Uchaguzi wa Papa ni wa kiimani, siyo uchaguzi kama tulivyozoea

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,542
8,276
Wengi wakisikia uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, wanadhani ni uchaguzi kama hizi chaguzi tunaazozifanya kuwachagua viongozi wa kijamii.

Mchakato wa Uchaguzi wa kumpata Papa, ni mrefu na mgumu kwa sababu umejengwa kwa msingi wa kiimani kuliko werevu wa kibinadamu. Mambo muhimu yanayoonesha utofauti mkubwa wa uchaguzi wa Papa na Chaguzi nyingine za kawaida:

1. Hairuhusiwi kupiga kampeni yoyote ile.

2. Hakuna majina ya wagombea, iwe ni wao wenyewe kwa kutaka au kupendekezwa.

3. Uchaguzi kura hupigwa mara 2 kwa siku, asubuhi na mchana, kwa kutumia maboksi mawili tofauti.

4. Kila kadinali anatakiwa kuandika jina la mtu anayemfikiria anafaa kuwa kiongozi mkuu wa kanisa, bila ya yeye kujadiliana na mtu mwingine yeyote. Mtu huyo anayestahili kuwa Papa anaweza kuwa miongoni mwa makadinali au hata asiye kadinali alimradi ana daraja la uaskofu.

4. Kila zoezi linapokamilika, kura huhesabiwa, na anayekuwa amependekezwa na makadinali wengi, lazima iwe kuanzia theluthi 2 kwenda juu , ndiye anayetangazwa kuwa Papa.

5. Kama hatapatikana aliyepata theluthi 2 kwenda juu, zoezi hurudiwa kwa siku 3 mfululizo.

6. Kama hata baada ya siku 3, hakuna aliyepata kura kuanzia kura theluthi 2 kwenda juu, waumini wanatengaziwa kuwa papa hajapatikana, bila hata ya kusomewa matokeo, kujua nani wamepigiwa kura na wamepata kura ngapi kila mmoja.

7. Kama Papa hakupatikana baada ya siku 3 mfululizo za kupiga kura, uchaguzi husimamishwa, na makadinali huingia katika maombi maalum. Kisha zoezi hurudiwa.

A. Wakati wote, makadinali wanapoingia kwenye maombi na wakati upigaji kura unaendelea, wakristo wengi huwa nje, nao wakifunga na kuomba ili Mungu amteue kiongozi wake mkuu wa Kanisa la hapa Duniani, kupitia kura zinazopigwa na makadinali.

NB: Historia inaonesha kuwa kuna wakati baada ya kupita miezi 6 bila ya kupatikana papa, waumini waliokuwa nje wakiomba na kufunga, huku kipindi cha baridi kikiwa kimeingia, walikasirika na kwenda kuvunja paa la jengo ambalo makadinali walikuwa wamejifungia. Waumini hao walidai kuwa makadinali walikosa imani ndiyo maana papa ameshindwa kupatikana. Makadinali wakapigwa na baridi kali, baada ya siku chache, Papa alipatikana.

Mpaka sasa, rekodi inayoonesha papa alipatikana kwa taabu sana, baada ya miaka mitatu, ni wa mwaka 1268, kufuatia kifo cha Papa Clement wa 4. Sababu zinazotajwa ni kwamba kulikuwepo makadinali waliotaka kutumia mbinu za kisiasa kuipata nafasi hiyo.

Kati ya mapapa wanaotajwa kupatikama kwa urahisi kabisa, ni Papa John Paulo wa pili, ambaye mzunguko wa kwanza tu, tayari kura zilitimia, na mchakato ukawa umekamilika.

Waumini wakatoliki na wasio wakatoliki, tumwombe Mungu amteue mtumishi afaaye kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya taasisi mojawapo kubwa kabisa ya kidini, yenye nafasi ya kugusa maisha ya watu wengi bila ya kujali imani zao
 
Kama ndivyo then why kuwe na rumours kuhusu yule jamaa wa ghana?

Huwezi kuzuia rumours. Hizo ni fikra za mtu mmoja mmoja, labda kwa sababu ni kati ya makadinali wanaoshikilia nafasi kubwa pale Vatican. Na inawezekana hizo rumours zipo huku Afrika. Huko America America, Ulaya na Australia kunaweza kuwa na rumours za watu tofauti.
 
CCM inaamini:

1. Binadamu wote ni sawa

2. Rushwa ni adui wa Haki

3. Ujamaa na Kujitegemea ndio itikadi sahihi ya kuleta maendeleo

Hizo zimebbakia tu kuwa nadharia.

CCM ya leo haiiamini katika usawa wa binadamu, ndiyo maana mtu asipokuwa CCM au akawa ndani ya CCM, lakini akakikosoa chama, Serikali au Rais anageuka kuwa adui, na kuwa binadamu asiye na haki yoyote, anaweza kutekwa na kuuawa au kupotezwa au kubambikiwa kesi za ajabu.
 
