Kuelekea 2025 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Macho yote Mwaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Kimalingano

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
626
820
Nikisiliza kwa makini namna kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu, nashuhudia kabisa kuwa uchaguzi huu ni maandalizi ya moja kwa moja kwa ajili ya mwakani. Si ajabu watu wanatekana, wanauana na kila aina ya hujuma wanafanyiana ikiwemo ndani kwa ndani ya vyama vya siasa na vyama kwa vyama.

Pia, si ajabu hata maagizo ya Mhe. Samia kupitia Nchimbi kuwa walioenguliwa kwa sababu ndogo ndogo waruhusiwe kugombea hayakutekelezwa. Kwa sababu uchaguzi wa mwakani utakuwa wa mtu binafsi zaidi kuliko Chama. Mgombea wa ubunge, kwa mfano, atalazimika apambane yeye binafsi bila msaada mkubwa wa Chama chake.

Hata Rais Samia atatakiwa kutumia watu wake wa karibu kama alivyofanya Kikwete awamu yake ya pili kwa kuwatumia familia yake na baadhi ya watu wake wa karibu zaidi kutokana na ukweli kuwa atakuwa amelazimisha CCM imusimamishe ingawa hawataki kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom