Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania wameokoa Maisha yangu

Sijapenda
Hayo maji yanatoka Gaza umeambiwa?
Mara Mia ungemshukuru sir100😃
 
Assalam Aleykum!

Habari zenu wakuu,
mimi nachukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwenda kwenye Ubalozi wa nchi ya Palestina hapa Nchini Tanzania kwa kuokoa maisha yangu.

Nilikuwa katika zunguka zunguka zangu hapa jijini kutafuta mkate wangu wa kila siku, nikiwa na njaa pamoja na kiu ya maji huku nikiwa
Sina hata senti mfukoni mwangu japo ya kuniwezesha kununua andazi.
Ghafla nikatokea kwenye ubalozi wa Palestina hapa Dar es salaam,
ubalozi huu umeweka maji safi ya kunywa nje ya geti lao, ambapo mwenye uhitaji anaruhusiwa kunywa, kunawa n.k bila kuomba ruhusa,

Kwakweli hili ni jambo kubwa sana kwangu nimeliona,
bila shaka sote tunafahamu ni kiasi gani jua linawaka hapa jijini kwetu,

Kwa kitendo cha ubalozi kuweka maji safi kabisa na salama ya bure kwenye ubalozi wao wameokoa Maisha yangu.
Ni jambo zuri na lenye ubinadamu linalo faa kuigwa hata na balozi zingine ikiwemo ubalozi wa Israeli hapa Tanzania,
na hata taasisi zingine waige mfano huu wa serikali ya Palestina kupitia ubalozi wao hapa Tanzania.
Unaaaafk kwann huitaje israel mbona baloz zngne azjaweka hyo huduma syo huduma ya lazm baloz ya palestina wao wameona watoe bila kulazmishwa na nyumbu yeyote lakn wee unataka shda zako ziwe na wengne kinywa maji futa mdomo acha kelele kama chura
 
Bado tuna hali ngumu kama taifa.
Nchi yenye milima na mabonde yenye maji tele lakini tunanyweshwa maji ma wageni


Eeee Mwenyezi Mungu tusaidie.

Ndio maana chawa wamejaa, wakipewa hata 10k wanakusofia kama Mungu.
Umaskini wa AKILI unaoulindwa kwa wivu mkubwa na ccm unadhalilisha sana utu wa watanzania.
 
Back
Top Bottom