Upotoshaji wa padre kuoa watolewa ufafanuzi

kuna kiapo anaapishwa hivi nitatumia kifaransa:VOUS ÈTES PRETRE A JAMAIS maana yake WE NI PADRI WA MILELE
kwa hiyo upadri upo palepale hiyo nina uhakika na mi nimesomea upadri
kuna kiapo anaapishwa hivi nitatumia kifaransa:VOUS ÈTES PRETRE A JAMAIS maana yake WE NI PADRI WA MILELE

kuna kiapo anaapishwa hivi nitatumia kifaransa:VOUS ÈTES PRETRE A JAMAIS maana yake WE NI PADRI WA MILELE
 
Asante basi tuseme padre mstaafu Kalugendo maana kama Lowasa tunamuita waziri mkuu mstaafu basi na huyu tumuite padre mstaafu tu yatosha.
Msilazimishe ujinga wenu wa siasa ufanane na imani zetu tena zilizotulea
 
Hakuna cha sakramenti wala sakramento,, Askofu Kilaini yupo sahihi kabisa.

Hakuna sehemu kwenye biblia zilipoandikwa sakramenti,, sakramenti ni mapokeo tu ya kanisa. Tatizo ni kutokusoma biblia na kuishia kusoma mapokeo ya kanisa.

Someni neno la Mungu muifahamu kweli, nayo itawaweka huru kweli kweli
.

Ahsante Askofu kwa kufunguka bila kuwaficha waumini wako.
Kumbe na wewe in.mbumbumbu. Hujui. kuwa biblia ni sehemu tu ya mapokeo yaliyo katika maandishi
 
Msilazimishe ujinga wenu wa siasa ufanane na imani zetu tena zilizotulea
Wapi pana siasa au ujinga..?
Je hakuwahi kuwa padere wa RC ??
Je hajafunga ndoa kanisani ?
Je hajafanya tukio la kipekee kufanya na mtu aliyewahi kuwa kasisi??
 
UPOTOSHAJI WA MTANDAO KUWA PADRE AOA WATOLEWA UFAFANUZI

BAADA ya mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari kupotosha kuwa Kanisa Katoliki limemfungisha ndoa padri wake, imefafanuliwa kuwa, Padri akiomba kuondolewa upadri wake anaruhusiwa kuoa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini ameeleza kuwa,katika wito wa Upadri katika Kanisa Katoliki , mapadri hawaoi na hiyo ni sheria ama nidhamu ya Kanisa siyo ya Mungu hivyo Papa ana uwezo wa kuitengua.

“Katika Kanisa Katoliki Padri ni kasisi, ni kuhani anayetolea sadaka altareni. Kutokana na nidhamu ya Kanisa Padri haruhusiwi kuoa lakini pale anaposhindwa kuendelea na wito wake ama anapoonekana kwamba anashindwa kuuishi upadri wake anaruhusiwa kuomba kuacha na anaruhusiwa kulingana na taratibu za Kanisa.

Mapadri ambao mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari vinazungumzia siyo mapadri walishafuata taratibu zote na kupata kibali kutoka kwa Baba Mtakatifu kuwa wamefunguliwa na upadri wao umeondolewa hivyo wana uhuru wa kuoa kwani wamefanywa walei si mapadri.

Padri akishavuliwa upadri haitwi tena Padri wala hawezi kutoa huduma kama padri, ana haki za kuishi ulei wake. Kulingana na taratibu za imani ya Kanisa Katoliki mlei anafunga ndoa aishi na mume ama mke wake kwa uhalali na kuweka maagano yao mbele ya Mungu na hapo hakuna kosa.

Tatizo ni tafsiri ya wanahabari kukuza mambo na kusema padri wa Kanisa Katoliki kaoa wakati alishaondolewa upadri.

Dr Wilbroad Slaa alikuwa Padri wetu tena Katibu Mkuu wa TEC ambaye nilimrithi lakini aliacha upadri kulingana na taratibu za Kanisa akaoa, huyu mwingine Kalugendo naye vilevile alifuata taratibu yupo huru na wako sahihi.

Hakuna aibu Kanisa Katoliki iliyopata wala halijakosea. Tuna taratibu zetu ni mambo tu ya kuelewa,” amesema Askofu Kilaini.

Kwa upande wake Padri Stefano Kaombe aliyefungisha ndoa hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Petro Osterbay amesema kuwa, vyombo vya habari haviko sahihi kusema Padri wa Kanisa Katoliki ameoa kwani Kanisa likishamaliza taratibu zake za kumfanya padri mlei yaani kumuondolea ukasisi wake linamuondolea hadhi yake ya upadri.

