Ulaji wa Nguruwe wapigwa Marufuku

4a0b372cb09f5d228ccbb78c6400bf63.jpg
 
Watu hata waambiwe mkila mtakufa bado hawatasikia mpaka wafe....chezea KITIFIRE.
Homa ya nguruwe haiambukizi binadamu wala haiui mtu kamwe. Madhara ya homa ya nguruwe ni ya kiuchumi full stop. Unaambukiza na kuua nguruwe kwa haraka na kwa wingi. Hayo ndio madhara ya homa ya nguruwe (African swine fever). Kwa hiyo ukila mnyama mwenye ugonjwa huwezi kuugua wala kufa. Lakini hata hivyo kuruhusu uuzaji wa nguruwe wenye homa unapaswa kudhibitiwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa. Acheni kusikiliza wanasiasa wanapoelezea masuala ya kitaalam badala ya kuwaachia wataalam waeleze
 
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme, amepiga marufuku uingizaji na uchinjaji wa nguruwe, kufuatia mlipuko wa homa ya nguruwe.

Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na madiwani na watendaji wa Manispaa ya Dodoma.

Alisema hadi sasa zaidi ya nguruwe 200 tayari wameshakufa kutokana na mlipuko huo.

Aliwataka wakazi wa manispaa hiyo kutokula mizoga ya nguruwe ili kuepuka maambukizi ya homa ya nguruwe ambayo kwa asilimia 100 inaua.

Aliwataka kula nyama ya nguruwe iliyopimwa na wataalamu wa afya.

Alisisitiza madiwani kutoa elimu kwa usahihi kwa wananchi wao kuhusu madhara ya mlipuko huo.

Alitaja kata zilizokumbwa na mlipuko huo kuwa ni kata ya Ipagala na Miyuji ambayo zaidi ya nguruwe 200 wameshakufa.

Aliagiza kufanyika doria na kuwakamata watu wote watakaobainika kukaidi amri hiyo.

“Ninawaagiza nyinyi madiwani pamoja na watendaji hakikisheni mnatoa elimu iliyo sahihi kwa uwazi bila kificho, ukizingatia kuwa ugonjwa huu unaua tena kwa asilimia mia moja, hivyo ni marufuku kuingiza ndani ya wilaya hii na wala kuchinja pasiporuhusiwa na wataalamu wa afya,” alisema.

Alisema ingawa ufugaji wa nguruwe ni sehemu ya kujiingizia kipato, kipindi hiki cha mlipuko hakuna sababu ya kupuuza bali wanatakiwa kujiepusha ulaji holela wa nyama hiyo.

Aliwataka wafugaji kujiepusha na uchukuaji wa vyakula vinavyobaki hotelini na sokoni kwa kuwa vinasadikiwa kuwa na vimelea vinavyochangia uwepo kwa homa hiyo.
Afadhari kwa ufafanuzi mkuu, vinginevyo bia zingeshuka bei

Kumbe ni dom pekee
 
Homa ya nguruwe haiambukizi binadamu wala haiui mtu kamwe. Madhara ya homa ya nguruwe ni ya kiuchumi full stop. Unaambukiza na kuua nguruwe kwa haraka na kwa wingi. Hayo ndio madhara ya homa ya nguruwe (African swine fever). Kwa hiyo ukila mnyama mwenye ugonjwa huwezi kuugua wala kufa. Lakini hata hivyo kuruhusu uuzaji wa nguruwe wenye homa unapaswa kudhibitiwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa. Acheni kusikiliza wanasiasa wanapoelezea masuala ya kitaalam badala ya kuwaachia wataalam waeleze [/
sawa mtaalamu tutaendelea kula
 
Kipindupindu kilipokuja hamkukataza ulaji wa vyakula.

Imekuja homa ya nguruwe mnakataza kula kitimoto.....kwani nguruwe wote wana hiyo homa?
 
Back
Top Bottom