Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,531
- 3,332
Kampuni ya usafirishaji katika jiji la Dar-es-Salaam (UDART) maarufu kama mwendokasi inatakiwa ijitathmini utendaji wake mara moja kwani huduma ya usafiri wa mabasi haya ni kero kwa wananchi.
Madereva wakifika katika vituo vyao vikubwa (terminal) badala ya kupakia abiria waliojazana kwenye vituo wao wanapaki mabasi pembeni na kuanza kupiga soga. Kitendo kinachopelekea abiria kukaa vituoni zaidi ya dakika 30 mpaka 40. Hivi mnadhani hawa wananchi waolipa hizi 1000, 650 au 400 hawana kazi za kufanya?
Kiukweli mnakera hasa kituo kikuu cha Morocco, Kimara, kivukoni na Gerezani.
Wito wangu kwa serikali iruhusu makampuni/wawekezaji wengine waingize mabasi katika njia ya mwendokasi ili kuboresha ushindani katika utendaji kazi. Abiria hatakiwi kukaa kituoni zaidi ya dakika 5.