“Kuna kuondolewa hadhi ya upadri na kufunguliwa kifungo cha useja. Mtu anaweza kufanywa mlei lakini kifungo cha useja kikabaki au unaweza kufunguliwa vyote.

Bw. Privatus Kalugendo alifunguliwa vyote Septemba 14 mwaka 2008 kwa hati ya Papa yenye Protokali No.4182/08.

Hivyo Bw. Kalugendo alikuwa huru tokea siku hiyo kufunga ndoa kwani hakuwa padri na hakufungwa useja.
Ufafanuzi huu upo vuzuri na asiye elewa ana lake jambo
 
Hakuna kitu kigumu duniani kama kuishi bila kushiriki tendo la ndoa haswa ikiwa reproductive system yako ipo sawa.
 
Hakuna sehemu kwenye biblia zilipoandikwa sakramenti,, sakramenti ni mapokeo tu ya kanisa. Tatizo ni kutokusoma biblia na kuishia kusoma mapokeo ya kanisa.
Biblia ni mapokeo..

Sakramenti zote saba zimewekwa na Yesu peke yake....Labda hujui maana ya Sakrament....
 
Nimempata sawia kabisa ....Kanisa limetukanwa mno na wajanja wajanja wa injili ....sasa hatuwaachi tena wapotoshe ....fact kwa fact tu ....
Kwanza si kweli kwamba Pd Karugendo aliacha upadre kwa hiari yake. Pd Karugendo alishtakiwa vatikani na askofu wake askofu Niwemugizi wa jimbo la Rulenge.

Pia si kweli kwamba Dr Slaa ameshapata ruhusa hii

Kabla yake Pd Karugendo alishasimamishwa kutoa huduma za kanisa tangia 2000. Ruling ya vatikani ilitoka 2008.

Ikumbukwe muda wote huu Karugendo aliendelea kujitambulisha kuwa ni padre.

Utawala wa Kanisa Katoliki kamwe haumpi mnyonge haki. Utawala msonge.

Hapa Tanzania mapd wengi wanateswa na maaskofu wao na hawana pa kukimbilia. Hata balozi wa Baba Mt hawezi ingilia utawala wa ndani wa majimbo.

Kinadharia pd anaruhusiwa kuacha na kufunga ndoa. Kiuhalisia jambo hilo ni gumu na hatua zake ni kama haziwezekani.

Hapa Tz kwa mfano kuna mamia ya maombi lkn yanabaki ktk makabrasha. Hayo maombi yanapelekwa vatikani kupitia kwa askofu husika. Uzoefu ukiandika askofu hapeleki.

Huyu Karugendo alipokwa hadhi yake ya upd kwa hila ndio maana kwa shingo upande wametoa hiyo hati.

Process ya maombi kama hayo huchukua sio chini ya miaka 10 kwa ombi moja.

Kama Yesu alivyoonya viongozi vipofu muwapime kwa matendo yao sio wanachokisema midomoni ili wema wao huonekane kwa watu.

Fanyeni uchunguzi muone ktk majimbo ya Tanzania mapd wa aina ya karugendo wako wangapi.
 
Bahati mbaya sana ya watanzania wanaaminishwa mambo wasiyoyajuwa kwahiyo wanapokea tu kama dodoki.

Kuna kitu sio askofu Kilaini wala pd Kaombe amekisema. Ukishapewa upadre wewe ni padre milele si papa wala nani anayeweza kukuondolea kwa sbb upadre ni sakramenti.

Upadre sawa na ubatizo vinaacha indelible mark kwa muhusika chapa isiyofutika milele. Mf ukishabatizwa halafu ukaingia imani ya kislamu wewe bado ni mkristu kwa sbb ya ile chapa isiyofutika milele.

Kwa sababu hiyo Dr Slaa na Karugendo wote ni bado ni mapd wa kanisa katoliki tena wanaruhusiwa ktk mazingira maalum kutoa huduma za kanisa yakiwemo masakramenti.

Tofauti ya hawa ni kwamba wenyewe wameomba ruhusa inaitwa laicization kumbe kilichoondolewa ni hadhi tu ila sio essence ya upadre wenyewe.

Ni makosa makubwa kufikiri kwamba upadre ni kutokuoa au kutokuoa ni upadre.

Waulizeni tena waliowapa majibu hayo. Nitarudi tena na vifungu vya sheria mjisomee wenyewe
Sasa wewe unajua zaidi kuliko Askofu na padre? Kumbuka wamesema kwamba hiyo siyo sheria ya Mungu Bali ni sheria ya kanisa lao wenyewe, hii sheria waliiweka wao na siyo biblia, kwa hiyo cha mungu ndo kinakuwa cha milele lakini walichokiweka wao wenyewe wanaweza kukiondoa.
 
Back
Top Bottom