Wengi wakisikia uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, wanadhani ni uchaguzi kama hizi chaguzi tunaazozifanya kuwachagua viongozi wa kijamii.
Mchakato wa Uchaguzi wa kumpata Papa, ni mrefu na mgumu kwa sababu umejengwa kwa msingi wa kiimani kuliko werevu wa kibinadamu. Mambo muhimu yanayoonesha utofauti mkubwa wa uchaguzi wa Papa na Chaguzi nyingine za kawaida:
1. Hairuhusiwi kupiga kampeni yoyote ile.
2. Hakuna majina ya wagombea, iwe ni wao wenyewe kwa kutaka au kupendekezwa.
3. Uchaguzi kura hupigwa mara 2 kwa siku, asubuhi na mchana, kwa kutumia maboksi mawili tofauti.
4. Kila kadinali anatakiwa kuandika jina la mtu anayemfikiria anafaa kuwa kiongozi mkuu wa kanisa, bila ya yeye kujadiliana na mtu mwingine yeyote. Mtu huyo anayestahili kuwa Papa anaweza kuwa miongoni mwa makadinali au hata asiye kadinali alimradi ana daraja la uaskofu.
4. Kila zoezi linapokamilika, kura huhesabiwa, na anayekuwa amependekezwa na makadinali wengi, lazima iwe kuanzia theluthi 2 kwenda juu , ndiye anayetangazwa kuwa Papa.
5. Kama hatapatikana aliyepata theluthi 2 kwenda juu, zoezi hurudiwa kwa siku 3 mfululizo.
6. Kama hata baada ya siku 3, hakuna aliyepata kura kuanzia kura theluthi 2 kwenda juu, waumini wanatengaziwa kuwa papa hajapatikana, bila hata ya kusomewa matokeo, kujua nani wamepigiwa kura na wamepata kura ngapi kila mmoja.
7. Kama Papa hakupatikana baada ya siku 3 mfululizo za kupiga kura, uchaguzi husimamishwa, na makadinali huingia katika maombi maalum. Kisha zoezi hurudiwa.
A. Wakati wote, makadinali wanapoingia kwenye maombi na wakati upigaji kura unaendelea, wakristo wengi huwa nje, nao wakifunga na kuomba ili Mungu amteue kiongozi wake mkuu wa Kanisa la hapa Duniani, kupitia kura zinazopigwa na makadinali.
NB: Historia inaonesha kuwa kuna wakati baada ya kupita miezi 6 bila ya kupatikana papa, waumini waliokuwa nje wakiomba na kufunga, huku kipindi cha baridi kikiwa kimeingia, walikasirika na kwenda kuvunja paa la jengo ambalo makadinali walikuwa wamejifungia. Waumini hao walidai kuwa makadinali walikosa imani ndiyo maana papa ameshindwa kupatikana. Makadinali wakapigwa na baridi kali, baada ya siku chache, Papa alipatikana.
Mpaka sasa, rekodi inayoonesha papa alipatikana kwa taabu sana, baada ya miaka mitatu, ni wa mwaka 1268, kufuatia kifo cha Papa Clement wa 4. Sababu zinazotajwa ni kwamba kulikuwepo makadinali waliotaka kutumia mbinu za kisiasa kuipata nafasi hiyo.
Kati ya mapapa wanaotajwa kupatikama kwa urahisi kabisa, ni Papa John Paulo wa pili, ambaye mzunguko wa kwanza tu, tayari kura zilitimia, na mchakato ukawa umekamilika.
Waumini wakatoliki na wasio wakatoliki, tumwombe Mungu amteue mtumishi afaaye kwa nafasi hiyo ya juu kabisa ya taasisi mojawapo kubwa kabisa ya kidini, yenye nafasi ya kugusa maisha ya watu wengi bila ya kujali imani zao