Usafi wa Mkuu wa Kaya uko wapi?

Jana wengi wetu tusiochoka kufuatilia siasa za Tanzania tumeona na kushuhudia kambi rasmi ya upinzani wakizuiliwa kusoma hotuba kivuli ya bajeti wizara ya mambo ya ndani kwa sababu za kuwa na mambo yanayokiuka kanuni na taratibu za bunge.

Najiuliza kama ishu mojawapo ni hili dudu la Lugumi kwa nini inakuwa ngumu kuacha watu wafunguke ili kama serikali ya Magufuli inayopambana na majipu ikapata majipu humo ndani ya Lugumi? au ndo vile tena mkuki kwa nguruwe ila unaorudi kwa boss unakuwa mkali?

Mkuu wa kaya simamia hili ndugu ili tukuelewe upo serious na majipu au kuna baadhi yanakuzidi kimo!
Na una BAATI hawajaufuta uzi wako adi saa hii, Magufuli hatajwiiiii!!!!!
 
Uko hakigusa nahama nchi
590820d306ecb5fa9913f77905b3286d.jpg
huku?
 
Picha lilianza pale alipoanza kupinga bunge kwenda live wakati yy mwenyewe akiwatumbua watu anakuwa live bila chenga kichekesho cha pili ni pale sakata la lugumi waziri anapokuwa na mgongano wa maslahi na taasisi anayoiongoza wakati anne kilango alitumbuliwa kwa kutokuwa mfuatiliaji wa mambo
 
Oedipus the king kumbe kweli kile kitabu kinaelezea maisha halisi ya watu . maana kuna kisa mule ndani mfalme Oedipus anatamka laana juu ya watu waliomua mfalume wa zamani kiasi kwamba hajui kwamba yeye ndo anahusika na laana hiyo mwisho wa siku inaonekana yeye ndo mwuaji lakini mfalme alikuwa na busara sana maana alijitoboa macho na kubaki kipofu maana alipewa ujumbe kwamba yeye ndo mhusika wa mauaji na nabii kipofu. nchi inabidi ikubali upinzani uipe macho ili ione hata kama tunawachukia wapinzani.
 
Back
Top Bottom