Ushauri mzuri sana huu mpaka naona wivu kuwa laiti ningelikuwa mimi ndio nashauriwa!Sasa rasmi wewe ni rafiki yangu , nilikuwa natafuta rafiki mlevi kama mimi ili sasa tuukatae ulevi tuweke misingi .
Njoo sasa Mbeya Carnival tunywe kidogo nitalipa mimi ila tukimaliza tuanze mada ya kuacha pombe tuzipambanie ndoto zetu .
Note , nitakukopa kidogo ili ufike siku ya posho ila usipolipa sitaona shida kuja kukuchamba huku jukwaani , njoo rafiki yangu
Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
😂😂😂 JF bwana!Unataka ushauri wa namna ya kuacha pombe au uchangiwe uendelee kunywa? Au labda ushauri wa namna ya kutengeneza pombe yako mwenyewe ili u save hiyo buku 10 iliyibaki? Funguka
Njoo hapa bar Tbt hiyo ten tuipige supu alafu tutakupa mawazo.
Humu ndani ni burudani sana Kwa kweli- usingizi ukikata lazima nichungulie, labda bando liishe…😂😂😂 JF bwana!
Nenda ukakopeNipe hata kawazo kidogo kuteleza si kuanguka, hapo naamini nimeteleza.
😂😂Unafikiri saizi viwanja vya kumalizia hela Tukuyu hamna? Tena unapukutika dakika kumi nyingi (Kwa mwanaume lakini, nyie si mnapewa tu!). Sasa njoo nikupeleke ila nikopeshe twente kwanza ukija ninavyokupigiaha ruti za viwanja vikali vya kumaliza hela nakurudishia. Ila nilikuwa kyela matema.Tukuyu pesa iishe?
Yaani mitungi wakati unapiga ikikukolea inafurahisha sana ila baada ya hapo kesho yake inaumiza balaa mzee.....Walev tunakutana na changamoto nyng sana,mwenyew jana nimechoma 50 elfu nimeamka na buku 5 tu.yan nimeshinda geto tu hata kutoka sitaman.mitungi ya kingese sn
Kaka unamajanga kama yangu nini kaka!! Funguka maana maandishi yako yanaongea.Ulivyopata hiyo pesa ulikuja kuomba ushauri humu wa namna ya kuitumia?
Mkuu cha teni hakijaisha bado!?Yaani mitungi wakati unapiga ikikukolea inafurahisha sana ila baada ya hapo kesho yake inaumiza balaa mzee.....
Jitathimini.Wasalaam ndugu zangu, aisee ama kweli pombe sio chai.
Juzi Ijumaa katika mazingira yetu ya kazi wakatuzingatia ile posho ambayo tunayoipataga kila ufikapo mwisho wa mwezi, sasa hizi posho zinazaombatana na weekend sio nzuri kabisa ndugu zangu.
Sasa si nikaenda kulewa! Nimeamka Jumaatatu leo asubuhi mfukoni nina 10,000/= tu na sina salio lingine zaidi ya hii teni! Naombeni ushauri wazee, nasavaivu vipi na hii teni mpaka tarehe za mwishoni mwa mwezi ujao? Maana nimewaza mpaka naanza kunyonyoka nywele na kuilaumu mitungi.
Pia ni kwa namna gani nitaacha mitungi. Hapo naombea gesi isiishe geto maana nilivyoamka asubuhi nikajaribu kutingisha mtungi wa gesi ni mwepesi balaa, ila bado haijaisha lakini itakata tu ndani ya wiki hii.
Naanza kuukumbuka ule wimbo wa msondo ngoma, "Kuzaliwa mwanaume kila kitu kwako kitakuwa ni taabu tu!"
Wazee nitafika Septemba tarehe kama hizi kwa balance ya 10,000/= mfukoni? Nikisema nitoe buku nikabeti mpira au tatu mzuka si ndio watapita nayo yote? Au niuze simu?
Mitungi sio, aliyegundua na kuitengeneza mitungi atakuwa hana akili fresh, maana inamaliza hela vibaya, akili inarudi wakati ushapukutika mifuko myeupe.
Pia na hizi kampani za hovyo hovyo za mitungi niachane nazo, maana naweza kufa kwa mawazo. Yaani mimi nabaki na teni wakati leo ndiyo kwanza tarehe 28 August? Sasa tarehe 28 September nitafika kweli? Naombeni ushauri niishi nayo vipi hiyo teni.
Maana wanasema ukikwama shirikisha na wengine, ila mitungi sio wazee.