UpWork Freelancing: Kama wewe ni kijana ambae huna kazi pita hapa

swalii langu ni kuwa mpaka wao wakutafute au na wewe unaweza omba kazi. Kainetics
Unaomba ndugu, kazi zinakuwa posted na bajet husika na maelekzo ya kazi nzima. Unafilter tu kazi za makumpuni ya Africa una apply kwenye hizo. We ile ukiamka asubuhi una apply walau kwenye project kama 25 zilizo filtered hivyo hivi then unaendelea na shughuli zako.
Humo mchana utarudi kwenye account lazima utakuwa walau company moja imekupitisha au kadhaa zimekuuliza vi maswali vya kukupima. Unajibu kawaida na kazi inaanza
 
Hio Translation,Proofreading na Resume Translation zinaenda saawa. Ndizo zinapaswa zitangulie then ongeza nyingine Translation related others. Mambo ya Microsoft PowerPoint, hizo Copy writing na Editing zitoe.
YYYYYY.JPG

HIVIII
 
Unaomba ndugu, kazi zinakuwa posted na bajet husika na maelekzo ya kazi nzima. Unafilter tu kazi za makumpuni ya Africa una apply kwenye hizo. We ile ukiamka asubuhi una apply walau kwenye project kama 25 zilizo filtered hivyo hivi then unaendelea na shughuli zako.
Humo mchana utarudi kwenye account lazima utakuwa walau company moja imekupitisha au kadhaa zimekuuliza vi maswali vya kukupima. Unajibu kawaida na kazi inaanza
THANKS MKUU
 
Kainetics swali lingine mfano umepata kazi kawaida unatakiwa ufanye kwa mda gani. mfano kama nina uwezo wa kuimaliza ndani ya 1hr. Au kuna limit ya masaa unakuta mteja anakupa.
 
Unapaswa uielewa point ya kulipwa kwa saa ndugu.

Kazi ambayo wewe unaona ni nyepesi ivo uifanye ndani ya lisaa, utalipwa kwa hilo lisaa tu. Na mtu uliemzidi experience utakuta analipwa kwa masaa matano au nane ivi. Kama ni project ndefu unaweza fanya hata masaa 18 kwa week.

So kama bei yako ni $5/hr kumbuka UpWork wanachukua asilimia yao unabaki na kana $4 kamili.

Ukipata kazi jitahidi ujivute kidogo yawe walau masaa 2-7 (itadepend na kazi) ila ukijivuta sana unaweza pigwa chini akaoewa anae wahu kidogo.

Hivyo ukipokea kazi ukaona unaweza ipiga in one hour or less, relax uifanye hata kwa 4 hrs. Ili end product iwe vizuri zaidi naulipwe hela inayoeleweka sio kulipwa ya lisaa limoja peke ake.
 
Link Ukijisajili unapata sh 3500 baada ya hapo kila siku utakua ukipata shs 350 ukifikish sh 13000 unatoa hi haina garam ni bure mitandao ya kujisajili ni tigo au voda kumbuka kujisajili ni mara moja kwa mtandao moja ukijisajili mara mbili unafungiw account
 
Hii hela unayotoa kila siku inakuwa inatoka wapi ?
 
Habari wana JamiiForums, kwa bahati mbaya au nzuri, mambo mengi ambayo naandika au natamani kushare humu yashaongelewa tayari , na hata hii kitu ambayo naandika saa hivi. Freelancing.

Though, approach nlioona inatumika na wengi ni tofauti kabisa na ile ambayo nimekuwa nikitumia hivyo naona ni vyema kushare.

Title ya thread nimeandika 'Kama wewe ni kijana ambae huna kazi pita hapa' maana nahisi wengi ambao wanapitia hio kitu wanaweza pata unafuu wakiamua kuipa Freelancing nafasi, kwa kuwa swala la ukosefu wa ajira ni shida ambayo inataka kuzoeleka. Ila hii ni kitu inayoweza fanywa na mtu yeyote yule, as long as uko serious.

