Untold Story: Mjue Simon Magus, mchawi tishio kutoka Israel aliyekaribia kuufuta Ukristo Duniani

The only thing inayoweza kumbadili mtu ni neno brother maana ndio kweli pekee tuliyopewa na unajua neno ni Mungu mwenyewe.. Tunapishana hapa neno la Mungu linajitosheleza.

Ila muhimu kwa muamini yoyote wa kristo kusoma biblia na kuielewa.. Mungu ametupa neno tulisome na tuweza kung'amua/kapata ufunuo na humo ndio kuna kuna.. Nje ya hapo yaliyo nje ni vigumi sana mtu kuna kama hili ni sahii au sio sahii
Hapa nimekubaliana tena na wewe, lakini tena sijakubaliana na wewe.

Ulioosema NI VIGUMU SANA MTU KUJUA HILI NI SAHIHI NA HILI SIO, hapo hapana.

Neno la Mungu likiwa moyoni mwako vizuri, UTAWEZA KUNG'AMUA KILICHO SAHIHI NA KISICHO SAHIHI.

Hata vitabu vyangu utajua vinafaa kumjenga mtu au havifai.

Neno la Mungu katika Biblia NDIO KIPIMO PEKEE cha kutenganisha kinachofaa na kisichofaa.

Mfano ukitaka kujua nabii wa uongo na wa kweli, kanisa la kweli na la uongo, mchungaji wa kweli na wa uongo, mafundisho ya kweli na ya uongo, PIMA KWA KUTUMIA BIBLIA.

USISEME NI VIGUMU SANA kana kwamba HATUNA KIPIMO CHA KUTAMBUA.

Ni sawa na daktar ana thermometer afu anasema ni vigumu kutambua mtu aliye na homa na asiye na homa.

Ukiwa na mtazamo huo wa kuona bado mambo ni magumu pamoja na kuwepo Biblia, basi itabidi uishi kimachale sana.
 
Hapa nimekubaliana tena na wewe, lakini tena sijakubaliana na wewe.

Ulioosema NI VIGUMU SANA MTU KUJUA HILI NI SAHIHI NA HILI SIO, hapo hapana.

Neno la Mungu likiwa moyoni mwako vizuri, UTAWEZA KUNG'AMUA KILICHO SAHIHI NA KISICHO SAHIHI.

Hata vitabu vyangu utajua vinafaa kumjenga mtu au havifai.

Neno la Mungu katika Biblia NDIO KIPIMO PEKEE cha kutenganisha kinachofaa na kisichofaa.

Mfano ukitaka kujua nabii wa uongo na wa kweli, kanisa la kweli na la uongo, mchungaji wa kweli na wa uongo, mafundisho ya kweli na ya uongo, PIMA KWA KUTUMIA BIBLIA.

USISEME NI VIGUMU SANA kana kwamba HATUNA KIPIMO CHA KUTAMBUA.

Ni sawa na daktar ana thermometer afu anasema ni vigumu kutambua mtu aliye na homa na asiye na homa.

Ukiwa na mtazamo huo wa kuona bado mambo ni magumu pamoja na kuwepo Biblia, basi itabidi uishi kimachale sana.
Siwezi kuishi kwa machale maana sijiongozi wala mimi sio wangu tena mwenyewe.. Endelea na uandishi kaka
 
Siwezi kuishi kwa machale maana sijiongozi wala mimi sio wangu tena mwenyewe.. Endelea na uandishi kaka
Mimi naona mnapishana na mleta mada sehemu ndogo sana. Vitabu vya historia kuhusu Bibilia vinafaa pia kwa mafundisho. Ndiyo maana hata watumishi wa Mungu wanakwenda vyuo vya Biblia kujifunza mambo mengine ya ziada, ambayo yanasidia katika kuelewa kwa kina yaliyoandikwa kwenye Biblia, ambayo Biblia iliandika kwa ufupi.
 
Miaka ile Yesu anazaliwa, kulikuwa na kijiji kimoja kiitwacho Gitta, kilichopo ndani ya Samaria, hapo hapo nchini Israeli. Katika kijiji hicho, alizaliwa kijana mmoja, ambaye twaweza kusema alikuja kuwa adui hatari zaidi kuwahi kutokea katika historia nzima ya Ukristo.

