BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 500
- 1,209
Kero hiyo ipo zaidi katika Interchange ya SGR ambapo Barabara inayotumika kwa chini ni mbovu na wakati wa mvua hali huwa inazidi kuwa mbaya.
Barabara hiyo inayotumiwa na magari mengi yakiwemo yanayotoka au kwenda Shinyanga imekuwa na msongamano muda mwingi hasa Asubuhi na Jioni, unaweza kutumia hata dakika 60 ukiwa kwenye foleni hapo na hivyo kusababisha shughuli nyingine kusimama.
Baadhi ya Abiria wamekuwa wakilazimika kutoka ndani ya Daladala na kupapnda Bodaboda ili kuwahi kwenye shughuli zao, hali hiyo inachangia kuongezeka kwa gharama za nauli.
Ninachojiuliza mimi na Wananchi wengine wa Mwanza ni kuwa Serikali pamoja na Shiriki la Reli Tanzania (TRC) hawaoni hii kero inayoendelea hapo na wana mpango gani wa kutusaidia?