Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,754
- 121,803
Wanabodi,
Baada ya rais Magufuli kuombea malaika watoke mbinguni kuja kuifunga mitandao ya kijamii yenye uongo na Uzushi kama humu jf, wana mitandao wote resiponsible hatuna budi kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kuitumia mitandao ya kijamii more responsibility kwa nia njema (in good faith) ya kujenga, kuwa wakweli na hata tukikosoa tukikosoa constructively kwa kukosoa ili kujenga na sio kukosoa ili kubeza.
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho wake unageuka kuwa ndio ukweli, hivyo dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukiletwa humu, kama kuna mwenye ukweli autoe tuu hapo hapo ili kutoupa fursa uongo huo kuendelea kusema.
Nakiri kupandisha uzi huu baada ya kuwa inspired na bandiko la mwana jf huyu.
Dawa ya uongo uzushi na upotoshaji ni ukweli, utoaji majibu kwa uharaka na usahihi.
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa mwisho unageuka ukweli na mfano mdogo ni hii dhana ya udikiteta, ni uwongo tuu na uzushi kumzushia rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni dikiteta kwa kitendo tuu cha kupiga marufuku mikutano ya hadhara.
Uzushi huu ulianzia humu jf na mwanzilishi namjua!, haukukanushwa, uzushi huu ukadakwa na Chadema mara wanaibuka na ukuta, haukukanushwa sasa hadi sasa neno dikiteta limeanza kuwa rasmi.
Iwapo Ikulu yetu ingekuwa na mtu wao humu jf na wakaukanusha mara moja uzushi ule kwa kuusema ukweli jina la udikiteta isingekuwepo.
Katiba imetoa uhuru wa kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhara, rais alipopiga marufuku mikutano hiyo ilikuwa ni kazi ndogo tuu watu wake kuingia humu na kueleza Mhe rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu fulani fulani, basi kusingekuwepo hoja ya udikiteta wala ukuta, lakini kitendo cha mpaka leo hii ninapoandika hapa hakuna kanusho lolote lenye kuonyesha mamlaka ya rais kutenda kinyume cha maelekezo ya katiba, kunapelekea uwongo huo wa udikiteta kuonekana kama ndio ukweli wenyewe.
Kila uongo ukiachwa unageuka ukweli na ukikanushwa unafutika.
Paskali

Mkuu Sema, naunga mkono hoja.Mh rais kwanza Napenda kukupongeza kwa Kazi nZuri Na jitihada zako ambazo zinaanza kuzaa matunda, songa mbele maana tunakuombea pamoja Na changamoto hizo tutafika. Lengo la kuandika andiko hili Ni kukushauri Na kukuunga mkono juu ya sikitiko lako juu ya upotoshaji mitandaoni.
Ushauri wangu Ni mfupi kuwa dawa ya Moto Ni Moto Na kwamba ili kukabiliana Na upotoshaji huu , dawa sio kuizuia Bali kuwawezesha wafanyakazi wa serikali kukabiliana Na upotoshaji huu kwa kuwa tayari kueneza ukweli kupitia mitandao hiyo hiyo . Kwa kuanzia kila msemaji Au afisa Habari wa wizara Na vitengo vya serikali afundishwe namna bora ya kutumia mitandao hiyo . Pili iwepo sera ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii kwa kila kitengo cha serikali Na Tatu TCRA waongezewe uwezo wa kushughulikia wahalifu wa mitandaoni kwa kupewa mafunzo zaidi...
Wadau tuongezee....
Moderators: please Naomba msiunganishe uzi huu Na mwwingine .