Tunathubutu kusema kwamba, hakuna mtu aliyewahi kuwa na 'upako' wa kishetani kama yeye, na kufanya miujiza kama yeye, na kubeba nia ya dhati ya kuushambulia Ukristo kama yeye.

Najua unafahamu maadui wabaya na katili walioangamiza mamilioni ya maisha ya Wakristo ulimwenguni, hususani baadhi ya makaisari wa Dola ya Rumi (Roman Empire) katika jitihada zao za kujaribu kuufuta Ukristo duniani.

Lakini kijana huyu wa kijijini asiye na mbele wala nyuma, alitumika na shetani kwa viwango au ufundi wa hali ya juu, HADI KUFANYA WAKRISTO, TENA WALIOKUWA TAYARI KUIFIA IMANI YAO, KUSHINDWA KUENDELEA KUWAAMINI MITUME WA YESU HASA PAULO NA PETRO, NA KUHAMISHIA IMANI YAO KWA KIJANA HUYU.

Mfano, mwujiza wake tu wa kutembea angani hadharani mara kwa mara huku akijiita ndiye Masiha ulitosha kung'oa imani ya baadhi ya Wakristo.

Pamoja na miujiza yake mingi yenye uzani mzito na vishindo vya aina yake, lakini jaribio lake la 'kufa', 'kufufuka' na 'kupaa' kwenda mbinguni lilikuwa linafanikiwa kabisa kuivuruga imani ya Ukristo ambayo msingi wake mkuu ni kifo na ufufuko wa Yesu Kristo wa Nazareti.

Achana na wachawi kama yule 'dagaa' wa Matendo 13:6-12 ambaye pamoja na kujiita Bar-yesu, Paulo alimpiga tu upofu wa siku kadhaa na 'biashara' ikaishia hapo.

Kwa huyu kijana wa Gitta, angepigwa upofu si ajabu angeota macho mengine, na angeongeza mengine mawili awe na macho manne!

Mtume Petro na Paulo, wakiwa wameshikiliwa kwenye kilindi cha ushindani mzito mbele ya Mfalme Nero na maafisa wa ngazi za juu za dola ya Rumi, pamoja na 'mobu' ya maelfu ya watu wa jiji la Roma, walifanikiwa dakika ya mwisho sana kumsambaratisha mchawi yule, pakapatikana ushindi usiomithilika kuanzia ikulu ya Kaisari, mpaka viunga vyote vya jiji la Rumi, na ulimwengu mzima wa wakati ule.

Hata hivyo, ushindi huu ulifungua mlango mwingine wa kisasi kibaya mno, kwani palifuatia mlolongo wa matukio ambayo moja kwa moja yalisababisha vifo vya Mtume Petro na Mtume Paulo, pamoja na Wakristo wengi muhimu pale jijini Roma, Italia.

Makala hii itapitisha jicho lako hatua kwa hatua uone kwa undani kila kilichotokea kwa huyu mchawi, na matukio ya kushangaza yaliyotokea kabla na siku ya mauaji ya Petro na Paulo.

Usiwahi kudhani tu kwamba kwa kuwa Kaisari Nero alikuwa mkatili kama tumjuavyo, aliamka tu siku moja na kuamua kuwaua Petro na Paulo.

Kulikuwa na mlolongo wa matukio (chain of events) yaliyosababishwa na mchawi yule mpaka kumfanya Nero awaue Mitume wale muhimu zaidi kwa Ukristo wakati ule.

Hapa ndipo nilikumbuka na kuzidi kuamini ile nadharia iitwayo 'Butterfly Effect'. Shetani aliitumia kulipepeta Kanisa la Mwanzo kama ngano!

Ngoja kidogo nikufafanulie hii nadharia: Wataalamu husema kwamba mambo ya ulimwengu yameungana na kushikamana kiasi kwamba kitu kimoja kidogo sana kinaweza kusababisha mambo makubwa sana ulimwenguni.

Sasa, nakupa mfano mzuri wa 'Butterfly Effect' ambao hata wewe unaujua maana ulitokea miaka ya juzi hapa, kisha tuendelee na makala yetu.