Huitaji mtaji wowote isipokuwa skillsets zako, bando, simu na laptop. (Kama ni University underGraduate una advantage kubwa, ila hata kama hujafanikiwa kufika chuo lakini unajikubali kwenye kile unachofanya hii inakuhusu).

Hivyo basi, ndani ya hizi dakika ngapi ntajaribu kuonesha namna sahihi unavyoweza ingiza pesa 'kama mtanzania' kwa kufanya hii freelancing. Walau kuingiza kati ya laki mbili hadi nne kwa mwezi.

Utangulizi
View attachment 2320635

Hio ni screenshot yangu ya Freelancer Profile ya Upwork. Nime censor picha yangu pamoja na Bio, kwa sababu ambazo ntaelezea sio muda. Kwa haraka haraka ukiiangalia utaweza kuona yafuatayo;

Japokuwa picha nime censor, iko potrait,hd na sura inaonekana vizuri.

Pembeni ya Jina langu kuna 'Verified Blue Tick' hii ikimaanisha nimepass mtihani wao.

Inaonesha location yangu ni Dar es Salaam, Tanzania na Muda.

Job Success Rate ni 78%.

Nina $1,000+ in Earnings ( Roughly Million mbili kwa Tsh zetu).

Nimefanya kazi 18 zenye total ya masaa 318.

Kuna hio One liner yangu iayoonesha nadeal na kutengeneza websites na applications, Chini naonekana na charge $7 kwa saa then inafuata description.

Kila kitu nlichoandika hapo juu (mbali na hela niliokwisha ingiza,) kina umuhimu wake kwenye kudetermine success rate yako kwenye kupata kazi na wateja wa kurudi na ntajaribu kuelezea namna utakavyo setup profile yako iwe presentable.

Mambo mengi ambayo ntaongelea kama ushawahi pitia hizi thread nlizoona za freelancing, hayatakuwa sio mageni isipokuwa kitu kimoja ; Badala ya kuchukua tender za wazungu, chukua kazi za makampuni ya kiafrika, yaani East na Southern Africa. Simple.

Kama umesoma kufikia hapa huelewi hata freelancing au hio UpWork ni nini, ngoja niielezee kiufupi;

Freelancing ni nini?

Freelancing ni aina ya biashara ambapo makampuni yanakuajiri kwa masaa kadhaa kuyafanyia kazi fulani. Kazi inaweza kuwa yeyote ile na malipo utalipwa kwa saa.

Hivyo basi, kama umesomea lugha advance na chuo, na uko vizuri kwenye kiswahili na kingereza unaweza kuwa mtafsiri, au kama uko creative kwenye kufanya graphics za aina yoyote ile, au unapenda kuandika kama mimi na unaweza fanya creatve writing, copywriting, proofreading na editing, au uko mtaalamu kwenye web design, au programming, au unajua video editing, kutunga nyimbo, motion graphics , nk unaweza fanya freelancing.

Freelancing unaweza fanya kwa kujiunga kwenye tovuti au apps zinazojishughulisha na hio kitu, kama Freelancer.com, Fiverr na UpWork. Ila hii guide ni kwa UpWork.

Unahitaji Nini Kuwa Freelancer?

Kama utataka kuwa freelancer, kitu cha kwanza utahitaji uwe na uelewa kuhusu kile unachotaka kufanya, yaani uwe Intermidiate au Pro.

Mbili, uwe umekisomea kitu husika na walau uwe una Undergraduate Degree. Kama huna lakini una uhakika uko vizuri kwenye skillset husika, unaweza chukua course inayohusiana na skillset husika mf. Web Design kutoka Udemy yenye cheti na kutumia hicho ili kuchukua test na kuwa verified.

Utabidi uwe na mambo ya msingi kama Picha yako inayoonesha sura vizuri, namba ya simu, anwani na namna ya kupokea malipo(Kama PayPal).

Itabidi uwe na simu, laptop(kama kazi yako ni ya kwenye computer) na bando.

