DOKEZO UDART wameanza wizi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Siku za hivi karibuni hawa watu wa mabasi yaendayo Kasi(UDART) Wameanza wizi wa wazi wazi. Ukienda kukatq ticket halafu ukatoa hela kubwa zaidi ya gharama ya ticket yako wanakuambia uwaongezee 150 au 200 ndipo upewe change yako. Kama huna itabidi wakusubirishe. Na kama una haraka zako utachukua ticket yako na kuwaachia hiyo 150 au 200.

Kwa hesabu za haraka haraka unaweza ona ni hela ndogo sana hiyo 150 hadi 200 kwa mtu mmoja. Lakini ukikaaa na kufikiria kama endapo abiria 1000 wataachia hiyo 150 hadi 200 basi jumla yake ni 150,000 hadi 200,000. Maana ni vituo vyote vya mwendokasi wanafanya hivyo.

Sasa huu ni wizi wa mchana kweupe. Hizi hujuma zimeanza tokea kuanza kwa mwaka mpya. Hakukuwa na tatizo la change mwaka jana na kurudi nyuma. SUMATRA, LATRA pamoja na TAMISEMI liangalieni hili. Hawa UDART wanatuibia Watanzania.
 
Tunachokiweza Watanzania ni kifo tu mengine kamwe hatuwezi. Huu mradi ulikuwa mradi bora na kuigwa lakini kama kawaida ya mwafrika mtanzania ameshauharibu. Nasisitiza tunachokiweza watanzania ni kifo tu.
 
Naalafu wanakawaida ya kuwapa watu chench pungufu usipokuwa makini, hasa ukitoa 10k na unaharaka
 
Hapo ni mazingira ya upigaji yanatengenezwa na hao jamaa. Mwanzo walianzaga na style ya kujisahaulisha chenchi. Badala ya kurudisha 350 ukimpa buku yeye anarudisha shilingi hamsini hamsini ila hazifiki 350.

Yamkini anaweza kupa 250 ila kama hutagundua anakua kakupiga 100! Akifanya hivi kwa watu 300 tu tayari ana elfu 30 yake.

Kitu ambacho naona ni kuwa huenda jamaa walikuwa na namna ya kupata hela bila kuibia abiria ila sasa huo mrija umezibwa kwahio imebidi wageukie abiria na kuanza kuwapiga mchana kweupe na maboss wao wamebariki hilo bila shaka.
 
Inashangaza kuwa eti vituo vyote sh 50, 100 na 200 hazipo. Zimeenda wapi?? Au wanataka kutuambia kuwa hiziz silver zinataka kuondoshwa kwenye mzunguko wa BOT?? Wizi wizi wizi.
 
Tunachokiweza Watanzania ni kifo tu mengine kamwe hatuwezi. Huu mradi ulikuwa mradi bora na kuigwa lakini kama kawaida ya mwafrika mtanzania ameshauharibu. Nasisitiza tunachokiweza watanzania ni kifo tu.
Watanzania sisi tupo bado kwenye process wa evaluation ya kuwa binadamu kamili bado hatujakamilika.
Tuvumiliane.
 
Nauli isingekuwa ya chenji chenji..........ingekuwa buku au jero tu ili kusiwe na kero hizi za chenji
 
halafu huduma zao ni mbovu mbovu mno mno ktk maeneo haya;
1. Kukaa vituoni mida mrefu (hadi saa 1) bila kupata usafiri.
2. Kujaza abiria kwa kaisi cha kutisha hadi kukosekana hewa ndani ya mabasi yao.
3. Lugha chafu sana kwa wakataji tiketi (hasa kituo cha kimara terminal)
4. Hakuna huduma za kijamii ktk vituo vyao (ie washroom na maji ya kunawa ktk vi tank)
 
Inashangaza kuwa eti vituo vyote sh 50, 100 na 200 hazipo. Zimeenda wapi?? Au wanataka kutuambia kuwa hiziz silver zinataka kuondoshwa kwenye mzunguko wa BOT?? Wizi wizi wizi.

Hizo wanazolipa watu wa change kamili zinaenda wapi?
 
halafu huduma zao ni mbovu mbovu mno mno ktk maeneo haya;
1. Kukaa vituoni mida mrefu (hadi saa 1) bila kupata usafiri.
2. Kujaza abiria kwa kaisi cha kutisha hadi kukosekana hewa ndani ya mabasi yao.
3. Lugha chafu sana kwa wakataji tiketi (hasa kituo cha kimara terminal)
4. Hakuna huduma za kijamii ktk vituo vyao (ie washroom na maji ya kunawa ktk vi tank)

Kimara nishabomoana na mdada askari

Na nimemuweka alama siku nikimkuta mitaa yangu lazima nimvuruge

Wananyanyasa sana abiria
Halafu serikali naona washabariki

Wananchi tujipambanie tu wenyewe
 
Kitu ambacho naona ni kuwa huenda jamaa walikuwa na namna ya kupata hela bila kuibia abiria ila sasa huo mrija umezibwa kwahio imebidi wageukie abiria na kuanza kuwapiga mchana kweupe na maboss wao wamebariki hilo bila shaka.
sisi tumelaaniwa kwa wizi
 
Hapo wezi ni wakata tickets na sio kampuni ya UDART, maana hizo fedha haziingii katika mfuko wa ofisi.
Kama vipi nyie abiria 1000 mucheze mchezo , chenji chukueni kwa zamu. Kila siku anatoka mmoja na kitita cha 150,000 tshs.
😝😝😝😝😝
 
Mambo haya yanatia uchungu mnoooo
Nimeanza kujionea ukweli wa Yeremia 10:23b.:"MWANADAMU ANAYETEMBEA HANA UWEZO WA KUONGOZA HATUA YAKE."
Sasa kama siwez ongoza hatua zangu ntawezaje kuwaongoza wengne?
 
Siku za hivi karibuni hawa watu wa mabasi yaendayo Kasi(UDART) Wameanza wizi wa wazi wazi. Ukienda kukatq ticket halafu ukatoa hela kubwa zaidi ya gharama ya ticket yako wanakuambia uwaongezee 150 au 200 ndipo upewe change yako. Kama huna itabidi wakusubirishe. Na kama una haraka zako utachukua ticket yako na kuwaachia hiyo 150 au 200.

Kwa hesabu za haraka haraka unaweza ona ni hela ndogo sana hiyo 150 hadi 200 kwa mtu mmoja. Lakini ukikaaa na kufikiria kama endapo abiria 1000 wataachia hiyo 150 hadi 200 basi jumla yake ni 150,000 hadi 200,000. Maana ni vituo vyote vya mwendokasi wanafanya hivyo.

Sasa huu ni wizi wa mchana kweupe. Hizi hujuma zimeanza tokea kuanza kwa mwaka mpya. Hakukuwa na tatizo la change mwaka jana na kurudi nyuma. SUMATRA, LATRA pamoja na TAMISEMI liangalieni hili. Hawa UDART wanatuibia Watanzania.
Walivyoacha kutumia electonic devices kwenye kuhakiki tiketi nilijua tushapigwa...

Huu unaouweka hapa ni wizi endelevu
 
Back
Top Bottom