Tarehe 17 December 2010, katika jiji la Sidi Bouzid nchini Tunisia:

Kijana mmoja maskini, muuza matunda kwenye mkokoteni mitaani, jina lake kamili akiitwa Tarek El-Tayeb Mohamed Bouazizi, mwenye kutokea familia ya 'kihohehahe', alifanya tendo moja la kijasiri lililoishia kubadili mifumo ya kisiasa na kiuchumi ulimwengu mzima na kugeuka kuwa shujaa wa kupigiwa mfano.Kwa kifupi ilikuwa hivi; asubuhi ya tarehe hiyo, aliamka na kuanza kusukuma mkokoteni wake huko mitaani akitafuta wateja wa matunda yake. Kama tujuavyo, watu wafanyao shughuli za namna hii, wakionekana katikati ya jiji basi migambo au polisi 'huwadandia' kama chui anavyorukia swala kutokea juu mtini. Ndivyo ilivyotokea siku hii.

Kijana Tarek alivamiwa na afisa wa manispaa aliyekuja akiwa na wasaidizi kadhaa. Baada ya 'kupigwa tanganyika jeki', kunyang'anywa matunda yake, kupigwa na kudhalilishwa, akaamua kwenda ofisi za meya wa jiji kujaribu kuuona uongozi wa juu ili atoe malalamiko yake.

Baada ya meya kukataa kuonana na kijana Tarek, nadhani akajisemea moyoni: "Watajua hawajui".

Akatoka pale ofisi za jiji, akatumia visarafu vya mtaji wake wa matunda kununulia petroli, akarudi pale ofisi za jiji na kuendelea kupiga makelele akitaka kuonana na uongozi atoe malalamiko yake.Lakini mamlaka za pale ziliendelea kumpuuza hadi akachoka.

Akiwa ameshakusanya 'kiringi' cha watu, akajimwagia petroli ile mwili mzima, akalaani vitendo vya uonevu vinavyofanywa na serikali dhidi ya wananchi, akatangaza kuwa haoni sababu ya kuendelea kuishi ikiwa yupo katika nchi yenye serikali isiyojali wananchi wake.

Watu wakidhani ni mkwara tu, kijana Tarek akajiwasha moto!Tarek aliungua vibaya mno, ambapo siku chache baadaye, tarehe 4 Jan 2011 alifariki wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake.

Taarifa za kitendo kile zilisambaa haraka na kuwagusa wananchi wa Tunisia, 'wakachafukwa,' wakaingia barabarani, mitaa ikachafuka, maandamano nchi nzima, nchi ikapasuka puuuu!! Wananchi walikuwa hawatanii, walikuwa na hasira kali! Baada ya siku kumi pekee toka Tarek afariki, raisi wa Tunisia bwana Zine ben Ali akaachia ikulu akiwa amekaa madarakani kwa muda wa miaka 23! Raisi akajiuzulu hivi hivi ujue!!

Haikuishia hapo, wananchi wa nchi zingine za Kiarabu wakaguswa na mapinduzi yale. Wakajisemea moyoni: "Ahaaaaaa! Kumbe!!" Nao wakaanza vuguvugu. Dunia nzima tukapata lile neno maarafu la 'Arab Spring'.

Tukashuhudia mapinduzi ya kutisha kwenye nchi za kiarabu. Marais wakaona 'cha moto.' Upepo ukabadilika dunia nzima. Ikawa sio nchi za kiarabu tena, nchi zingine zikapokea 'moto' ule hadi 'manchi' makubwa kama China.Maraisi wakang'olewa madarakani, watu wazito kama raisi Muammar Ghaddafi wakauawa! Fikiri, serikali 'nzito' kama ya Libya kuanguka! Nchi kama Misri kiliwaka, kikanuka, moto ukawaka ulimwengu mzima wa Waarabu.Kila mtu duniani aliguswa, na bado tungali tukiguswa na matokeo ya Arab Spring iwe unajua au hujui.

Nataka kukuonesha nini?

Nataka uone tukio dogo mno la afisa mmoja kunyanyasa muuza matunda mtaani lilivyoleta mabadiliko dunia nzima! Huu ni mfano mzuri wa Butterfly Effect. Maana halisi ya hili neno ni kwamba, kale kaupepo kadogo kanakopulizwa na vimabawa vya kipepeo wakati akiruka, tunapaswa kuamini kuwa kanaweza kusababisha kimbunga au dhoruba kubwa yenye maafa, dunia nzima tukatafutana!Ingawa hilo haliwezekani abadani, lakini twapaswa kuamini hilo kwa maana kwamba, kitu kidogo sana kinaweza kuleta 'impact' kubwa hadi dunia nzima ikasimama!

