Usafi wa Mkuu wa Kaya uko wapi?

Naomba niwiwe radhi kwa swali ambalo huwa sipendi kuliuliza na Mwalimu Nyerere alisha tukataza nasikia tu Lugumi ila naomba tu kujulishwa huyu Mheshimiwa ni mtu mwenye asili ya Wapi?
 
CCM wameamua kwa nguvu zote kujifunga kibwebwe cha kutetea Lugumi kwa kila mbinu kulinda chama kisichafuke.
Yani wameona potelea pote hizo mashine hazijafungwa kwenye vituo vya polisi ila hakuna namna ni lazima chama kisitiriwe.
 
Sarakasi za wapinzani kutafuta gia kila wanapofika kwenye kilima. Hivi leo haya ndo yamekuwa ufisadi wa rais kwa vile wapinzani wanataja?

Mbona Lowassa waliyemtaja kwa muda wote wamemkumbatia sasa.
 
Naomba niwiwe radhi kwa swali ambalo huwa sipendi kuliuliza na Mwalimu Nyerere alisha tukataza nasikia tu Lugumi ila naomba tu kujulishwa huyu Mheshimiwa ni mtu mwenye asili ya Wapi?

Ni Msukuma wa Bunda mkuu....mkwe wake na IGP wa enzi za mzee wa msoga...
 
Picha lilianza pale alipoanza kupinga bunge kwenda live wakati yy mwenyewe akiwatumbua watu anakuwa live bila chenga kichekesho cha pili ni pale sakata la lugumi waziri anapokuwa na mgongano wa maslahi na taasisi anayoiongoza wakati anne kilango alitumbuliwa kwa kutokuwa mfuatiliaji wa mambo
Hapo ndio mwenye ufahamu unaona kuwa utumbuaji ni usanii tu na hakuna dhamira ya kweli! Ajabu Watanzania wengi wameingia kingi na huu usanii haoni wala hawasikii!!!
 
Ameshaambiwa... Ukiigusa tu Lugumi na "sisi" tunakuharibia kuhusu ishu yako ya Nyumba za Serikali na MV Dar

Pia wanamstua kuwa "unajua wewe tulikufanyia mpango wa kuwa hapo mjengoni"?

Jamaa akiyasikia tu hayo maneno inabidi awe tu mpole na anyweee tu...
 
Ili la Lugumi mbona kihoja cha mwaka. Tunasubili hao wanaomwona Magu mpasua majipu apusue na hilo la sivyo tuwaone kama wimbo wao..ccm ni ile ile...ccm ni ile ile..

Natuongezee Magufuli ni ccm ile..ile..

Wasitufanyie usanii...
 
Hii ishu ya lugumi enterprises partnership limited liability company linakera sana
NDIO MAANA NASHANGAA RAIS ANAPOSEMA AOMBEWE KWA MUNGU KWANI MUNGU NI MTAKATIFU HACHANGANYWI NA UCHAFU ,VIONGOZI WA DINI KAMA KWELI MNAMTUMIKIA MUNGU ALIYE HAI ACHENI UNAFIKI BALI KUWENI WASEMA KWELI RAIS ANAPOKOSEA TUIGE YA YOHANA MBATIZAJI
 
nilivyoona tu matangazo ya LIVE bungeni yanasitishwa, nikajua tayari kuna majipu yanalindwa. leo nimeamini Kitu LUGUMI na meli mbovu. haa haa....
 
Jana wengi wetu tusiochoka kufuatilia siasa za Tanzania tumeona na kushuhudia kambi rasmi ya upinzani wakizuiliwa kusoma hotuba kivuli ya bajeti wizara ya mambo ya ndani kwa sababu za kuwa na mambo yanayokiuka kanuni na taratibu za bunge.

Najiuliza kama ishu mojawapo ni hili dudu la Lugumi kwa nini inakuwa ngumu kuacha watu wafunguke ili kama serikali ya Magufuli inayopambana na majipu ikapata majipu humo ndani ya Lugumi? au ndo vile tena mkuki kwa nguruwe ila unaorudi kwa boss unakuwa mkali?

Mkuu wa kaya simamia hili ndugu ili tukuelewe upo serious na majipu au kuna baadhi yanakuzidi kimo!
Magu dawa yake ni kivuli chake mwenyewe..Anakiogopa sana japo chamfuata kila sehemu...Ningependa atujibu haya masuala coz anayasikia sana...Lugumi Lugumi Lugumi
 
Back
Top Bottom