ARIUS MZUSHI
JF-Expert Member
- Jun 18, 2017
- 272
- 110
Na dawa ya ukweli ni nini??
Mkuu mbona hueleweki fafanuwa! make lini uongo uligeuka kuwa ukweli!!!Najikumbusha kitu kuhusu dhana ya udikiteta, jee huu udikiteta unaozungumzwa sana nchini Tanzania ni kweli upo au ni dhana tuu?.
Kama ni uongo na uzushi, mbona haukanushwi?!.
Na jee kweli uongo ukisemwa sana bila kukanushwa hugeuka kuwa ukweli?.
P
Lissu kajimaliza...kauli zake hizo, haina tofauti na kauli ya kipuuzi aliyowahi kuitoa Zitto Kabwe kuwa Kilimanjaro inainyonya Shinyanga. Na Zitto alisurubiwa, , kweli na mwalimu wangu maarufu hapa JF ( Nguruvi3 )na wanaJF wengine na mimi ni kwemo kwa kauli ile.....
Bado hoja ya Lissu inahitaji kujadiliwa ili kuweza kubaini ukweli wa jambo hili vinginenvyo etaleta sinto faham nyingi sana kiasi cha watu kushangaa mbona Rais hazindui miradi katika mikoa ya kaskazini.
Hatuwezi kuacha hili jambo kuelea, nilazima Lissu ajibiwe kwa ushahidi aondoe hii dhana potofu.
General Mangi
Hapa nakumbushia uongo kusemwa bila kukanushwa hugeuka ukweli.Wanabodi,
Baada ya rais Magufuli kuombea malaika watoke mbinguni kuja kuifunga mitandao ya kijamii yenye uongo na Uzushi kama humu jf, wana mitandao wote resiponsible hatuna budi kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kuitumia mitandao ya kijamii more responsibility kwa nia njema (in good faith) ya kujenga, kuwa wakweli na hata tukikosoa tukikosoa constructively kwa kukosoa ili kujenga na sio kukosoa ili kubeza.
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukiletwa humu, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu hapo hapo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusema.
Nakiri kupandisha uzi huu baada ya kuwa inspired na bandiko la mwana jf huyu.
Mkuu Sema, naunga mkono hoja.
Dawa ya uongo uzushi na upotoshaji ni ukweli, utoaji majibu kwa uharaka na usahihi.
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho unageuka ukweli na mfano mdogo ni hii dhana ya udikiteta, ni uwongo tuu na uzushi kumzushia rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni dikiteta kwa kitendo tuu cha kupiga marufuku mikutano ya hadhara.
Uzushi huu ulianzia humu jf na mwanzilishi namjua!, haukukanushwa, uzushi huu ukadakwa na Chadema mara wanaibuka na ukuta, haukukanushwa sasa hadi sasa neno dikiteta limeanza kuwa rasmi.
Iwapo Ikulu yetu ingekuwa na mtu wao humu jf na wakaukanusha mara moja uzushi ule kwa kuusema ukweli jina la udikiteta isingekuwepo.
Katiba imetoa uhuru wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhara, rais alipopiga marufuku mikutano hiyo ilikuwa ni kazi ndogo tuu watu wake kuingia humu na kueleza Mhe rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu fulani fulani, basi kusingekuwepo hoja ya udikiteta wala ukuta, lakini kitendo cha mpaka leo hii ninapoandika hapa hakuna kanusho lolote lenye kuonyesha mamlaka ya rais kutenda kinyume cha maelekezo ya katiba, kunapelekea uwongo huo wa udikiteta kuonekana kama ndio ukweli wenyewe.
Kila uongo ukiachwa unageuka ukweli na ukikanushwa unafutika.
Paskali
Hapana Pasco alichoongea ni sawa ... pia ni kweli upo uongo unao tetewa lakini si inatakiwa utetewe kwa sheria na taratibu ... sasa kama hizo sheria na taratibu wanazo zitetea zitakuwepo basi hautokua uongo tena ...Kaka Pasco, hoja yako hasa ni ipi? Unaandika mambo mengi lakini hulengi kwenye hoja. Unathibitishaje kuwa unaouita uzushi ni uzushi au uongo kweli? Kwani hakuna uzushi na uongo unaotetewa? Uongo ni uongo;ukweli ni ukweli
Lissu kajimaliza kwa kusema ukweli au kwa kupigwa risasi?Lissu kajimaliza...kauli zake hizo, haina tofauti na kauli ya kipuuzi aliyowahi kuitoa Zitto Kabwe kuwa Kilimanjaro inainyonya Shinyanga. Na Zitto alisurubiwa, , kweli na mwalimu wangu maarufu hapa JF ( Nguruvi3 )na wanaJF wengine na mimi ni kwemo kwa kauli ile.
Duru za siasa: Chama cha ACT -Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani
Hamkani si shwari tena, by chinua achebe.Lissu kajimaliza kwa kusema ukweli au kwa kupigwa risasi?
Mkuu ostrichegg , sina uhakika, lakini humu jf, sidhani kama kuna member mwingine yoyote aliyeuzungumzia udikiteta kama mimi!.🤣 🤣🤣🤣Kwa hiyo sasa hutaki tena kukumbuka jinsi ulivyokuwa unajitahidi kuupaka rangi UDIKTETA ili sio tu kuupendezesha bali pia kuweka mzingira ya 'kutosahauliwa'?. Kama ni kweli basi ninakutakia heri ingawaje itabidi kukuangalia kidogo kabla sijakuamini.
Bandiko hili bado linasadifu , kama haya aliyo yaandika Kabendera kuhusu kifo cha Ben Saanane, kama ni uongo, serikali ikanushe na kueleza ukweli Ben Saanane alitowekaje.Wanabodi,
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukiletwa humu, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu hapo hapo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusema. Kila uongo ukiachwa unageuka ukweli na ukikanushwa unafutika. Paskali