Udbs ipo acha uongoChuo kizima hakina hata wifi, kwa dunia ya leo ya sayansi na teknolojia bila internet ni sawa na bure.
Habari za wakati huu wadau.
Huku Nikiamini katika uelewa wetu juu ya umuhimu na nafasi ya Chuo kikuu cha DSM katika nchi yetu.
Nimeona ni vema niwasilishe haya labda itasaidia kuboresha chuo chetu hiki na kukifanya kisimame tena hasa wakati huu ambapo kinaporomoka kielimu kwa kasi hatarishi.
Back to my aim,
1-Kwa nini chuo hakina library na maabara japo moja ya kisasa ya biotechnology, Chemistry ama Physics hadi Leo mwaka 2017? Wanafundishaje wanafunzi hapa? Products zinazotoka zipoje?? Kwenye international market zinafit vipi?
NB: asante wachina mnatujengea hii library, maana huenda hawa walimu wetu wasingegundua kama tunahitaji library.
2. nyie mnaohusika na hii website ya chuo, hivi hamuoni aibu??
Hamjifunzi hata vyuo vingine wanafanyaje?
Nini kinawakwamisha? Ukifungua website ukitaka kutafuta kozi za postgraduate unakutana na attachment (world document) imeorodhesha kozi zote za UDSM..
Sasa foreigner anajuaje course contents?
Sio mtaalamu wa haya mambo but it is disgusting kwa chuo kikubwa kama hiki,
Halafu hiyo picha ya mkuu wa chuo what for???? Tena hapa ni vyuo karibu vyote tz ukifungua websites unakutana na picha za wakuu wa vyuo? Who cares? Hebu tuwe serious. We can't market our education in this way.
3.
Mnafanyaje analysis ya mahitaji ya soko?
Wahitimu wenu mnatupimaje kama tunaendana na mahitaji ya jamii kwa wakati husika?
Vipi kwenye soko la kimataifa? Tunafit huko?
4. Mazingira na Miundombinu ya Chuo kwa ujumla.
Mimi nlidhani nikiingia chuoni walau nikute mazingira safi, yanatunzwa na majengo walau yana mwonekano wa chuo kikuu, ukizingatia hapa kuna wataalamu wa mazingira, mainjinia, botanists, zoologists, economists, na wataalamu wa kila aina,
Na jamii kwa ujumla ichukulie UDSM kama sehemu pa mfano wa Kuigwa. Sio mahala pachafu kama palivyo sasa.
UDSM pamoja na kuwa na uoto mzuri wa asili, mazingira haya hutunzwa na mvua za msimu na hata majengo ya chuo yamechoka mithiri ya mabanda ya kufugia ng'ombe ya SUA.
Jamani pakeni rangi japo hilo jengo la utawala,
Au mnasubiri tena Magufuli awaambie mpake kama alivyowaambia mjenge hostel??
Be proactive aisee, or pisheni wakae wengine.
Tizama haya majengo ya chuo kikubwa nchini
Hili la kwanza ni jengo la utawala, Lina minara juu utadhani jengo la Jeshi la kdf, sijui tigo wamefunga mitambo yao huko juu.. I don't know.
View attachment 473913
View attachment 473915View attachment 473916
Meanwhile, vyuo Vingine vya Hadhi ya UDSM
Makerere University-UG
View attachment 473924
View attachment 473917
Cairo University -Egypt
View attachment 473918
University of KwaZulu Natal-SA
View attachment 473919
University of Cape town -SA
View attachment 473920View attachment 473921
NB, UDSM pesa sio shida kwao.
Wala Human resource sio Tatizo .
Hivyo sioni sababu yoyote ya msingi kwa UDSM kutokuwa level za Pretoria University.