Unazikumbuka hizi movies? Ulikuwa wapi?

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,536
23,985
1. BABY'S DAY OUT
8f7a972a936acfc309d238023d17911f.png

Mabwana watatu wanaojifanya wapiga picha wanamteka mtoto mdogo wa miezi tisa toka familia ya kitajiri kwa lengo la kutengeneza pesa ya maana kutoka kwa wazazi wake.

Bahati mbaya mtoto anakuja kuwatoroka na kuzamia ndani ya jiji la Chicago. Sasa mabwana hawa watatu wanabakiwa na shughuli pevu ya kumtafuta mtoto huyu anayetambaa katikati ya jiji kubwa kabla hajapatikana na wazazi wake.
74c8048dd40f3430c98b198016a3cf32.png

Sasa huo msako wake sio poa. Ni mateso na mahangaiko.

2. HOME ALONE
596dabb4d20e99d3167f00ede73b28fe.png

Kelvin ni mtoto kwenye familia kubwa ya McAllister, lakini pamoja na ukubwa wa familia yao, Kelvin anahisi familia yake haimjali.

Bahati mbaya kwenye safari ya familia, Kelvin anasahaulika na hatimaye anabaki nyumbani mwenyewe (home alone). Mwanzoni anajihisi furaha kuwa peke yake lakini muda si mrefu furaha inageuka kuwa mapambano pale anapobaini kuna wezi wanataka kuvunja na kuiba humu ndani.
287f10de9e513258a2735c90bb6db3cb.png

Sasa yampasa apambane nao peke yake akiwa na faida ya kwamba yeye anaifahamu nyumba hii kuliko wezi hawa.

3. THE MASK
bf87f87cd6e2794cf9efe49b34b44bec.png

Stanley ni kijana mwema na mwenye haya ambaye anafanya kazi ya ukarani benki. Shida yake ni kwamba hana bahati kwenye mapenzi na sababu ya upole wake basi anaonewa na karibia kila mtu anayemzunguka. Rafiki wa karibu alonaye ni mbwa wake.

Lakini maisha haya yanakuja kugeuka pale anapookota kinyago cha ajabu karibia na bahari. Anapovaa kinyago hicho anakuwa mtu mwenye haiba tofauti na pia mwenye nguvu za ajabu!
0c6fbeb8de8aa9d2cd565ad76341057d.png

Anaweza akaongea na yoyote na anaweza akafanya chochote.

Ila anakuja kuingia matatani baada ya kuiba pesa benki na kisha kesi hiyo kutupiwa kwa genge la wahuni ambalo sasa linalazimika kumuwinda Stanley na kinyago chake.

4. DEAD OR ALIVE (DOA)
0fc15fce5e2b9a9574d25c59a5918e50.png

Kufika kwenye hiki kisiwa ambacho kinalindwa na ulinzi mkali, ni mpaka upewe na mwaliko tu. Ndani ya kisiwa hiki kunafanyika shindano kali ambalo linawakutanisha wapambanaji wenye uwezo mkubwa toka pande zote nane za dunia.

Na humu ndani kanuni ni moja tu, mnapambana mpaka abakie mtu mmoja atakayetoka hai na donge nono la pesa - dola milioni kumi.
d1241444c8bce61a4200e4841a1a4d93.png

Sasa wapambanaji wanne wanaoingia humu kisiwani wanaungana na kuanzisha ajenda yao ya siri. Lengo lao ni kupambana na wanaoendesha hili pambano ili kubaini siri wanayoificha.

5. RUSH HOUR
d7435ecc6021c46d173c733c008f09f6.png

Han ni mwanadiplomasia wa China nchini Marekani ambaye anampoteza binti yake baada ya kutekwa na genge la wahuni linaloongozwa na mchina bwana Sang.

Kwasababu hii, Han anamwalika polisi kutoka China (Mr. Lee) ili aje kumsaidia huku Marekani kwasababu anamfahamu vema Sang na genge lake.

Lakini shida inakuja, FBI hawataki kufanya kazi na Lee maana inaweza ikaharibu mahusiano baina ya mataifa haya mawili endapo likitokea la kutokea.

Kwahiyo wanamtelekeza mwana kwenye kitengo cha polisi cha Los Angeles (LAPD) na hapo anakabidhiwa kwa mpelelezi 'nigga' James Carter kwaajili ya uangalizi, hii ikiwa ni adhabu kwa mpelelezi huyu kwasababu aliharibu moja ya misheni alopewa.

Sasa mabwana hawa wawili ambao wametengwa na vitengo wanajikuta wanaungana kumsaka mtoto alotekwa, tena nje ya mfumo maalum wa usalama.

6. FRIDAY
02ff063995c5f0fad4fa6086d94a4a7e.png

Ni siku moja tu, Ijumaa, lakini Craig ana kazi kubwa ya kufanya kabla siku hii haijaisha.