Wengi wakisikia uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, wanadhani ni uchaguzi kama hizi chaguzi tunaazozifanya kuwachagua viongozi wa kijamii.

Mchakato wa Uchaguzi wa kumpata Papa, ni mrefu na mgumu kwa sababu umejengwa kwa msingi wa kiimani kuliko werevu wa kibinadamu. Mambo muhimu yanayoonesha utofauti mkubwa wa uchaguzi wa Papa na Chaguzi nyingine za kawaida:

1. Hairuhusiwi kupiga kampeni yoyote ile.

2. Hakuna majina ya wagombea, iwe ni wao wenyewe kwa kutaka au kupendekezwa.

3. Uchaguzi kura hupigwa mara 2 kwa siku, asubuhi na mchana, kwa kutumia maboksi mawili tofauti.

4. Kila kadinali anatakiwa kuandika jina la mtu anayemfikiria anafaa kuwa kiongozi mkuu wa kanisa, bila ya yeye kujadiliana na mtu mwingine yeyote. Mtu huyo anayestahili kuwa Papa anaweza kuwa miongoni mwa makadinali au hata asiye kadinali alimradi ana daraja la uaskofu.

4. Kila zoezi linapokamilika, kura huhesabiwa, na anayekuwa amependekezwa na makadinali wengi, lazima iwe kuanzia theluthi 2 kwenda juu , ndiye anayetangazwa kuwa Papa.

5. Kama hatapatikana aliyepata theluthi 2 kwenda juu, zoezi hurudiwa kwa siku 3 mfululizo.

6. Kama hata baada ya siku 3, hakuna aliyepata kura kuanzia kura theluthi 2 kwenda juu, waumini wanatengaziwa kuwa papa hajapatikana, bila hata ya kusomewa matokeo, kujua nani wamepigiwa kura na wamepata kura ngapi kila mmoja.

7. Kama Papa hakupatikana baada ya siku 3 mfululizo za kupiga kura, uchaguzi husimamishwa, na makadinali huingia katika maombi maalum. Kisha zoezi hurudiwa.

A. Wakati wote, makadinali wanapoingia kwenye maombi na wakati upigaji kura unaendelea, wakristo wengi huwa nje, nao wakifunga na kuomba ili Mungu amteue kiongozi wake mkuu wa Kanisa la hapa Duniani, kupitia kura zinazopigwa na makadinali.

NB: Historia inaonesha kuwa kuna wakati baada ya kupita miezi 6 bila ya kupatikana papa, waumini waliokuwa nje wakiomba na kufunga, huku kipindi cha baridi kikiwa kimeingia, walikasirika na kwenda kuvunja paa la jengo ambalo makadinali walikuwa wamejifungia. Waumini hao walidai kuwa makadinali walikosa imani ndiyo maana papa ameshindwa kupatikana. Makadinali wakapigwa na baridi kali, baada ya siku chache, Papa alipatikana.

Mpaka sasa, rekodi inayoonesha papa alipatikana kwa taabu sana, baada ya miaka mitatu, ni wa mwaka 1268, kufuatia kifo cha Papa Clement wa 4. Sababu zinazotajwa ni kwamba kulikuwepo makadinali waliotaka kutumia mbinu za kisiasa kuipata nafasi hiyo.

Kati ya mapapa wanaotajwa kupatikama kwa urahisi kabisa, ni Papa John Paulo wa pili, ambaye mzunguko wa kwanza tu, tayari kura zilitimia, na mchakato ukawa umekamilika.

Waumini wakatoliki na wasio wakatoliki, tumwombe Mungu amteue mtumishi afaaye kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya taasisi mojawapo kubwa kabisa ya kidini, yenye nafasi ya kugusa maisha ya watu wengi bila ya kujali imani zao
Mbona sijaona chochote cha ajabu cha kuutofautisha huu uchaguzi na chaguzi zingine? Mwisho wa siku papa anapatikana kwa kupigiwa KURA kati ya makadinali wanaofahamika "wagombea".

Mi nilidhani labda jina linashushwa kutoka mbinguni..
 
Hivi papa huwa hawafanyi miujiza na ishara zozote zaroho mtakatifu? Binafsi sijawahi ona hata kamtoa mtu mapepo,au kamgusa Mgonjwa akapona!nk. Mbona Inakuaga anashangiliwa tuuu

Mwanadamu yeyote hana uwezo wa kufanya miujiza. Miujiza hufanywa ama na Mungu ama shetani. Ukisikia mtumishi wa Mungu anasema kuwa yeye anafanya miujiza, ujue ni tapeli. Lakini Mungu, kwa gekima yake anaweza kufanya miujiza kwa kupitia mikono ya wanadamu. Hata shetani anaweza kufanya miujiza kwa kuputia mikono ya wanadamu.

