Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,660
- 119,278
Wanabodi,
Tangu kuanza kwa pilika pilika za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sijawahi kuzungumza lolote kuhusu uchaguzi huu kutokana na kuwa bize na shughuli za kitaifa, kwanza ni Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika kitaifa mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kufuatiwa na Wiki ya Azaki iliyomalizika jana Jijini Dodoma, hivyo leo ndio nimepata fursa kuendelea na zile makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa".
Mada kuu kuhusu makala ya leo ni hizi figisu figisu za uchaguzi serikali za mitaa zinazoendelea na zilizopelekea Chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema, kujitoa kikifuatiwa na Chama cha ACT Wazalendo kwa hoja za kutotendewa haki. This is not good at all kwa mustakabali mwema wa taifa letu, kwasababu kama ni kweli hawakutendewa haki, machozi ya kilio cha haki husababisa a very bad karma kwa taifa letu, na ubaya wa karma sio tuu inaweza ku hit taifa letu kama taifa, lakini karma ina tabia ya ku hit at individual level kwa baadhi ya viongozi wetu individuals if they have a hand kwenye haya yanayotokea.
Hapa naomba kukumbusha tena kuhusu ile sauti nilio isikia kuhusu uendeshaji wa chaguzi zetu, nikatoa ushauri huu Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Sitaki kuingia ndani kwenye technicalities zilizopelekea wagombea wa upinzani wote kuenguliwa, bali natoa wito kwa rais Magufuli aingilie kati hali hii au yeye mwenyewe kama rais wa JMT, au kupitia kwa msaidizi wake Waziri Jaffo wa Tamisemi, ayafumbie macho makosa yote madogo madogo ya wagombea wote wa vyama vyote vya upinzani walioenguliwa kwa mizengwe au kwa sababu zozote, ziwe ni za kweli za halali au ni figisu tuu, ayafute na watoe a general amnesty ya jumla kwa kila aliyegombea apitishwe tuu hivyo hivyo despite all the odds ili Tanzania tuingie kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani kwa ushindani wa haki, uwazi na usawa kwa vyama vyote kutendewa haki sawa, kwa demokrasia kuachwa kufuata mkondo wake, hivyo hawa waliosusa wote kwa kuweka mpira kwapani warudi uwanjani kipute kipigwe mechi ichezwe watu washindane.
Ushindi mnene, mnono, mtamu wa raha ni ule ushindi unaotokana na kupatikana kwa ushindani halali wa haki unaopatikana na kuendeshwa kidemokrasia kwenye uwanja ulio sawa, a level playing ground na sio ushindi wa uwanja tenge!, wala sio ushindi wa mezani au ushindi wa bao la mkono!. Ushindi wa dhulma, unabeba a bad karma repercussions, hivyo ukifika muda wa pay back time ya Karma ya dhulma hii, mtashangaa tuu watu wanapukutika, bila kujua sababu kumbe ni karma inakula vichwa!.
Kwa observation yangu, kwa kasi ya rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, kwa haya tuu aliyowafanyia Watanzania kwa miaka hii minne tuu tangu alipoingia madarakani, na mambo anayoendelea kuyafanya kila uchao, ni mambo mkubwa kuliko rais mwingine yoyote aliyewahi kufanya, ukimuondoa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyetupatia uhuru na kutujengea umoja, usawa, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania kama binadamu wote ni sawa kwa kuwa kitu kimoja, Taifa moja lenye umoja, lisilo na ubaguzi wa rangi, udini, ukabila, jinsia na hali, hivyo Rais Magufuli na CCM inakwenda kushinda a clear victory ya ushindi wa kishindo cha wazi wa over 90% kihalali kabisa, hivyo hakuna haja wala sababu yoyote za kutumia figisu figisu zozote, ukiwemo ule utaratibu wa CCM wa ushindi wa bao la mkono kwenye baadhi ya maeneo yenye a strong opposition.
Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, kuhamia Dodoma, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya juu kwa juu, mradi wa umeme wa Stigler's, Tanzania ya viwanda, elimu bure, vituo vya afya, zahanati na mahospitali kila kona, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote huru na wa haki nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote wa vyama vyote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na Uchanguzi wa kidemokrasia huru na wa haki na mshindi apatikane kihalali, ki haki, ki demokrasia kupitia kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi huru na wa haki!.
Nakumbuka wakati naanza kujenga familia nilipokuwa Baba Kijana, nilikuwa nikicheza na watoto wangu michezo mbalimbali kama mashindano ya kukimbia, mnashindana kukimbia, ili kumjengea mtoto ari ya confidence ya kushinda, wewe unakimbia mdogo mdogo ili usimshinde mtoto ukamvunja moyo, unamuacha mtoto akupite na akushinde na akiisha shinda, mtoto anafurahi kweli kweli kuwa amemshinda baba!.
