Unataka urafiki wenu uendelee kudumu? Basi usijenge nyumba jirani na yule "best friend" yako

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,892
16,406
Good afternoon JamiiForums.

Je, unataka urafiki wenu uendelee kudumu miaka na miaka? Basi usijenge nyumba jirani na yule "best friend" yako. Usifikiri mkijenga majirani ndio mtadumisha urafiki wenu mkuu. Hapana kwa sababu kuu moja kwamba, wewe na yeye mnaweza kuwa "best friends" lakini wake zenu wasiwe mtu na shoga yake. Umenipata mkuu? Umenisoma mzee baba?

Hii imekaa hivi, Pipa na Mfuniko ni marafiki wa muda mrefu sana. Walikutana kazini au zamani walikuwa wanakaa mtaa mmoja na kucheza wote ile michezo ya kitoto. Kuna uwezekano mkubwa pia hata labda Pipa na Mfuniko walikutana chuoni UDSM wakitokea shule tofauti za secondary, lakini walipokuwa chuo walikuwa wanafanya mambo yao kwa pamoja mpaka wakawa marafiki.

Inawezekana walikuwa kozi moja, walikuwa discussions group moja, walikuwa wanakunywa beer wote siku za weekend na kufukuzia pisi kali za chuo. In sort itoshe kusema kwamba, Pipa na Mfuniko ni marafiki wa kufa na kuzikana.

Punde baada ya kuhitimu elimu ya juu mwaka 2013 walikula msoto mwaka mmoja na hatimaye kupata kazi kampuni tofauti Dar lakini bado wakawa wana-hangout pamoja.

Kosa ambalo huyu Pipa na rafiki yake mfuniko wanaweza kulifanya likaja kuua urafiki wao ni pale ambapo wataamua wote kwenda kununua kiwanja sehemu moja. Hahahahaaa, that's a fatal mistake my friend. Usinunue kiwanja kisha ukajenga na kuishi jirani na rafiki yako mkuu kwa maana nyie mnaweza mkawa maswahiba lakini wake zenu wasishibane.

Kama pipa amenunua kiwanja Boko, basi mfuniko ajitahidi aende akanunue huuuuuko Kibamba ili kuongeza ladha ya urafiki. Kama mnakaa Arusha, wewe ukipanga nyumba Njiro, basi rafiki yako yeye akakae Sakina. Msikae karibu kama kweli mnataka urafiki wenu uendelee kudumu.

Kuna kitu kimoja ambacho kimejificha katika urafiki nahisi watu wengi hawakifahamu. Urafiki ni mtamu kama mnaonana mara moja moja. Hii ndio siri kubwa na urafiki mtamu. Ukikaa muda mrefu haujaonana na mtu ndio mnakuwa na mambo mengi ya kusimuliana, na hapa ndio utasikia "aisee, Pipa alikuja kikazi Dar akitokea Mwanza, tulipiga story mpakaa saa saba usiku". Kwanini wapige story mpaka usiku wa manane? Sababu ni moja tu, hawajaonana muda mrefu.

Urafiki wa kuonana kila wakati wa kuwa majirani ipo siku wake au watoto zenu watawagombanisha. Mdogo wake uliyeanza kazi juzi juzi tu hapa, hivi unawajua wanawake au unawasikia? Hivi unafikiri wahenga waliposema kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzio waliokosea? Wewe (Pipa) unaweza ukanunua sofa mpya lakini rafiki yako (Mfuniko) hajabadili viti mwaka wa tano sasa.

Unafikiri kinachofuata ni nini kama sio shemeji yako (mke wa Mfuniko) kumnunia mkeo? Mama watoto wako amepika vizuri siku ya X-mass, lakini kwa best yako pamedorora, ni nini kitafuata hapa kama sio beef?

Wake zetu tunawapenda sana, lakini wao kwa wao wasipoiva chungu kimoja sidhani kama mtu na best yake wataendelea kuchekeana kama zamani, tena mbaya zaidi ukute mke wa mfuniko anafanya kazi Bank lakini yule wa Pipa yeye ni mama wa nyumbani, mbona urafiki huo wa tangia utotoni/chuoni utaingia doa.

Kama unataka urafiki wenu uendelee kudumu muda mrefu, usijiroge ukajenga eneo moja na best friend yako, ooooho sasa wewe jifanye mjuaji, kuna siku utaukumbusha huu ushauri wangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mkuu kwa maoni yangu mimi ni kuwa...

Hii itakuwa ni mbaya endapo tu nyie marafiki mtalazimsha wake zenu wawe marafiki kama nyie.

Hapo ndo itakuwa mbaya.

Lakini ikiwa hamfosi na kulazimisha wake zenu wawe marafiki basi mnaishi vizuri tu huku mkiendelea na urafiki wenu.

Kitendo cha kuwalazimisha hao wake zenu wawe marafiki hiko ndo kinaweza keta shida kwa sababu kila mke atakuwa na hulka zake,mbali na hapo haiwezi kulwta shida.

Kwa sababu wapo watu ambao huishi kama majirani na baadae huangukia kwenye urafiki kabisa wake kwa waume zao.

Jii maana yake ni kuwa acha hao wake wazoeane wenyewe kwa wenyewe kama wanaendana tabia watakuwa marafiki na kama hawaendani watabaki kufanyiana ubinadamu wa kawaida tu.

Sidhani kama kwangu ni sahihi kukata kauli ya moja kwa moja katika suala hili
 
Mkuu, mimi na wewe kama ni marafiki na tupo chini ya mjumbe mmoja wa nyumba 10, basi automatically wake zenu watakuwa marafiki au maadui.
 
ilo nalo nineno la maana kbs mtu wang
 
Mkuu, mimi na wewe kama ni marafiki na tupo chini ya mjumbe mmoja wa nyumba 10, basi automatically wake zenu watakuwa marafiki au maadui.
Sio kweli kama utalszimisha hii iwe kwa jumla.

Lakini itakuwa kweli endapo utasema kwa baadhi.

Ninao ushahidi wa wazi wa watu ambao ni marafiki lakini wake zao wanaishi kama majirani wa kawaida.

Nyie marafiko mkijielewa na kujua mipaka yenu hapo hakuna kitakachoharibika.

Mkianza kuingiza na kusikiliza maneno ya watu pia inakuwa shida nayo.
 
Back
Top Bottom