Au, mtu mmoja, hohehahe, asiyedhaniwa anajua chochote, au kuweza chochote, asiyejulikana, anaweza kujikuta akiipigisha magoti dunia nzima!

Sasa, tuanze makala yetu namna hii...

Simoni Magus alizaliwa kijijini Gitta nchini Israeli, akaishi miaka ile ile ambayo Kristo aliishi.

Shetani alianza kumtumia kichawi tangu akiwa mdogo, na alitumika kwa namna ya kipekee kwa lengo la kuja kuumaliza Ukristo kwa staili ya aina yake.

Mpaka Yesu anasulibiwa, anafufuka na kupaa, tayari Simoni Magus alishapata umaarufu na kuogopwa katika Samaria yote.

Alikuwa na uchawi wenye nguvu za kipekee kabisa alizotumia kufanya miujiza ya kuinyamazisha Samaria yote.Bahati nzuri Biblia ikamtaja mahali. Ilikuwa siku moja huyu mchawi Simoni alipookoka!

Tusome hiki kipande kwa makini:

Matendo ya Mitume 8:9-11
9 Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.

10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.

11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.

Kutokana na Maandiko haya, tunapata kujua kwamba Simoni alianza uchawi tangu akiwa mdogo. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa nguvu za kichawi.

Kutokana na ishara na maajabu yake tangu akiwa mdogo, watu wa Samaria wakamwamini na kusema 'mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu'.

Sasa, kuna wakati Mwinjilisti Filipo kutoka Yerusalemu akatembelea Samaria kwa ajili ya kumhubiri Kristo, naye akawa anafanya miujiza.

Mchawi Simoni akahudhuria mkutano, akaona ishara za Filipo, akastaajabu, akaokoka!

Matendo ya Mitume 8:13
Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.

Baraza la wazee jijini Yerusalemu wakasikia kwamba watu wa Samaria, tofauti na walivyotarajia, wamekubali kumpokea Yesu na kubatizwa. Wakamtuma mtume Petro aende Samaria kuwaombea waliookoka wajazwe Roho Mtakatifu.

Kwenye mkutano wa watu kujazwa Roho Mtakatifu, Simoni akahudhuria, akaona watu wakijazwa Roho Mtakatifu.

Akapiga mahesabu moyoni kwamba, akipata Roho Mtakatifu, akajumlisha na uchawi wake, dunia 'itamkoma'! Kwa kuwa alijiweza kifedha alizokuwa akipata kupitia uchawi, akadhani anaweza 'kupiga dili' na Mtume Petro, amwuzie huyo Roho Mtakatifu. Lakini Mtume Petro akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akavumbua 'true colours' za moyo wa Simoni.

Kumbe hakuwa ameokoka, wala hakuwa amezaliwa mara ya pili na kunuia kuacha uchawi wake.

Hebu tusome mwendelezo wa hiyo stori katika kipande hiki cha Maandiko:

Matendo ya Mitume 8:18-24
18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,

19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.

20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.

21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.

22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako.

23 Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu.

24 Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja.


Kufikia hapa, Biblia ikafunga ukurasa, haitaji tena habari za Simoni. Lakini haidhuru, kupitia vyanzo lukuki nje ya Biblia tunapata kuujua ukweli wa jinsi Simoni alivyokuja kuwa mwiba mkali dhidi ya imani ya Ukristo.

Huyu ndiye mpinzani mbaya zaidi kuwahi kutokea aliyeutikisa Ukristo kwa namna ambayo hakujawahi kutokea mpinzani wa aina ile.

Simoni Magus aliendelea kujiimarisha zaidi kwenye shughuli zake za kichawi.

Ilifika wakati akaanza kujulikana eneo lote la Mashariki ya Kati. Akawa mashuhuri na mtu mzito kweli kweli. Uwezo wake wa kupaa angani na kutembea huko juu mbele ya watu mchana kweupe ulimpa jina kubwa hadi Kaisari wa Rumi kumsikia na kumfahamu.

Jamaa alikuwa hatembei kama mimi na wewe. Alikuwa akipaa, na ukisikia kupaa usiwaze 'kokoo' mmoja wa miaka 80 kupaa na ungo usiku wa manane.Simoni alikuwa akipaa na kutembea juu mchana kweupe hadharani.

Kitu kibaya zaidi alichokuwa akifanya ni kusisitiza watu kwamba Kristo Yesu wa Nazareti sio Mwana wa Mungu, bali yeye ndiye mwana wa mungu.

Miujiza kama hiyo ya kutembea hewani na kubadilisha mapepo yake yakawa kama watu halisi ilikuwa ni miujiza iliyozidi kuwafanya watu waanze kupata shaka na Yesu wa Nazareti.

Siku zote na mahali popote alipoenda alikuwa akiwashambulia vikali Mitume Petro na Paulo.

Alisisitiza sana kwamba hao ni wachawi tu, na waongo wasio na lolote.

Kama nilivyosema, Simoni Magus aliendelea kupata umaarufu mkubwa zaidi kiwango ambacho habari zake zikafika barani Ulaya, zikatua nchini Italia, mpaka ndani ya Ikulu ya Roma, kwa Kaisari Nero.

Mkuu huyo wa dunia nzima ya wakati huo, mfalme Nero, akasikia habari zake, na mbaya zaidi akazipenda, na kutuma ujumbe wa kumkaribisha Simoni Magus aende Rumi waonane.Kipindi hiki tayari Ukristo ulishaingia Rumi, ukashamiri kiasi ambacho watu matajiri na mashuhuri pale Rumi, na wenye vyeo walishakubali kumwamini Yesu na kuipokea imani ya Ukristo.

Watu matajiri, maafisa wa ngazi za juu za serikali ya Rumi, pamoja na wananchi wengi walishakubali kuachana na miungu ya Kirumi, na kuupokea Ukristo.

Lakini Mfalme Nero hakuwa ameupenda Ukristo, hasa kutokana na baadhi ya wake zake kuokoka na kuamua kuvunja ndoa naye. Maafisa wengine wa ikulu ya Rumi walikuwa wamekumbana na kadhia hiyo hiyo ya wake zao kuachana nao kwa sababu ya kuepuka ibada za miungu ya Kirumi, na kuambatana na Ukristo.

Maafisa wengine walijiuzulu nafasi zao pale ikulu na baadhi ya watu waliacha kujiunga na jeshi la nchi ili wawe na uhuru mpana wa kuabudu katika imani mpya ya Ukristo huku wanajeshi wengine wakiacha jeshi. Walijua wakiwa katika jeshi, watalazimika kutumikia sanamu za serikali ya Rumi (Roman paganism).

Kutokana na hayo, mfalme Nero akauchukia Ukristo. Akiwa katika hali hii, akasikia jinsi Simon Magus anavyoupinga Ukristo kwa juhudi nyingi.

Akapanga kumkaribisha Rumi. Mchawi Simoni 'alitimba' pale jijini Rumi kwa mkwara wa miujiza 'ya kufa mtu'! Alipofika alimshambulia sana Mtume Petro kwa maneno makali akidai Petro ni mchawi tu na mwongo. Akawa anabadilisha miti kuwa majoka yanayotembea, sanamu za mawe zikawa zinacheka na kutembea, na yeye mwenyewe kutembea angani.

Simoni alipoingia ikulu mbele ya mfalme Nero, akaanza kujigeuza sura na umbile lake na kuwa katika maumbile tofauti-tofauti.

Mfalme Nero kuona hivyo, akaamini kwamba Simoni alikuwa kweli ndiye Mwana wa Mungu.

Wakati huu Mtume Paulo alikuwa ameshaagizwa na Mungu atoke pale Rumi kwenda Hispania kwa huduma, pale Rumi hapakubaki tena mtu 'mzito' kiimani kama kina Petro, Barnaba, Timotheo, wote hawa hawakuwepo.

Ndio maana wakati mtume Paulo anaondoka hapo jijini Rumi, Wakristo wa hapo waliangua kilio wakimtaka Mtume Paulo asiondoke.

Ushindani ulikuwa mzito, na ulichukua muda mrefu Mtume Paulo akiagizwa na Mungu aondoke Rumi aende Hispania, lakini Wakristo wakimzuia.

