Uchaguzi 2025 Uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA kufanyika Oktoba 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
126,495
241,223
Taarifa ikufikie Popote ulipo kwamba, Uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya Kitaifa wa Chadema utafanyika mwezi wa 10, 2024, hii ni baada ya kumalizika kwa Chaguzi zingine zote za Chama hicho katika ngazi zote za chini.

Taarifa hii nzuri imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Benson Kigaila.

NYONGEZA: Fomu za kugombea Uchaguzi huo zitachapishwa nyingi sana na Wakati ukifika Mtatangaziwa, Jitokezeni kuzichukua, hakuna kizuizi chochote, ukijipima kwamba unaweza jitokeze.

Mungu Ibariki Chadema.

JamiiForums442997317_236x211.jpeg
 
Uchaguzi au mazingaombwe mwenyekiti asiye na kikomo ni mbowe makamu lissu katibu mnyika wala msipoteze pesa kwenda tanga kufanya uchaguzi!
 
Taarifa ikufikie Popote ulipo kwamba , Uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya Kitaifa wa Chadema utafanyika mwezi wa 10 , 2024 , hii ni baada ya kumalizika kwa Chaguzi zingine zote za Chama hicho katika ngazi zote za chini .

Taarifa hii nzuri imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Benson Kigaila .

NYONGEZA : Fomu za kugombea Uchaguzi huo zitachapishwa nyingi sana na Wakati ukifika Mtatangaziwa , Jitokezeni kuzichukua , hakuna kizuizi chochote , ukijipima kwamba unaweza jitokeze .

Mungu Ibariki Chadema

View attachment 2967247
Itatoka Fomu moja tu ya Mbowe
 
Iko wazi kwamba Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe alitangaza pale Mlimani City kwenye mkutano wa Bawacha kwamba huu ni muhula wake wa Mwisho anang'atuka na anapenda mrithi wake atoke Bawacha.

Sasa mh Benson umetangaza Uchaguzi wa Viongozi wa taifa Kufanyika October Baada ya chaguzi zote Kuwa zimekamilika, nafikiria ni vema ungekazia katika tamko lako Kuwa Mwenyekiti wa sasa anang'atuka ama la Ili Kuwapa Uwanja mpana na Huru Wanachama waliotamani kugombea Nafasi ya Mwenyekiti Taifa.

Niko Hapa nasubiri ufafanuzi.

Wasalaam 😄
 
Back
Top Bottom