kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,738
- Thread starter
- #61
Aisee, mimi hufurahia sana Kiswahili cha Wabongo hasa wakisoma taarifa ya Habari, matamshi hayana mbwembwe nyingi, sio lazima waseme taarifa za habari kwa Kiingereza, Kiswahili tosha hivyo. Unajua Kiswahili kama lugha yetu ya Africa Mashariki, Tanzania ichukue jukumu la kuendesha maswala ya lugha, kama ni hiyo Azam ichangamke, wanahabari hao wasafiri hadi nchi kama Marekani watuletee habari kwa Kiswahili.
Kenya Kiswahili kidogo, si chao, wanahabari Wakenya huenda hadi Urusi kutangaza habari, ila ni za kizungu bado.
Azam wafanye bidii kwa hili, Kisha, wafanye bidii kwa muonekana wa picha na sauti ya studio ilainishwe, hapo basi hata mimi ntazikiza Azam, kwa tamaa ya kujua Kiswahili zaidi.
halafu wewe wanjala nina wasiwasi una asili ya tz maana sometimes maneno yako hayafanani na maneno ya wakenya ninaowafahamu.
hata hilo jina lako(wanjala)lina asili ya tz.embu uliza vizuri wazazi wako.