Hadi siku Wakristo wakiwa sehemu moja waliposikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: "Paulo ameitwa kufanya huduma katika maisha yake, mwacheni aende, atarudi hapa na atatumika chini ya utawala wa Mfalme Nero, mtu yule mbaya na katili, na hata hivyo Paulo atakufa mbele ya macho yenu".

Waliposikia sauti ile walitulia, wakamwacha Mtume Paulo aondoke kwa amani. Mji wa Rumi ukabaki 'yatima' kwa muda wa miaka kumi na tatu! Ndio kipindi hiki mchawi Simoni Magus alitamalaki kwelikweli!

Siku chache tu baada ya Mtume Paulo kuondoka Rumi, Simoni Magus akiwa anaishi sehemu inaitwa Aricia, aliungurumisha miujiza mitaani kiasi kwamba Wakristo wakaanza kudhani huyo ndiye Yesu! Wakristo walipokusanyika makanisani, kulikuwa kukitokea ubishi mkubwa miongoni mwao, wakijiuliza kwamba Simoni Magus ndiye Kristo au la!

Simoni alitenda miujiza mizito kama kufufua wafu, kuponya wagonjwa, na ule wa kutembea angani! Ilifika mahali pabaya mno, kwani Wakristo wote pale Rumi walimwamini Simoni, kasoro watu saba tu, mwanaume mmoja aliyeitwa Narcissus na wanawake sita!

Imagine, watu saba pekee walibaki na imani ya Ukristo! Simoni alifanikiwa kuwachota Wakristo wale, na hii ni kutokana na miujiza ya kutisha aliyokuwa akiifanya.

Lakini sasa, wale wanawake waliobaki, wanne waliamua kujifungia ndani daima, usiku na mchana, wakifunga na kuomba, wakimwomba Mungu amrudishe Mtume Paulo hapo Rumi au amtume Mtume mwingine yeyote ili aje apambane na Simoni Magus.

Mungu akasikia maombi yale, akawa anamwandaa mtume Petro kule Yerusalemu kwa ajili ya kuja kupambana na Simoni na kurudisha imani ya wale wapendwa waliopotea.

Baada ya miaka kumi na mbili, wale wamama wakiomba, ndipo Mtume Petro alitokewa na Yesu na akaamriwa haraka sana, bila kujiandaa, aondoke Yerusalemu, aende Kaisaria, atakuta meli inayoenda moja kwa moja Italia, apakie humo, akapambane na Simoni Magus.

Mtume Petro aliaga Wakristo wa Yerusalemu siku ile ile, akaanza mbio za kuwahi meli ile, akaingia, akaanza safari ya siku nyingi baharini.

Hakuwa amejiandaa, na mbaya zaidi hakuwa amebeba chakula na mahitaji mengine muhimu ya safari.

Safari ya Mtume Petro iliishaje?

Alipofika Rumi ni nini kilitokea hasa alipokutana na Simon Magus uso kwa uso?

Usiache kabisa kusoma upate kujua 'mshike-mshike' uliotokea pale Rumi, mji mzima ukasimama kwa miezi kadhaa Mtume Petro akishindana na Mchawi Simoni, hadi siku ile alipomporomosha akaanguka kutoka angani na kufa kifo cha aibu.

Lakini utaona kwa undani jinsi Mfalme Nero alivyokasirika mchawi wake kufa, akaishia kuwaua Mtume Petro na Paulo, matukio ambayo tumeyaeleza kwa kina yalivyotokea.

Hii ni moja ya makala zinazopatikana katika vitabu vyetu viwili ambavyo vyote unavipata kwa shilingi 20,000 pekee.

Wasiliana nasi kwa namba hii 0762 731869 useme unataka soft copy au hard copy.

Kwa muhtasari tu, ni kwamba, katika vitabu hivyo, utakutana pia na zile nyaraka zilizogundulika pale Uturuki zenye maelezo aliyoyatoa Mariamu mama yake Yesu, ambapo kupitia maelezo hayo utamfahamu Yesu kiundani tangu utoto wake, maisha yake ya kawaida na tabia zake akiwa nyumbani, na alichokuwa akifanya pale nyumbani hasa kukitokea ugomvi, lakini pia utaijua tabia ya ajabu aliyokuwa nayo Yesu kwenye kula kwake na kuvaa kwake. Maelezo hayo hayakuandikwa kwenye Biblia, ingawa ni mazuri sana kujifunza kumhusu Yesu.