(Sio lazima ila ni mhimu) Ujaribu kutengeneza kijiwebsite cha portfolio kinachoonekana vizuri. Lipa hata Web Designer akutengezee, hii ni sawa na resume au CV yako. Kama hujui Portfolio ni nini, ni tovuti inayoonesha kazi zako bora. Kama unasema wewe ni Video editor, edit video kadhaa uweke kwenye website yako iliyokaa ki video editor kuonesha uko pro na unajua unachokifanya.

Lastly na mhimu kuliko hayo yote; Itabidi ufahamu kujibrand.

Kufanya Freelancing Kwa Akili Kama Mtanzania

Changamoto ambayo wengi wanakutana nayo ni kupata kazi kwenye hizi sites maana wanaofanya hizi mambo ni wengi mno, na wewe ulie anza leo huwezi pewa kazi kirahisi kama kuna mimi ambae nlikutangulia kujiunga.

Pia watu wa ughaibuni huko wanapenda kupewa kipaumbele kwa kuwa grading system za haya makampuni ya Upwork , Freelancer, Fiverr na kadhalia yanapenda kuamini kuwa waliochukia elimu kwao huko wan tendency ya kuwa bora kuliko watu wa huku. Kitu ambacho kina ukweli kwa asilimia kadhaa. Na kama unaenda fanya kazi ambazo ni IT au Programming related, waTanzania hatuna reputation nzuri.

Hivyo, usishindane na wazungu bali exploit marketplace ya waafrika. Baada ya wiki kadhaa au miezi fulani utajishukuru.

Fanya Hivi;

Jiunge kwenye hio Upwork, kwa majina halisi na verify email yako na unga namna yako ya kupokea malipo.

Ukishajiunga Upwork, na ukasetup profile yako, chagua skills zinazoendana na kile unachojua ila ziwe kama 15 tu. Mfano mimi ni Web Designer. Ila naweza Design Apps za Android pia, hivyo nayo ntaichagua pamoja na programming languages ninazofahamu, PhP, Javascript, HTML5 na CSS3. Pia mambo kama UI Design, Debugging na Optimisation yako related na nnayafamu hivyo ntayalist.

Baada ya hapo , kinachofuata ni kuandika Bio yako; ambapo kuna kichwa na maelezo(niliyoficha). Hivi vina play part yake kwenye kudetermine kama watakupa kazi au kukuacha. Ndo maana nikasema kuji brand ni muhimu.

Kujibrand Kwenyewe

Heading

Heading yangu ni simple, ila creative: "I turn crazy ideas into websites, even apps | 5 years experience."

Hio inatosha kumpa idea anaetoa gig mimi ni mtu wa aina gani. Moja, kuweka neno 'crazy' ni kwamba naweza kabiri concept ngumu likija swala la kutengeneza dynamic websites na apps. Na sentence ya pili inasema nina experience ya miaka 5. Hivyo sijaanza jana.

Lastly, ni title yenyewe haiko formal hivyo kuonesha nina personality sio kujaribu ku impress kwa kuweka uongo (Haha, wakati experience yenyewe ni miaka tatu ya kujifundisha mwenyewe lakini hayupo atakae niuliza ).

Hivyo kama labda utakuwa unataka kuwa mtafsiri, au video editor. Weka title ambayo sio rahisi kusomeka formally na pie ikutofautishe na wenzio kwa kukupa ka personality.

Tuseme uko fluent kwenye Kiswahili, Kingereza na Kifaransa na unataka fanya kazi za Translation, tumia title ilotulia kama;

"I can change the voice in my head into three different languages (English, Swahili and Français) | Since I was little :)"

Title ya hivyo inaonesha ujuzi wako, experience na personality yako.

Description

Hii ni mhimu kuiandika kwa kuelezea ni nini unachojua, unakijua toka lini, na ndani ya huo muda umeweza kufanya project zipi na zipi na unalenga wateja wa aina gani.

Link porfolio yako pia. Unaweza pitia bio za wenzio kuona zimeandikwaje, nawe unadike ya kwako ila usi copy na kupaste.

Accolades

Je kitu unachosema unakifanya umekisomea? Kama ndio kwenye ku edit profile yako, chagua chuo uliko graduate na course uliyosomea. Iwe inaendana na kile unachoenda kuwa unafanya. Kwa Web Design, kama umesoma Computer Science inatosha.

