Unatambua kwanini mwanamke aliesalitiwa anasamehe na mwanaume dont?

Kwa asilimia kubwa ya wanaume yale ni maeneo yake ya kujidai ambayo mwanaume mwingine yoyote hana ruhusa ya kuingia. Na inapotokea mwanaume mwingine kapita basi hakuna cha msalie mtume ni mahusiano au ndoa kufa japo wako asilimia ndogo sana ya wanaume ambao labda wanaweza kusamehe. Inawezekana pia wanaume tulio wengi hatuwezi kusamehe kitu kama hicho kinapotokea ukilinganisha na wanawake pamoja na baadhi kuwa na moyo wa kusamehe lakini si kusamehe hili tendo la njemba nyingine kujidai kwenye utamu.
Ni kweli...ila maumivu ya kusalitiwa ni sawa kwa wote regadless ni mwanaume au mwanamke
 
Wanawake tuna moyo wa kusamehe sanaa! Ila mwanaume akisalitiwa jamani yaani dunia nzima inaweza jua jinsi wanavyoumia na ndiyo wanavunja mahusiano papo hapo
Na % kubwa huwa wanasusia na mapenzi kabisa!!! Teh teh teeeeeh, mkuki kwa nguruwe.
 
Mwanamke akichepuka halaf ukamsamehe inakuwa ni sawa na paka aliyeingia jikoni akaiba mboga halaf ukamuacha tu.

Ataendelea na hiyo tabia ndio maana mwanamke akichepuka hamna jingine zaidi ya kumuacha
 
Ni Hivi, namna ambavyo mwanamke na mwanaume tunatazama vitu ni tofauti sana. Ndio Maana tukija kwenye suala la michepuko Hali inakuwa tofauti.
Mwanaume ameumbwa kumiliki, na milki yake ina mipaka fulani endapo mipaka hiyo ikivamiwa huwa na kawaida ya kupambana ilikuokoa. Ikitokea kashindwa repercussion yake ndo huamua kuachana kabisa na hizo mambo kama njia ya kujinusuru na hilo.

Hali huwa tofauti kwa wanawake wao hawana karama ya kumiliki ndio hapo tu tunapotofautiana. Kwa kutokuwa na karama hii ndio maana huwa ni rahisi kwa mwanamke kukubaliana na Hali yoyote ile, hasa katika suala mahusiano.

Men look for respect in every thing they do.
But women look for affection, it depend on how thing makes her feel about.
If it doesn't feel alright she tend to get rid of it.
 
Wanawake design wana kitu special moyon kinachowafanya wasamehe na kusahau haraka yaliyotokea BUT most of us ME da ukijua KE amekusaliti hata kama sio mke just a girlfriend tu ambaye hata kwao bado hawakujui siku hiyo hiyo inakuwa mwisho, wapo wanaosamehe ila ni wachache
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom