisi unapendeka sana. Lakini anajitokeza "mwehu" mmoja anaanzisha uzushi kuwa u mgonjwa taabani au umetangulia mbele ya haki na hao uliodhani wanakupenda wanageuka washangiliaji au wanatabasamu kwa habari hizo bado utaendelea kusema hayo uliyofanya ndio mahitaji ya wananchi wako? Huwezi kubaki na fikra hizo kama unatumia akili.
Huo mfano wa Gaddafi ndio sahihi kabisa, na hilo linadhibitisha kuwa kama uchaguzi ni wa haki na huru uwezekano wa CCM kuambulia hata 30% ni mashaka.
Pascal, hivi kiongozi mtaani kwangu namjua ni mpenda rushwa, kiburi na hana maono utendaji wa Magufuli unambebaji katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa?
CCM wamejiwahi, walikuwa wanagaragazwa haijapata kutokea katika historia yake.
Hujamuelewa Paskal, ameandika kwa mfumo wa fasihi, kimsingi Paskal anamkejeli tu mwananzengo mwenzake kama anaamini yeye ndio ajaye aache Watanzania wachaguwane kwa haki watamduwaza kwenye sanduku LA kura.

Kilichowazi kwa sasa ccm haina imani na Watanzania, sijui unaelewa lugha hii? Si kwamba tu Watanzania hawana imani na ccm, Bali ccm pia haina imani na Watanzania.
 
Walio Jitoa Ni Wachache Sana kuliko walio Ondolewa. A.C.T Walio ondolewa ni 94%, CHADEMA Ni 82 % kama sikosei.

Je! Hapo Kuna Uchaguzi Au Kuna Uchafuzi?.
Ziliwekwa taratibu ili zifuatwe. Ukishindwa kiziguata, unaondolewa tu. Hata Bunge la Congress la Marekani sasa liko kwenye mchakato wa kutaka kimuondoa Rais Trump madarakani kwasababu amekiuka utaratibu. Simple!
 
Baada ya Gaddafi kufa libya imekuwa na demokrasia?
Haikuwa kwa sababu hakueka misingi mizuri tangia mwanzo ya kidemokrasia amesabisha chuki kwa wananchi na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Unapoanzisha makundi mawili moja unalifavor na jengine unalikandamiza matokeo yake baada ya muda wale wanaokandamizwa watakuja juu na wakifanikiwa lile kundi jengine wataona haiwezekani. Hapo ndio msingi wa vita unapoanza so inatakiwa misingi ya haki na uwazi iwepo mapema ili kila mmoja aone thamani yake.
 
P sio kwamba hapendi kutoa uhuru huo ila anajua nn kitatokea chama kishapotea mvuto ndio njia pekee ya kujinasua pia sio kila mtu anaweza kuhimili presssure ya matokeo katika uchaguzi huru chochote chaweza tokea.
 
Hizi ni dalili za ubinafsi wa kipuuzi!!! Hujui kuwa gharama kubwa inayotokana na matumizi makubwa ya nishati ya mafuta kwenye foleni pale makutano Ubungo itapungua sana!? Upungufu huo utasidia ela zilizokuwa zinatumika kununulia mafuta za zitatumika kununulia vitu vingine vya muhimu kwa watanzania wote hata na huyo mkulima wa chikichi Kigoma!?

Acha ubinafsi wa kipuuzi!!!
Miaka nenda rudi ambayo sisi tumekuwa tukiishi taabuni Ni sababu ya foleni ya Ubungo kumaliza hela za serikali?
Ninachojua Mimi Ni hiki, ili nchi ipate pesa nilazima iuze vitu nje. Bila kuuza vitu nje hamna pesa itakayoingia.
Ninachosema Mimi serikali iboreshe miundombinu c, tupate pembejeo kwa gharama nafuu, tulime kwa wingi (massive production) ili tuweze ku enjoy economies of scale, na tuweze kusafirisha bidhaa zetu kwa wepesi, zifike kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kwa wakati.
Huwezi kuendesha nchi wala kuhudumia taifa lako kwa kutegemea hela ya kubana matumizi ya mafuta, hizo ni fikra za kifukara kabisa na za kibwege.
 
Hata akiwasamehe wapinzani wasikubali ,wakikubali ndo mwisho wao na 2020 wakaze moyo wajitoe tena japo najua ni ngumu kwa kuwa wengi wanategemea siasa kuishi
Huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza tatizo na kulitatua ili apate umaarufu zaidi. Sitashangaa nikisika Dr Abasi akisema “Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli amewasamehe wote waliojaza fomu kimakosa”.
 
Paskali,
"Law of probability," inakataa kuwa katika makundi mawili mathalan yanajaza form zilizo sawa na wajazaji wa makundi hayo wawili wanafanana kwa kila hali katika sifa zao pakawa makosa yawe yanafanywa na kundi moja tu.

Hili kisayansi haliwezekani kabisa kwa asili 100.

Lakini tujaalie kuwa hili limewezekana ingawa sijui "control" gani itumike.

Tatizo litakuwa limehamia kwenye "Law of Probability," itabidi sheria hii yenyewe iangaliwe upya ili paweze kupatika maelezo na huu si utafiti mdogo.

Kwa ajili hii basi ya hayo niliyoeleza hapo juu hivyo vifungu vya sheria havina maana yeyote ikiwa utatumia, "Law of Probability," nikikusudia sayansi namba kutegua tatizo hili.

Kwa nini basi hayo yametokea?

Jibu ni kuwa kutakuwa na, "intervening cause."

Sasa hapa mwanasayansi uwanja ushafunguka atakapofikia kujua hili katika utafiti wake kitakachofuatia ni kutafuta sababu ya matokeo haya ya makundi mawili yaliyo na sifa sawa lakini moja lijitokeze na kuonekana hodari na hili lingine liwe "mbumbumbu," limesheheni watu wajinga hawawezi hata kujaza taarifa nyepesi za majina na anuani za nyumba zao wenyewe wanazoishi miaka na miaka.

Hawa "mbumbumbu," kwa miaka mingi wamekuwa viongozi katika jamii wakiwaongoza watu.

Hapa yanahitajika maelezo.
Asalaam Aleykum mzee wangu, out of topic, hivi hamuwezi kumuomba Sheikh Alhad Musa awaombee masheikh wetu wa Uamsho watolewe gerezani? Watakaa huko mpaka lini? Hivi huyu sheikh Alhad kila siku yupo ikulu anashindwa kuwatetea masheikh wenzake waachiwe wakati mpaka wabakaji Babu seya wameachiwa?
 
Back
Top Bottom