Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Septemba 25.2024 na kueleza kuhusu Tigo kuhusika na tukio lake la kushambuliwa
Simulizi ya Tukio la kushambuliwa kwake
"Ilichukua takribani wiki moja kama siku tisa (tangu Polisi wamuachilie huru Tundu Lissu bila masharti yoyote, ambapo alokamatwa baada ya kutoa taarifa ya kukamatwa kwa ndege ya Bombadier ya Tanzania nchini Canada), baadaye Septemba saba 2017 ndiyo nikashambuliwa kwa risasi, sasa baada ya kushamhuliwa kwa risasi haya ambayo nimeyasema (kuhusu kile kinachodaiwa kuwa kampuni ya tiGO ilitoa mawasiliano ya Siri kwa Tundu Lissu na kupeleka serikalini ambako anadai kuwa yalisaidia waliofanya jaribuo la kumuua kumfuatilia) tumeyafahamu jana (Jumanne ya Septemba 24.2024) na ushahidi uliotolewa Mahakamani huko nchini Uingereza" -Lissu
Namna TIGO walivyohusika
"Inaelekea tiGO walikuwa wameajiri mtu anayechunguza (yaani mchunguzi wa ndani), waliajiri askari Polisi wa kiingereza aliyekuwa anafanya kazi London Metropolitan Police, walikuwa wameajiri aliyekuwa mfanyakazi wa London Metropolitan Police, sasa siku chache baada ya kushambuliwa huyu Internal Investigater wa tiGO anaitwa MichaeL Clofford akasikia kwenye kikao cha siri kwamba yule jamaa aliyepigwa risasi sisi ndiyo tulitoa data zake, na kwamba sisi ndiyo tulipewa kazi ya kufuatilia" -Lissu"Sasa akaanzisha uchunguzi, kwamba inakuaje kampuni ambayo inapaswa kutunza siri za wateja inakuaje inashiriki kutoa siri za mteja ili auawe, sasa alianza kuchunguza, akachunguza akapeleka taarifa kwa mabosi wake, taarifa ya uchunguzi wake mabosi walipoona kwamba huyu jamaa amefanya uchunguzi sasa hii inaweza kutuharibia baadaye wakamuachisha kazi, sasa Michael Cliffod ameishtaki hiyo kampuni kwa kumuchisha kazi kwa sababu ya kufanya uchunguzi wa tiGO ya Tanzania na kumpa Magufuli (Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) taarifa zangu ili niuawe" -Lissu
"Sasa tangu 2019 walikuwa wanapambana Mahakamani hii kesi ifanyike hadharani au ifanyike faragha, Mahakama ya Uingereza ikasema hii kesi inahusisha viongozi wakubwa, na ina maslahi kwa umma kwa hiyo siyo siri, mimi nimefahamu siku marehemu Ali Kibao alipouawa" -Lissu
Mashtaka kwa Tigo
"Kwa kifupi Millicom (kampuni mama ya tiGO) hawajakanusha hiyo taarifa (taarifa ya kudai kuwa kampuni ya tiGO imetoa taarifa za siri za Tundu Lissu), kwa hiyo Milicom hawapingi (Mahakamani) kwamba walimsaidia Magufuli (Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) kunifanyi upelelezi ili nishambuliwe ili niuawe, Mawakili wamefuatilia na jana (Jumanne Septemba 24.2024 kwa mara ya kwanza 'The Guardiana' ya Uingereza imechapisha hii taarifa" -Lissu
"Sasa hii habari kubwa sana kwa kuwa tunapata mwanya wa kuwajua waliiohusika na waliowawezesha, kesi bado inaendelea na ndio kwanza imetolewa hadharani, huyu Clifford ameanza kutoa ushahidi na matumaini yetu ni mwamba ataeleza zaidi lakini amesema ameandaa ushahidi katika ripoti ya maandishi na amewapa mabosi tiGO anayo zao labda wachome moto na wakiichoma moto itabidi wachome mambo mengi sana na vilevile tutailazimisha tiGO ituambue ilikuwa inawasiliana na akina nani na nani wa serikali ya Tanzani, na nani aliyeomba mawasiliano yangu yafuatiliwe masaa 24" -Lissu
"Itabidi tupewe tuambiwe majina na itakayotuambia majina hayo ni tiGO, sasa kampuni mama si ipo Uingereza tunaanzanao tukiwapeleka kwenye Mahakama za Prof. Juma (Mahakama za Tanzania) hatutaenda kwenye Mahakama za Prof. Juma tunaenda Uingereza, tutakwenda huko walipo na majeshi ya kutosha ya wanasheria wa kimataifa, hii inahitaji watu wa kimataifa zaidi na tukienda huko tumewaambia walianzishe, leo nimezungumza na Bom Amsteederm nimemuambia una mamlaka kamili ya kulianzisha dhidi ya tiGO na serikali ya Tanzania,
Sasa hatujazungumza juu ya madai ya mapesa nafikiri yatakuwa mengi sana" -LissuTundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Septemba 25.2024.
PIA SOMA
-
Tundu Lissu: Aliyeongoza Kikosi cha wauaji walioagizwa kuniua ni Paul Makonda, ndio maana Marekani ilimzuia