Utamwona Mariamu mama yake Yesu alivyokuwa akiudhika kwa vile Yesu alivyokuwa hahangaiki kutafuta mke, utajiri, umaarufu, wala kujijenga kisiasa, wakati huo akidhani Yesu angekuwa mfalme wa siasa za kidunia.

Utamwona pia Martha dada yake Lazaro alivyokiri kutamani kuwa mke wa Yesu, lakini utafahamu jinsi Yesu alivyokuwa akiishi dhidi ya wadada, hadi watoto wadogo wa kike.

Lakini habari za Yohana Mbatizaji ambazo Biblia haikuandika hazijaachwa. Utajua Yohana aliweza vipi kuishi ndani ya jangwa lile hatari la Yudea, tena tangu akiwa mtoto mdogo? Alifikishwaje katikati ya milima ile hatari? Majibu yote yapo na utaona jinsi malaika walivyomlea Yohana tangu utotoni pale nyikani.

Hivi unajua kuwa wale watesi wa Yesu kina Kuhani Mkuu Kayafa na Pontio Pilato walikuja kusurrender na kuukubali Ukristo? Soma upate visa hivi vya ajabu kabisa uone walichokutana nacho hadi mtu mzito kama Kayafa kuamua kujiuzulu mamlaka nyeti ya Ukuhani Mkuu na kuupokea Ukristo. Usiache kujua kilichotokea siku Yesu alipomtokea Kayafa akiwa amejificha ndani kwake. Ni katika visa hivi pia utakutana tukio zima la Yesu kufufuka likielezwa kwa urefu na wale maaskari waliolinda kaburi, utaona maajabu ambayo Biblia haikueleza.


Wajue kiundani majitu hatari makubwa yaitwayo Wanefili waliotajwa kwa ufupi kwenye kitabu cha Mwanzo sura ya sita. Fahamu walikotoka, fahamu walivyokuwa wakubwa na jinsi walivyoitesa dunia hadi kusababisha Mungu kuamua kuifuta dunia kwa yale mafuriko enzi za Nuhu na kuanza upya uumbaji wake.

Lakini pia tumehakikisha tunakuandikia ule ushuhuda wote maarufu duniani wa mchungaji Bernard wa Ghana na sasa unaweza kuona maisha ya mtu aliyepitia majanga ya kipekee tangu kuzaliwa na kahaba, kuishi majalalani, kuumwa hadi mahututi, kuokoka, kwenda Ulaya, kualikwa mara tatu na rais wa Marekani na utagundua kwamba ni dhambi kubwa sana kudhani kwamba wewe una matatizo magumu sana ambayo Mungu hawezi tena kuyatatua.

Hatukuacha pia kukueleza kwa undani kuhusu lile sanduku la Agano la Bwana tangu kutengenezwa kwake, miujiza yake na maajabu yaliyotokea siku ile sanduku lilipopotea.

Kwa shilingi elfu 20 utapata vitabu vyote viwili.
Chanzo cha taarifa zenu ambazo hazijaandikwa kwenye Biblia ni kipi?
Je, Mapiramidi ya Misri yalijengwaje, na akina nani?
 
Chanzo cha taarifa zenu ambazo hazijaandikwa kwenye Biblia ni kipi?
Je, Mapiramidi ya Misri yalijengwaje, na akina nani?
Hili nalo ni swali zuri kabisa. Ingekuwa ajabu sana kama katika vitabu hivyo tusingesema ni wapi tumepata mambo hayo.

Professionally, mwandishi anapaswa kuonesha ni wapi kapata anachoandika.

Unapoonesha sehemu ulizopata unachoandika ndivyo contents zako zinakuwa na authority kwenye mioyo ya wasomaji.

Ndio maana katika vitabu hivyo, tumeeleza wazi kabisa tunakopata habari hizo.

Kasoro zile habari ambazo zipo kila mahali, hizo huwa mara nyingi hatuna haja ya kuandika tulikotoa maana hata msomaji anakuwa anajua zilikotoka.
 
Back
Top Bottom