ecolizer baba
Member
- Sep 29, 2010
- 88
- 310
Siku za hivi karibuni hawa watu wa mabasi yaendayo Kasi(UDART) Wameanza wizi wa wazi wazi. Ukienda kukatq ticket halafu ukatoa hela kubwa zaidi ya gharama ya ticket yako wanakuambia uwaongezee 150 au 200 ndipo upewe change yako. Kama huna itabidi wakusubirishe. Na kama una haraka zako utachukua ticket yako na kuwaachia hiyo 150 au 200.
Kwa hesabu za haraka haraka unaweza ona ni hela ndogo sana hiyo 150 hadi 200 kwa mtu mmoja. Lakini ukikaaa na kufikiria kama endapo abiria 1000 wataachia hiyo 150 hadi 200 basi jumla yake ni 150,000 hadi 200,000. Maana ni vituo vyote vya mwendokasi wanafanya hivyo.
Sasa huu ni wizi wa mchana kweupe. Hizi hujuma zimeanza tokea kuanza kwa mwaka mpya. Hakukuwa na tatizo la change mwaka jana na kurudi nyuma. SUMATRA, LATRA pamoja na TAMISEMI liangalieni hili. Hawa UDART wanatuibia Watanzania.