Moja, kabla ya kufika saa nne ya usiku, inabidi awe amemsaidia rafiki yake Smokey ambaye anadaiwa dola mia mbili ya bangi kutoka kwa mtemi bwana BIGI. Huyu bwana hana utani.

Pili, inabidi awe amepata kazi maana nyumbani kwa wazazi hapakaliki, anataka kutimuliwa.
Na tatu, atemane na mwanamke anayemganda maana kuna pisi kali anaifukuzia.

Yote haya inabidi yatokee katika mtaa wao ambao haushiwi na matukio. Huku bunduki, mafumanizi na ubabe.
Atatoboa?
c004d2f54e28e9bbe75a25eaf29b7f47.png


7. BLOOD DIAMOND
e32027c7e84c3af3133b9cf97ff12d79.png

Katika nchi ya Sierra Leone ambayo imegawanyika vipande viwili kwasababu ya vita kali baina ya serikali na makundi ya waasi, ndipo matukio haya yanapotokea.

Bwana Solomon, ambaye ni baba, amepoteza kila kitu na anatafuta namna yoyote kuirejesha tena familia yake. Moja mtoto wake wa kiume ametekwa na waasi na kugeuzwa mtambo wa mauaji. Na pili mkewe na watoto wake wengine wawili wapo katika kambi ya wakimbizi.

Katika haja hii ya kuikomboa familia yake, akiwa anafanya kazi kama mtumwa katika mgodi wa waasi, anaamua kuificha almasi aliyoipata akiamini hii ndo' itakuwa tiketi yake.

Lakini bahati mbaya, bwana muasi (captain poison) anagundua janja yake na anamtaka aikabidhi almasi haraka iwezekanavyo kabla hajammwaga ubongo.
05dba8d5c5bc03e3626153e4dac1f41c.png

Mara kidogo wanajeshi wa serikali wanavamia eneo hili na kusababisha vurugu. Samson anaifukia almasi yake haraka kabla hawajakamatwa na kutupiwa rumande.

Huko sasa ndo anakutana na jamaa mzungu (Danny) mwenye njaa kali ya mawe ambaye baada ya kusikia kwamba jamaa ana jiwe, anafanya namna kumtoa ndani na anamuahidi atamsaidia kuikomboa familia yake endapo watashirikiana kulipata lile jiwe alilofukia.

Hapo sasa ndo' utajua kwanini ile almasi iliitwa 'blood diamond'.

Katikati ya vita, msako unaanza.
cb63ef2785f09b6b74234f3ba8e6dcd6.png


8. KILL BILL
691a1376dbde8b495d86e90a5e4a08fc.png

Baada ya kuishi miaka minne mfululizo akiwa hana fahamu tangu aliponusurika kuuawa na mpenzi wake katika siku ya harusi, hatimaye mwanamke (the bride) anaamka tena.

Anagundua mimba alokuwa nayo haipo tena na wale watu walokuwa karibu naye wote wamepotea wakiongozwa na aliyekuwa mwanaume wake, bwana Bill.

Sasa anaamua kurudi katika haiba yake ya zamani ya kuwa muuaji (an assassin) na lengo lake ni kuwatokomeza watu wote waliohusika kwenye kuharibika kwa mimba yake, kuharibika kwa harusi yake na kumpotezea muda wake wa miaka minne.
450f92767fe3e132baeea99d643c768b.png

Safari hii ya damu inapeleka vifo vya watu mamia.

Na The bride hajali mpaka pale Bill, chanzo cha yote, atakapopatikana.

BONUS:

Na vipi, unamkumbuka Mark Dacascos wa kwenye DRIVE na BLOODMOON?

3325d29c1486f15b9a170810e0e1f9e7.png
Je Antonio Banderas wa THE MASK OF ZORRO na ONCE UPON A TIME IN MEXICO?

da2523a61a7c1f8940f4fc631417fc1b.png
Inabidi uwe umeoa sasa na una watoto watatu.
 
Movies zote nimekuwekea pale mjini Telegram, search UZI MKALI utazipata utakavyo. Enjoy.
 
Baby's day out 1998 nilikuwa na miaka 4 ndio nakumbuka niliangalia sina kumbukumbu nyuma ya hapo asante kwa kumbukumbu ngoja niitafute niangalie na watoto wangu
 
Dah, umenikumbusha mbali sana wakati huo TV moja kijiji kizima. Kuna mzee mmoja alitoka kusoma South Africa ndio alikuja nayo tukawa tunaangalia kwake kwa kuchungulia Dirishani.
 
Dah, umenikumbusha mbali sana wakati huo TV moja kijiji kizima. Kuna mzee mmoja alitoka kusoma South Africa ndio alikuja nayo tukawa tunaangalia kwake kwa kuchungulia Dirishani.
Baby's Day Out kipindi hiko ilifanya nikamwagiwa maji dirishani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom