Tuwe wakweli hivi TPB, NBC na NMB ipi ni bank ya serikali?

Kwanza kwa Historia Mwalimu alipouliza kwa nini wanaiuza NBC alijibiwa kwamba ni kubwa sana kwa ivo haiendesheki. Nakumbuka kwenye hotuba yake moja aliuliza "wanasema wanaiuza kwa kuwa ni kubwa sana, kubwa kuliko Barclays. Can NBC open a branch in London?" Lakini wauzaji wakiongozwa na kina Idd Simba walishupaza shingo mpaka wakaiuza kwa bei ya kutupa na kuigawanya kwa kuanzisha NMB. Miaka ya karibuni Idd Simba alikiri kwamba katika makosa aliyowahi kuyafanya maishani mwake ni kutosikiliza maoni ya Mwalimu kuhusu kukataa kuiuza NBC.

Nguvu iliyonayo NBC si kwa kuwa ina mtaji wa serikali, bali ni kwa kuwa inafanya biashara na serikali. Nani asiyejua kwamba asilimia kubwa ya mishahara ya watumishi wa Umma na serikali inapitia kwenye Benki hiyo. Hata bila ya kusema kwa uhalisia malipo mengi ya serikali ankara zake zinapitia huko. Kama yenyewe iliona gawiwo ni la msingi kwa nini mishahara na hayo mambo mengine yasingepitishiwa TPB ambako ndiyo kuna hisa nyingi za serikali ili gawiwo liwe kubwa sana?

Unapoitafakari hali hii bila ya shaka utakuja kuona ni kwa nini mpaka sasa TTCL si moja wapo mwa makampuni makubwa ya mawasiliano nchini wakati makampuni hayo mengine yalianza kwa kutumia mitambo ya TTCL. Tatizo kubwa si hayo mashirika kutokuleta faida bali ni mfumo unaotumika kuyaendesha. Yanaitwa mashirika ya umma lakini kiuhalisia si mashirika ya umma bali ni taasisi za serikali.
 
Kwa ninavyofahamu Mimi NBC ilibinafisishwa enzi za Benja kwa kampuni ya ABC kutoka South Africa
B4 serikalj ilikua na umiliki wa asilimia 100 bt wakauza hisa nying kwa wazulu kampuni ya ABSA kama sijakosea na kubakiwa na 30% hivo ABSA ndo wakawa wamiliki kwa sababu wao walikua na hisa zaidi ya nusu
Bt pia serikali ina umiliki wake pale
 
Time mkuu... Huo muda wa kusubiri hadi hiyo benki ikue Rais hana. Kama imeshindwa kukua miaka yote hiyo ndio itakua ghafla sasa hivi?
Hili swali ni la msingi sana. Jee hiyo Benki inaendeshwaje? Weledi unaruhusiwa na pia mwenye benki (serikali) anawekeza kiasi gani cha mtaji wa fedha na rasirimali watu kwenye benki hiyo? Wakati fulani TPB ndiyo ilikuwa benki yenye wateja wadogo wadogo wengi kuliko benki nyngine yoyote ile, lakini serikali iliposema mishahara yote ya watumishi wa Umma ipitie NMB TPB ikapata mtikisiko mkubwa sana. Kusema kuisubiri ikue ni kosa lakini kujiuliza kwa nini haikui huo ndiyo weledi na busara ya kawaida ya kibinadamu.

Kama tuna akili timamu ni lazima tujiulize ni kwa nini Benki tunayomiliki asilimia thelasini ya hisa ndiyo inayotupa gawiwo kubwa wakati ile tunayomiliki zaidi ya asilimia sabini inatupa gawiwo lenye thamani ndogo?
 
Coperative Rural Development Bank aka CRDB -- ukisoma tuu hilo jina hupati shida kujua ni bank ya serikali
 
Kati ya 2005 hadi 2011 hawa walikuwa walipaji wakubwa. Hebu tupe data za sasa.

i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);

ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);

ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

xiii. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);

xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5
Zinaongelewa hisa na dividends
 
Cooperative Rural Development Bank aka CRDB -- ukisoma tuu hilo jina hupati shida kujua ni bank ya serikali
Ilikuwa benki ya Serikali wakati huo kabla haijagawiwa kwa waliyo nayo sasa. Na waliopewa hawakuona sababu ya kulibadili jina hilo.
 
Time mkuu... Huo muda wa kusubiri hadi hiyo benki ikue Rais hana. Kama imeshindwa kukua miaka yote hiyo ndio itakua ghafla sasa hivi?
Halafu kuna kiongozi wa miaka Ile angeizika mazima. Hawa viongozi wa Sasa wa TPB wamejitahidi sana
 
Halafu kuna kiongozi wa miaka Ile angeizika mazima. Hawa viongozi wa Sasa wa TPB wamejitahidi sana
Siyo "wamejitahidi" bali wameweza. Ni kama mtoto halali anayelelewa kama mwanaharamu halafu aendelee kuwa na heshima kwa watu wote hata wale wanaomtenda mabaya!!
 
Back
Top Bottom