Kama hujasomea bali umejifundisha kienyeji, Jichange uchukue course Udemy hata ya $10 yenye cheti, na uifanye. Then tumia hicho cha Udemy.

Lastly, ni kuverify account. Sio lazima, ila ni mhimu. Baadhi ya Freelancing platforms kuchukua mtihani kwenye kile unachosema unakijua watacharge $5 hadi $15, na kwendana na portfolio yako unaweza usiwe charged.

Kwenye kufanya haya yote, jitahidi kutumia laptop.

Sio mpaka ufaulu maswali yote, ila uki weza 65% kupanda utakuwa verified.

Fungua account ya Linked pia, for clarity.

Pricing

Kabla huja decide utakuwa unalipwa dollar ngapi kwa saa, angalia freelancer wengine wanatoa kwa bei gani. Ili usi overcharge.

Kwenye web design nacharge $7/hour. Na sio shida. Kumbuka una lenga ku deal na waAfrika sio wazungu.

Baada ya kumaliza hayo yote, twende kwenye kutafuta hizo kazi.

Kazi Zenyewe

Fact ambazo wengi wanazisahau ni kuwa kwenye Africa yetu hii hii, zipo nchi zinaendelea na zina presence online kama Misri, South , Kenya na Nigeria na baadhi ya makampuni na mashirika huweka kazi zao mtandaoni zifanywe na freelancers.

Freelancer wenye akili, ni wakenya maana wao wanajishulisha na hizi, huku wengi ambao nimekutana nao kwa Tanzania yetu wanajaribu bahati yao kwa project za wazungu. Nlikuwa nafanya hivyo, na probabilty yakupata kazi, ukiwa mtanzania na account mpya ni karibia na 2%.

Hivyo filter project unazosearch ziwe zinalipa below average na zina toka Africa. Chance yako ya kupata kazi utakuwa umeiboost kwa hadi 75% maana bei za wazungu kwa waafrika zinakuwa kubwa hivyo kama unaonekana uko vizuri kwanini wasikupe kazi wewe?

Changamoto na Ya Kuzingatia

Changamoto kubwa utakayokutana nayo ni namna ya kupokea malipo. Jitahidi kupata account ya PayPal unayoweza tumia kupokea hela. Unaweza tafuta line za Safaricom Kenya, etc na kuitumia kuactivate then ukailink na kadi yako ya tz. Au unaweza nicheck kutengenezewa account iliyo complete.

Nyingine ni namna ya kuprove umefanya kazi kwa masaa husika. Jitahidi kazi zako za kwanza uzifanya kwa wepesi ili uwe na Success score kubwa. Ila ukiziwaisha saana utalipwa kidogo, maana point ya kufanya kazi kwa masaa ni unalipwa kwendana na idadi ya masaa ulofanya kazi.

Kama ni kazi kama Transcription, Web Design, ku edit, copywriting au kutranslate maneno na utafanya kwa computer, tumia Screen recorder ku record session zako.

Au piga Screenshot kila baada ya lisaa. Maana waafrika kwenye mambo ya hela mambo mengi.

Mwisho ni jaribu jenga mazingira mazuri ya kupewa kazi za kurudi, ukijenga unaweza ombwa namba na kuanza hata kupewa kazi nje ya UpWork.

Mwisho

Nimefanya kazi 18 kwenye hio UpWork, lakini hizo ni kampuni nne tu. Inamaanisha wananipa kazi za kujirudia. Kampuni mbili za WaKenya (Ipo shule private, na Kampuni ya Insurance) na Moja ya wa South na nyingine ya Nigeria. Mambo kama SEO, Kuwatengenezea apps, directories, learning portals, ad campaigns, etc. So nawe waeza fanya kazi diverse pia.

Wa South na hao waNigeria zipo kazi, wameweza nipa nje ya UpWork. In short nipo kama Tech Support wa tovuti zao endapo kitu kikitokea. Point ni kuwa communicative na ongea vizuri, wata kuconsider, sio kama ilivyo kwa wazungu.

