UKAWA kurudi bungeni

Sijui kama nilisikia vizuri kwamba wenzetu UKAWA wamesema watarudi Bungeni kwa kile walichokiita "maslahi mapana ya Taifa".

Swali kwao ni kwamba walipoamua kutoka hawakuyajua hayo maslahi mapana ya Taifa? Si waseme tu kwamba wamezikumbuka posho zao!! Acheni longolongo nyie UKAWA. Kama mnayafahamu maslahi ya Taifa msingetoroka Bungeni wakati wa kujadili KATIBA na wakati huu. Mngepigana kwa hoja ndani ya Bunge. Pili msingeifanya Agenda ya kuonesha Bunge LIVE kama ni issue nzito ya kususia Bunge!
Au niwaulize kidogo, SERA ZENU KWA SASA NI ZIPI BAADA YA KUIFUTA SERA YA KUPINGA UFISADI?
 
hahahahahha ngoja waje wawakikishi kujibu. labda nijibu kwa niaba tu, ni kwamba SERA ILIYOPO SASA BAADA YA KUIFUTA ILE YA KUPINGA UFISADI NI.. KUHAKIKISHA BUNGE LINAKWENDA LIVE ILI WANANCHI WAONE TUNAVYOTOKWA NA MAPOVU MIDOMONI WAKATI WA KUJENGA HOJA HAIJALISHI KAMA TULIPULIZA KIDOGO NJE AU LA!
KWA KUANZIA TU NI HAYO.
 
Hata mimi nimesikia nikacheka sana hili mimi humu nililipigia kelele sana kuwa vichwa vyao si vizuri hawaangalii maslahi mapana ya taifa na majimbo wanayoyawakilisha.
Ninachojua ni kuwa mtu hata ukiwa na kichwa kibovu si tatizo basi uwe na washauri wazuri basi angalau!! UKAWA kuna tatizo tena kubwa
 
Kuhusu swala la Lugumi wakirudi watakuwa wameweka maslahi ya taifa mbele na huyu Tulia atakuwa ameshajifunza kuongoza bunge kwa kufuata kanuni za bunge.
 
Hawa jamaa hawajielewi kabisa kwakweli, wengi wapiga pesa tu hakuna lolote, kusitishiwa posho na wameona kitaa pamenuka ndo wanaamua kuludi eti kwa maslahi mapana ya Taifa, wanafiki tu, na tumekwisha wafahamu vizuri tabia zao.
 
Bora wangesema tu "maslahi mapana ya familia zetu" wangeeleweka tu.

Eti watetezi wa wanyonge,fumbaff kabisa
 
Hahaha wachumia tumbo bana eti kujadili masuala mapana ya taifa.Kiukweli wabunge wengi wa ukawa walikua hawaridhiki na mbowe kuwaburuza buruza kuwatoa nje lakini kwa vile wana nidhamu ya uoga dhidi ya mbowe walikua hawna jinsi, sasa wamenyimwa posho tu wanajifanya kurudi eti kwa maslahi mapana ya taifa..Na babdo mwaka huu mtaisoma namba ..Wengi wa wabunge wa chadema ni vijana na wanamadeni hivo kitendo kile cha kuwanyima posho ilikua ni pigo kubwa kwao....HEKO NAIBU SPIKA WAKAZIE HIVO HIVO HAMNA KUWACHEKEA CHEKEA SAFARI HII.
 
au wameamua kwenda kuungana na wagonga meza? ili kutuibia tu kodi zetu kipitia posho? UKAWA wakiungana na ccm wananchi tumekwisha.
 
Magazeti ya leo yanabainisha kuwa Katibu wa Kambi ya Upinzani, David Silinde amesema UKAWA wako tayari kurudi bungeni hata kama Naibu Spika atakuwa yupo kwenye kiti cha Spika.

Silinde amesema kitakachowarudisha bungeni ni kwenda kujadili masuala yanayohusu maslahi ya taifa na siyo vinginevyo. Mojawapo ya masuala hayo amesema ni lile la sakata la Lugumi.

13406955_1122900304441093_7193222630473890101_n.jpg
Gazeti gani hilo?
 
Back
Top Bottom