Kuelekea 2025 Ubalozi wa Marekani: Tumeshtushwa na taarifa za kuaminika kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi kuwadhibiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe kwa akili yako unafikiri huyo Balozi wa US atafanyanini? Slavery mentality inakusumbua. Badala ya kuwategemea watz unawaza kuwategemea mabeberu unafikiri watawasaidia kuchukua nchi au?!
Usiwapuuze wala usiwabeze Marekani, wanatufahamu vizuri zaidi kuliko sisi Watanzania tunavyowafahamu wao.

Aidha, Marekani Wana mbinu nyingi sana za kuweza kutudhibiti sisi. Tawala nyingi sana kama siyo zote kabisa zilizopo barani Afrika zinaweza kuhujumiwa kwa urahisi Sana na Marekani, tusiwabeze hata kidogo. Yaani ni Bora tukae kimya bila kujibizana nao hao Watu. Wakiamua kutuhujumu ni kazi ndogo kabisa kwao.
 
Hawajashtushwa na Trump kutaka kuuwawa??

Haya mabeberu bwana, kwa kuzuga tu hayajambo.
 
Ubalozi wetu utoe tamko la kulaani attempted homicide on D Trump. katika kipindi cha kampeni za uchaguzi
Jingalao katika ubora wako. İle ni attempted assassination na sio homicide. Na marekani walishughulikia kikamilifu mpaka mkurugenzi wa secret service alilazimika kujiuzulu kwa sababu ya uzembe
 
Serikali ya Tanzania nayo itoe tamko juu ya shambulio la mgombea wa chama Cha Republic- ndugu D.Trump,unyama -unyama
Kwani wanakatazwa? Ni wewe tu lkn itakuwa ni sawa na kusikia Marekani imepata majanga eti unapereka msaada wa kusaidia waathirika.
 
Usiwapuuze wala usiwabeze Marekani, wanatufahamu vizuri zaidi kuliko sisi Watanzania tunavyowafahamu wao.

Aidha, Marekani Wana mbinu nyingi sana za kuweza kutudhibiti sisi. Tawala nyingi sana kama siyo zote kabisa zilizopo barani Afrika zinaweza kuhujumiwa kwa urahisi Sana na Marekani, tusiwabeze hata kidogo. Yaani ni Bora tukae kimya bila kujibizana nao hao Watu. Wakiamua kutuhujumu ni kazi ndogo kabisa kwao.
Walishashindwa labda umebarehe karibuni ndio maana hujui mambo mengi. Walijaribu miaka ya 70s na 80s wakati huo na mpaka sasa TZ iko na Warusi na Wachina.
 
View attachment 3070012

Tumeshtushwa sana na taarifa za kuaminika kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakamata viongozi wa Chama cha siasa cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, washiriki vijana, na waandishi wa habari kabla ya mikusanyiko iliyopangwa kufanyika Mbeya katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Vijana.

Matumizi haya ya nguvu kupita kiasi yalisababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho cha upinzani kuumizwa vibaya na kuhitajika kulazwa hospitalini.

Uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani, na haki ya kupata mchakato wa haki ni haki za msingi, na serikali zote zina jukumu la kudumisha misingi hii ya kidemokrasia.

Tunaunga mkono wito wa mashirika ya kiraia ya Tanzania na tunaihimiza serikali ya Tanzania kuheshimu katiba yake, na kuhakikisha mazingira salama na wazi ya kisiasa ambapo sauti zote zinakuwa huru kushiriki.
............................

Statement from the U.S Embassy to Tanzania:

We are appalled by credible reports that police used excessive police force during recent arrests of leaders of the political party CHADEMA, youth participants, and journalists in the lead-up to planned gatherings in Mbeya on International Youth Day. The injuries sustained resulted in the hospitalization of some opposition party members.

Freedom of expression, peaceful assembly, and the right to due process are fundamental rights, and all governments have a responsibility to uphold these democratic principles.

We echo the calls of Tanzanian civil society organizations and urge the government of Tanzania to uphold its constitution, and ensure a safe and open political space where all voices are free to participate.

Pia soma=> Ubalozi wa Marekani watoa tamko baada ya Viongozi wa CHADEMA na waandishi kuachiwa. Je, ndio walioshinikiza kuachiwa?
Wapigwa ban washiriki wote katika uovu huu kama ilivyokuwa kwa yule kijana mkorofi.
 
Back
Top Bottom