Hata mitume, japo walifanya miujiza, lakini haikuwa wakati wote, bali ni wakati maalum, kwa kutegemea hekima yake.

Wapo mapapa ambao kwa mikono yao, miujiza ilifanyika, lakini siyo wakati wote. Hata huyu Papa Francus, kwa mkono wake, mara kadhaa miujiza ilitendeka:

Pope Francis may yet earn the accolade "The Healing Pope" for the miracles he has been performing when touching people with serious health problems.

When the Pope flew to New York last week as part of his six-day apostolic visit to the United States, he once again showed his healing power when he blessed a 12-year-old girl who was one of those who greeted him at JFK Airport, The Gospel Herald said.

Julia Bruzzese of Brooklyn, New York was in a wheelchair when the smiling Pope stopped by, touched her face and blessed her. She had been using the wheelchair ever since she suffered a sudden paralysis whose cause puzzled her doctors no end.

Her doctors said she seemed to exhibit symptoms of Lyme disease. But the problem was that her blood tests showed she was negative for that disease.

Tofauti kubwa ya wakatoliki na makanisa ya kiroho, hawajatanguliza miujiza kama msingi wa imani. Hivyo miujiza ya uponyaji hawaitangazi sana kwa sababu kuitangaza sana na kuihusisha na mtu fulani, inakuwa ni kutaka kupokonya utukufu, ukuu na sifa ya Mungu, ambaye ndiye hasa mponyaji.
 
Papal conclave - Mchakato uliodumu kwa miaka zaidi ya 2000 na mchakato mkongwe zaidi na wa kipekee uliosalia katika mfumo wa Monarchy. Makardinali hukusanyika huko Sistine Chapel kwa kuimba Litania ya watakatifu wote na misa ya watu wote hufanyika, Kisha Camerlengo hutamka maneno maarufu "Extra Omnes" yaani "Tokeni nje" hapo wale wasiohusika huambiwa watoke nje na milango hufungwa na mchakato huanza.Kuna wakati mchakato huchukua muda mrefu mpaka baadhi ya Makardinali hufia humohumo ndani ya kanisa, na mchakato huweza kwenda hata miezi mitatu. Kura zinapokuwa pungufu huchomwa na moshi mweusi huonekana, kura zinapojitosheleza moshi mweupe huonekana, Na papo hapo makardinali wote humpa heshima yule aliyechaguliwa, kisha anaenda kufungiwa katika chumba maarufu kama "Room of tears" ili kuchukua muda kutafakari kuondoa presha na kusali na kutafakari uzito wa kazi ambayo ipo mabegani mwake maana atakapotoka nje na kutambulishwa maisha yake yatabadilika na kuwa mtu tofauti kwa kiasi kikubwa. Kisha akitoka huulizwa "Je, umekubali kuwa papa? Na unachagua jina gani?" Baada ya taratibu za ndani kukamilika ndipo dunia hujulishwa kwa ile kauli maarufu ya " HABEMUS PAPAM" na hutambulishwa duniani.
 
Mwanadamu yeyote hana uwezo wa kufanya miujiza. Miujiza hufanywa ama na Mungu ama shetani. Ukisikia mtumishi wa Mungu anasema kuwa yeye anafanya miujiza, ujue ni tapeli. Lakini Mungu, kwa gekima yake anaweza kufanya miujiza kwa kupitia mikono ya wanadamu. Hata shetani anaweza kufanya miujiza kwa kuputia mikono ya wanadamu.

Hata mitume, japo walifanya miujiza, lakini haikuwa wakati wote, bali ni wakati maalum, kwa kutegemea hekima yake.

Wapo mapapa ambao kwa mikono yao, miujiza ilifanyika, lakini siyo wakati wote. Hata huyu Papa Francus, kwa mkono wake, mara kadhaa miujiza ilitendeka:

Pope Francis may yet earn the accolade "The Healing Pope" for the miracles he has been performing when touching people with serious health problems.

When the Pope flew to New York last week as part of his six-day apostolic visit to the United States, he once again showed his healing power when he blessed a 12-year-old girl who was one of those who greeted him at JFK Airport, The Gospel Herald said.

Julia Bruzzese of Brooklyn, New York was in a wheelchair when the smiling Pope stopped by, touched her face and blessed her. She had been using the wheelchair ever since she suffered a sudden paralysis whose cause puzzled her doctors no end.

Her doctors said she seemed to exhibit symptoms of Lyme disease. But the problem was that her blood tests showed she was negative for that disease.

Tofauti kubwa ya wakatoliki na makanisa ya kiroho, hawajatanguliza miujiza kama msingi wa imani. Hivyo miujiza ya uponyaji hawaitangazi sana kwa sababu kuitangaza sana na kuihusisha na mtu fulani, inakuwa ni kutaka kupokonya utukufu, ukuu na sifa ya Mungu, ambaye ndiye hasa mponyaji.
Scripted Scam
 
Back
Top Bottom