Hivyo tukubali tukatae, kwa hali ya sasa ya siasa za nchi yetu Tanzania kwa hii kasi ya JPM, Magufuli ni game changer wa the political dynamics za siasa za nchi yetu, ambapo rais Magufuli akiendelea kutawala, CCM itakomba kila kata, na kila jimbo!, hivyo ili Tanzania tuendelee kuwa ni nchi ya vyama vingi, kuna maeneo CCM inabidi tuu ijifanye kama baba anayecheza na watoto wake kwa kuwaachia tuu watoto washinde, yakiwemo majimbo uanayogombewa na wenyeviti wa vyama vikuu vya upinzani, majimbo ua Mbowe, Mbatia, Mrema, Zitto, Lipumba, Cheyo etc vinginevyo uchaguz Mkuu wa mwakani, 2020, Tanzania tunarudi kuwa nchi ya chama kimoja!.
Hivyo natoa wito kwa serikali ya CCM, chini ya Jemedari wake, JPM, kiukweli labisa, hata kabla ya uchaguzi, CCM tayari imeishashinda kwa ushindi wa kishindo sio tuu huu Uchanguzi wa Serikali za Mitaa, bali hadi Uchanguzi Mkuu ujao wa mwakani 2020 kutokana na sababu za ki political social dynamics ya siasa zetu, sheria zetu mbovu za uchaguzi, Tume isiyo huru na Shirikishi na uwanja tenge unao i favour CCM,
ukijumlisha na the Magufulification, CCM ni lazima ishinde ushindi wa kishindo, lakini ili CCM iweze kuufurahia ushindi huo, kwa ku enjoy na furaha ya kweli na kuusheherekea ushindi huo kwa raha na furaha, , lazima CCM ishinde kwa ushindani wa kweli, ushindani wa haki na ushindani wa usawa na sio kupata ushindi kwa kufanya figisu ili washindani wako wasuse, watie mpira kwapani na wewe upewe ushindi wa mezani!. Ushindi wa hivi sio ushindi mtamu, wala hauleti raha ya kudumu kwasababu karma itaingilia kati kuja kuikatisha hii raha kwa kula vichwa!.
Nakuomba Rais Magufuli na Waziri Jafo, jifanyeni kama mnacheza na watoto, kwanza wafungulieni njia watoto wote washindane kwa haki, washiriki kwenye uchaguzi huu na wa haki kwa uhuru na kwa haki sawa kwa vyama vyote despite mapungufu walionayo ili hata uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho, wakati Watanzania watakapo irejesha Tanzania kwenye mfumo wa Chama kimoja CCM, iwe ni Watanzania wenyewe ndio wameamua kuichagua CCM kwa haki kupitia uchaguzi huru na wa haki ulioendeshwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi ulioendeshwa kwenye uwanja sawa na tambarare wa ushindani, na sio CCM ishinde katika ule ushindani wa kugombea kisu cha makali kuwili, huku mshindani mmoja ameshika kwenye mpini na mshindani mwingine kwenye makali. Hivyo CCM ishinde kihalali kwa kufuatia kazi nzuri ya rais JPM na serikali yake na sio kwa sababu CCM ndio iliyokamata mpini!
Tena kwa maoni yangu uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaosimamiwa na TAMISEMI ndio uwe wa mwisho kusimamiwa na Tamisemi, tubadili sheria zetu za uchaguzi, uchaguzi zote zisimamiwe na sheria moja, chini ya Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, zuio la mikutano ya siasa liondolewe, wagombea huru waruhusiwe ili hata watu kama akina sisi wenye vyama tujitoe na kusimama as independent candodates tuweze kushiriki kugombea, hivyo uchaguzi wa 2025 tuchague viongozi wa serikali za mtaa, madiwani, wabunge na rais kwa siku moja. Hoja kuwa zitakuwa kura nyingi haina mashiko. Kwenye uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kila mpiga kura anapiga kura 5 kuchagua
Naomba nimalizie kwa ile kauli ya thread hii
"Ushindi Mtamu ni ushindi unaopatikana kwa ushindani wa haki kwenye uchaguzi huru na wa haki, unaaendeshwa na Tume huru na shirikishi ya uchaguzi na unaofanyika kwenye uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa, sio huu uwanja tenge tulionao, na kupata ushindi wa mezani!.
Mheshimiwa Rais, wetu, Dr. John Pombe Magufuli, aka.JPM, kasi yako ya maendeleo ya Tanzania unaoifanya, ina ku guarantee utailetea CCM ushindi safi wa kishindo cha halali katika uchaguzi wowote, tunakuomba sana!, sana!, sana!, "Please! Please! Please!, ruhusu tuu ushindani wa haki, wazi na usawa kwa vyama vyote, kushiriki uchaguzi kwa uhuru na haki sasa kwa wote!, utabarikiwa zaidi na zaidi, na Tanzania tutabarikiwa!, ukiruhusu hizi figisu zinazoendelea, hazina hatima njema kwako, kwa chama chako wala kwa nchi yetu, kwasababu kuna lijamaa fulani linaitwa karma'hilo linataka haki bin haki!, usipotenda haki, lenyewe linaingiliaga kati na halijuagi cha nani wala cha nini!, lenyewe ni haki haki tuu bin haki usipotenda haki!, karma itaingilia kati, na kwa vile no one knows what karma will do, it's better kutenda haki kuiepuka adhabu ya karma !.
Nawatakia Jumapili Njema
Na mimi nawahi kanisani
Misa ya Kwanza pale kanisa langu la St. Peters
Paskali

- Diwani, Shehia
- Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
- Mbunge wa Bunge la JMT
- Rais wa Zanzibar
- Rais wa JMT