$1k sio nyingi, ningekuwa serious na hizo mambo na kutaka kuifanya fulltime nadhani potential ya kuearn zaidi ipo, sema mambo mengi .

Changamoto ya kupata gig ya kwanza ukiivuka, kupata kazi nyingine itakuwa sio ngumu kivile tena, pambana, give it your whole, na kwa hako ka muda ambako utakuwa ukisubiri kazi, waweza jiajiri nyumbani kwa style hio maana hizi namna nyingine za kuingiza pesa online nazoshare ( humu na huko kwenye blog) wengine wananambia hawana hela ya kuanzia, so kama unahisi unayo masaa matano per day ya kupoteza , fanya freelancing huku unasubiria ajira au kujiajiri.

Nawasilisha.
Kati ya threads ZOOTE ambazo nmewahi kusoma humu ndani kuhusu freelancing, WEWE peke yako ndo umeweza kuidadavua vzr kinaga naga, kinagaubaga pasi ya chembe ya 'utapeli' ndani yake hongera sn mkuu!. Wengine huweka pesa mbele kuliko kuwaelewesha watu kias ambacho thred zao hua hazieleweki. Again, Asante kwa hii post!
 
1. Mkuu kwani mtu akiwa level kama ya diploma akataka kuwa verified inawezekana?

2. Na kama inawezekana, je? Atahitaji vigezo gani na budget kiasi gani kwa ajili ya kufikia vigezo?

3. Kuna umuhimu gani wa mtu kuwa verified tofauti na yule atakayekuwa hayuko verified?
 
Hello, kuwa verified hakuhusiani na elimu ile ya darasani au cheti ulichonacho. Na pia hauombi verification, bali UpWork wenyewe ndo hukutafuta ukifika vigezo fulani.

So, trick ni kufaham vigezo gani wanatumia ili nawe uwe navyo, au upachikiwe;
1. Overall look ya freelance profile yako. Kuanzia kwa picha uloweka kwenye profile yenyewe, skill-sets zako kama zimefuatana na specific au uko too general. Then bei ulojipea kama inaendana na soko au uko chini/juu sana na lastly ni kama portolio yako inaeleweka. Haya yote unaweza yaeka sawa mwenyewe, au kumpea mtu kiasi akurekebishie. Hata mimi.

2. Ukitoka kwenye profile, zinafuata zile Fluency tests Aidha iwe IELET's, DuoLingo au Udemy. Hapa test kuifanya ina range kama $50(Duolingo) hadi $200(IELETS) . Hii ni test normal tu kuonesha unaweza fanya kazi in an English speaking environment. Ukipass kuauzia alama 51% utapewa cheti anbacho utakiunga na profile yako.

3. Ni ufanye kazi kadhaa, na ulipwe.

4. Pata Reviews hata mbili au tatu ivi.

Hayo yote yakifanyika watakucheck wenyewe, wakuambie utume copy ya NIDA. Then utaona uko verified. Sema kua Verified sio lazima. Ukiwa vizuri kwenye hio 1, unaweza pata kazi kawaida tu.
 
1. Mkuu kwani mtu akiwa level kama ya diploma akataka kuwa verified inawezekana?

2. Na kama inawezekana, je? Atahitaji vigezo gani na budget kiasi gani kwa ajili ya kufikia vigezo?

3. Kuna umuhimu gani wa mtu kuwa verified tofauti na yule atakayekuwa hayuko verified?
Kwenye umuhimu, haupo saana mbali na kukupea credibility. Kama kazi inahitaji freelancer mmoja, na wame apply 20 ila mmoja yuko verified. Chances zake za kupata kazi ni kubwa kuliko wale wengine.

Pia inakujengea trust kupata zile kazi za muda mrefu. Kuanzia week 3 kuendelea.

Na kulipwa in advance, kwa kadhi baadhi. Sema yote hayo hata ambaye hayuko verified anaweza kua nayo. Kikubwa ni ulivyo jibrand, na uaminifu wako.
 
Back
Top Bottom