Ushauri: Dr Ayub Ryoba awe Msemaji Mkuu wa Serikali, Salim Kikeke awe Mkurugenzi Mkuu TBC

kua Rais wa nchi ningemteua Mkurugenzi mkuu wa TBC Dr Ayub Ryoba kumrithi Gerson Msigwa kwenye nafasi ya usemaji mkuu wa serikali na nafasi yake Ryoba ijazwe na aliyekua mtangaji wa shirika la utangazi la Uingereza BBC Salim Kikeke kua Mkurugenzi mkuu wa Shirika la utangazaji Tanzania TBC.

KWANINI DR RYOBA AWE MSEMAJI MKUU WA SERIKALI?
Ninatambua majukumu makubwa ya nafasi ya usemaji wa serikali, maana taifa zima litakuangalia wewe kulisemea kwa mema yote, serikali na miundo yake yote wewe ndiye utakua msemaji wake.

Kwa weledi alionao Dr Ryoba katika sekta ya habari, mabadiliko makubwa ambayo anayafanya TBC ni makubwa na yenye ubunifu wa hali ya juu sana, haina haja ya kuyaorodhesha yote lakini itoshe kusema kwamba nafasi hii inamtosha sana. Ni mzoefu katika sekta ya media, ni mwalimu na mchambuzi mzuri katika sekta hii, anaweza kua chachu kubwa sana katika sekta ya habari. Malalamiko ya kuminywa kwa uhuru wa habari kwa baadhi ya vyombo vya habari anaelewa vyema Dr Ryoba na nu mkweli tofauti na Mwanasiasa Msigwa.

KWANINI SALIM KIKEKE AWE MKURUGENZI MKUU WA TBC?
Pamoja na kwamba bado ni kijana kabisa Salim Kikeke lakini kwa muda ambao amekua kwenye media ana uzoefu mkubwa sana. Salim Kikeke amekua Mwasisi, mtayarishaji na muandaaji wa vipindi vya matangazo ya kiswahili ya kipindi Dira ya Dunia katika ubunifu wa hali ya sana katika shirika kubwa la utangazaji la BBC.

Ninaamini akiwa BBC amepata exposure ya kutosha kabisa ya namna ya uendeshaji wa vyombo vya habari katika teknolojia za kisasa. Akipewa nafasi Kikeke anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana TBC, kinaweza kikawa chombo kikubwa sana ukanda huu wa Afrika mashariki.

Ni wakati wa kijana huyu aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kazi hii ya utangazaji kupewa nafasi hii ili kama taifa tuweze kumfaidi.
Ramli Chonganishi.
 
Dr Ryoba ana uelewa mkubwa wa mambo mbalimbali ya nchi hii, hivyo angetufaa zaidi kwenye usemaji wa serikali hasa kipindi hiki ambacho wananchi hawamuelewi mama kwa sababu tu wamekosa taarifa jinsi maendeleo yanavyoenda.
Kwa Kikeke bado aendelee kulelewa ndani ya utumishi kama azina ya miaka ijayo
 
Dr Ryoba ana uelewa mkubwa wa mambo mbalimbali ya nchi hii, hivyo angetufaa zaidi kwenye usemaji wa serikali hasa kipindi hiki ambacho wananchi hawamuelewi mama kwa sababu tu wamekosa taarifa jinsi maendeleo yanavyoenda.
Kwa Kikeke bado aendelee kulelewa ndani ya utumishi kama azina ya miaka ijayo
Kwahiyo MAMA analeta maendeleo, hayaonekani ila inabidi watu waelezewe ili wayaelewe?
Kwamba Watu hawajui Sukari imetoka 1500 mpaka 4500 kipindi cha mama tunataka mtu aje kutuelezea "huko si kupanda ni kushuka ?"

Kwamba Sementi imetoka 15,000/- mpaka 18500 tunataka Mtu aje kujieleza?
Kwamba hakukuwa na tozo, sasa zimewekwa hata kwenda chooni unalipia tunahitaji mtu aje kutuelezea.?
Kwamba , Ripoti ya Ufisadi CAG hakuna hatua yeyote kwa waliotajawa na kila siku watu wanahamishwa vitengo tofauti na kipindi cha Jiwe walau alikuwa anafukuza wawili watatu , tunahitaji Ryoba aje kutuelimisha?


# Elimu elimu elimu
 
Back
Top Bottom