UHUNI WA UDART: Mmesikia Rais anakuja kuzindua mnajifanya mnajali, mlikuwa wapi siku zote?

Niliwahi kuleta uzi humu, nikiomba ushauri kuwa nataka kuleta MABASI yangu ya MWENDOKASI, watu wakanisema sana, na mwishowe kuna mtu akanambia nijenge Barabara yangu ya Mwendokasi. Sijui jinsi ya kufufua uzi, ningeuweka hapa ujionee!

Ulitakiwa ulete hiyo idea kabla huu mradi haujaanza
 
Kwa sisi watanzania hamna kitu.
Labda hiyo kampuni wapewe wachina, au wazungu, au wahindi.
Au hata wakenya.
Ila kwa sisi sidhani
 
Kama Mh. Raisi anafanya ziara basi nifikishieni haya:
1. chenji bado hawarudishi
2. usalama umepungua
3. mabasi machache
4. yaliyopo yanajaza hadi kero, comfort hakuna tena
5. abiria wanapoteza mda mwingi vituoni kusubiria mabasi

kama vipi kampuni ya UDART wanyanganywe mradi wapewe watu wengine, UDART they are totally inefficient

Nikusaidie kuongeza
6. Kauli zao pia chafu hasa wale wadada wa kwenye vituo
 
Mimi nina maswali mawili: Nauli rasmi ya UDA iliyoidhinishwa na SUMATRA ni sh. ngapi?

Je UDA ni kampuni binafsi au shirika la umma? ni hayo tu ntashukuru sana kwa majibu.
 
Maisha popote,ukiona mahali penye folen hamia kusikokua na folen,ukiona mwendokasi una kero msipande,Ukiona daladala hazina ishu nunua gari zenu,ukiona folen imekolea chukua bodaboda,hatuwez ridhika na kila kitu wala hatuwez ona baya kila kitu ndio tulivyoumbwa binadamu
 
Ni kweli lakini wengi wape
 
Mimi nina maswali mawili: Nauli rasmi ya UDA iliyoidhinishwa na SUMATRA ni sh. ngapi?

Je UDA ni kampuni binafsi au shirika la umma? ni hayo tu ntashukuru sana kwa majibu.
UDA ama UDART?
 
Sijaelewa Mhe.Raisi anaenda kufanya nini hasa? Mtu mmoja nimesikia anasema Raisi anaenda kuzindua kituo cha Gerezani cha Mabasi hayo! Hii Ni kweli? Raisi mzima wa nchi akafanye kazi ya kufungua kituo kama kile? Mbona ni jambo ambalo linapaswa kufanywa tu Na Waziri.Nilitegemea labda aende pale kuzindua awamu nyingine ya ujenzi wa Miundombinu ya mradi Huo.
Huenda atazindua awamu ya pili ya mradi "route" ya Mbagala.
 
Nimegundua nchi hii watu wanapenda kutumbuliwa wenyewe! Siku zote tumekuwa tunalalama huduma mbovu mabasi yaendayo kasi eti mmesikia mh Rais anakuja ndo mnajifanya mnatoa mabasi yenu full time!

Siku zingine mnayaficha ikifika saa 4 mnabakisha machache mnaleta tabu kwa wasafiri kukaa hata dk 40 kituoni!

Leo gerezani nimeona roaster ya safari inaonyesha gari linatakiwa kuondoka kila dk 4, maana yake ndani ya saa 1 zinaondoka gari 15 tu jaman huu si uhuni huu? Jamani UDA mkubali mmeshindwa wapewe wengne hii ni huduma hatutaki mafisadi kwenye miundombinu ya kodi zetu.

Wasimamiz wa vituo ni kama ma mungu mtu! wengine hasa watoto wa kike ni kuchat tu muda wote wanapunga upepo badala ya kusaidia watu wasafiri vituoni humo!

Magari yanajaza sana na kuna hatari ya magonjwa ya milipuko sijui serikali haioni hilo! Nataman mh Raisi kesho angeenda mpaka Kimara asubuh ajionee mateso wanyonge wanavyopata hapo kituoni.

USALAMA vituoni ni 0, akija mtu na kibomu chake ataondoka na kijiji kizima kama hatutamshtukia, hili nalo mpaka Rais aseme? Dah kweli sie vichwa ngumu!

Nalaani mnaotumia mradi huu kujipatia mabilioni wakati huduma za mateso tupu!

Shame on you UDA!
Sasa Magufuli akimtumbua MTU
Wazee wakuropoka Wanamtetea na ninyi mnatoa shangwe!!
Huu unafiki ufikie mwisho
Rais akitumbua
Na wale Wapuuzi wakileta midomo yao tuwakemee kabisa
 
Niliwahi kuleta uzi humu, nikiomba ushauri kuwa nataka kuleta MABASI yangu ya MWENDOKASI, watu wakanisema sana, na mwishowe kuna mtu akanambia nijenge Barabara yangu ya Mwendokasi. Sijui jinsi ya kufufua uzi, ningeuweka hapa ujionee!

Hahaha mnajua kutania!!
 
Back
Top Bottom