Chief Kumbyambya
JF-Expert Member
- Jun 16, 2022
- 632
- 2,059
Wasalaam ndugu zangu, aisee ama kweli pombe sio chai.
Juzi Ijumaa katika mazingira yetu ya kazi wakatuzingatia ile posho ambayo tunayoipataga kila ufikapo mwisho wa mwezi, sasa hizi posho zinazaombatana na weekend sio nzuri kabisa ndugu zangu.
Sasa si nikaenda kulewa! Nimeamka Jumaatatu leo asubuhi mfukoni nina 10,000/= tu na sina salio lingine zaidi ya hii teni! Naombeni ushauri wazee, nasavaivu vipi na hii teni mpaka tarehe za mwishoni mwa mwezi ujao? Maana nimewaza mpaka naanza kunyonyoka nywele na kuilaumu mitungi.
Pia ni kwa namna gani nitaacha mitungi. Hapo naombea gesi isiishe geto maana nilivyoamka asubuhi nikajaribu kutingisha mtungi wa gesi ni mwepesi balaa, ila bado haijaisha lakini itakata tu ndani ya wiki hii.
Naanza kuukumbuka ule wimbo wa msondo ngoma, "Kuzaliwa mwanaume kila kitu kwako kitakuwa ni taabu tu!"
Wazee nitafika Septemba tarehe kama hizi kwa balance ya 10,000/= mfukoni? Nikisema nitoe buku nikabeti mpira au tatu mzuka si ndio watapita nayo yote? Au niuze simu?
Mitungi sio, aliyegundua na kuitengeneza mitungi atakuwa hana akili fresh, maana inamaliza hela vibaya, akili inarudi wakati ushapukutika mifuko myeupe.
Pia na hizi kampani za hovyo hovyo za mitungi niachane nazo, maana naweza kufa kwa mawazo. Yaani mimi nabaki na teni wakati leo ndiyo kwanza tarehe 28 August? Sasa tarehe 28 September nitafika kweli? Naombeni ushauri niishi nayo vipi hiyo teni.
Maana wanasema ukikwama shirikisha na wengine, ila mitungi sio wazee.